Je, ni kweli Marekani na Iran zimesitisha mashambulizi?

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Kiongozi mmoja wa Iran, ameiambia shirika la habari la Reuters, kuwa Iran itasitisha mashambulizi yake iwapo Marekani itasitisha mashambulizi yake, ila bado wana mashaka kuhusu nia ya Washington.

Marekani imesitisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya Iran yaliyodumu kwa siku 13 mfululizo siku ya Jumamosi, Julai 25.

Kiongozi huyo aliye zungumza na Reuters siku moja baadaye, alisema, "Msimamo wa Iran ni mashambulizi kwa mashambulizi ikiwa mashambulizi yatasitishwa, Iran pia itasitisha operesheni zake. Ujumbe huu tayari umefikishwa kwa Marekani."

Kiongozi huyo pia aliongezea kuwa "Kuna mashaka zaidi kuliko matumaini kuhusu kusitishwa kwa mashambulizi."

Kwa mtazamo wao, kusitishwa kwa mashambulizi ni hatua ya kimkakati ya muda, na huenda usidumu.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, pia alidhibitisha siku ya Jumapili kuwa Rais wa Marekani Donald Trump amesitisha mashambulizi dhidi ya Iran ili kutoa nafasi kwa mazungumzo ya kidiplomasia.

Waltz aliiambia Fox News kwamba Trump amekuwa akitoa "nafasi kidogo ya kupumua" na "nafasi zaidi ya kujadiliana" katika mazungumzo hayo.

Waltz hakutoa maelezo kuhusu yaliyokuwa yakijadiliwa katika mazungumzo hayo. Hata hivyo, kumekuwa na utulivu katika mapigano kati ya Iran na Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita.

Pentagon ilisitisha operesheni zake za mashambulizi ya mabomu baada ya karibu wiki mbili za mashambulizi ya anga dhidi ya Iran.

Aidha, hakukuwa na taarifa za mashambulizi yoyote kutoka Iran dhidi ya nchi jirani mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu ya Marekani, Steven Chong, pia alisema siku ya Jumamosi, Julai 25, kuwa "Rais Donald Trump amesisitiza kuwa anapendelea suluhisho la kidiplomasia na kuongezea kuwa, ikiwa Iran itaendelea na shughuli zake za kigaidi katika Mlango Bahari wa Hormuz au dhidi ya washirika wa Marekani, basi wataendelea na mashambulizi.

Marekani na Iran zilikubaliana mwezi Juni tarehe 17 kuhusu Mkataba wa Makubaliano wa vipengele 14 wenye lengo la kusitisha mashambulizi ya kijeshi, kufungua tena Mlango Bahari wa Hormuz na kumaliza vita ndani ya siku 60 zilizofuata.

Hata hivyo, wiki tatu baada ya makubaliano hayo kusainiwa, Iran ilitekeleza mashambulizi kadhaa dhidi ya meli katika mlango wa Hormuz. Marekani ilijibu hatua hiyo na mashambulizi makali ya anga, huku Trump akitangaza usitishaji mapigano 'umekwisha'

Kituo kikuu cha kusimamamia oparesheni za kijeshi za Marekani, CENTCOM, imetekeleza mashambulizi za aina tofauti, katika maeneo tofauti nchini Iran kwa siku 13 mfululizo.

Iran nayo ilijibu kwa kuanzisha mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani katika eneo la Ghuba.

Bei ya mafuta ghafi ya Brent ilipanda na kupita dola 100 kwa pipa, kwa mara ya kwanza tangu mwezi Mei.

Kwa nini mashambulizi yamesitishwa?

Baada ya mashambulizi ya pande zote mbili kusitishwa, taarifa ziliibuka kwamba uamuzi huo ulifanywa binafsi na Donald Trump.

Maafisa wa Ikulu ya Marekani bado hawajaeleza sababu rasmi ya kusitishwa kwa mashambulizi hayo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyokusanywa na BBC Persian, vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa viliripoti kwamba Donald Trump anaepuka kuchochea zaidi mzozo na Iran, "angalau kwa sasa," baada ya kukutana na washauri wake wakuu siku ya Ijumaa.

The New York Times, ikinukuu maafisa wawili waliofahamu kuhusu mkutano huo, iliripoti kwamba hatari ya kupungua kwa akiba ya makombora ya Patriot ya Marekani na silaha nyingine za ulinzi wa anga katika Mashariki ya Kati ilikuwa miongoni mwa sababu kuu za uamuzi huo.

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Marekani aliliambia gazeti hilo kwamba "wanajeshi watatu wa Marekani waliuawa Ijumaa iliyopita nchini Jordan baada ya kombora la balistiki lililotengenezwa na Iran, kuipiga nchi hiyo."

Kwa mujibu wa The New York Times, kuenea kwa vita katika eneo hilo, kutengwa kwa washirika wa Marekani, madhara kwa uchumi wa dunia, kuongezeka kwa mzozo wa nishati na wimbi la wakimbizi ni miongoni mwa masuala mengine yaliyoibua wasiwasi ndani ya utawala wa Trump.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika mkutano na washauri wakuu wa Ikulu ya Marekani ambao unaaminika kuwa na ushawishi katika kubadili msimamo wa Trump, Makamu wa Rais JD Vance na Mwenyekiti wa Wakuu wa Majeshi, Jenerali Dan Kaine, walieleza wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa vita na Iran.

CNN iliripoti, ikisema kwamba Jenerali Kaine alieleza katika mkutano wa Ijumaa kuwa jeshi lina uwezo wa kutekeleza chaguzi zilizopo, lakini akaonya kuhusu madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na hatua hizo.