Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ataongoza kikao cha
dharura cha baraza la mawaziri leo Jumatatu huku moto wa nyika ukikaribia mji
wa Bordeaux, ulioko kusini-magharibi mwa nchi hiyo.
Wimbi jingine la joto linatarajiwa kufanya juhudi za
kudhibiti moto huo unaoendelea kuenea kuwa vigumu. Moto huo kwa sasa uko umbali
wa takribani kilomita 15 (maili 9) kutoka Bordeaux, meya wa mji huo, Thomas
Cazenave, alisema. Awali, alisema hakuna mpango wa kuwahamisha wakazi wapatao
850,000 wa mji huo.
Ufaransa imekuwa miongoni mwa maeneo yaliyoathirika
zaidi, huku hekta 42,000 zikiathirika na moto kusini-magharibi mwa nchi hiyo.
Hilo limeufanya kuwa miongoni mwa moto mkubwa zaidi wa misitu nchini humo tangu
Vita vya Pili vya Dunia.
Kwa jumla, zaidi ya watu wapatao laki mbili na ishirini
wamehamishwa katika eneo la kusini-magharibi mwa Ufaransa.
Kapteni Nicolas Braz, mmoja wa viongozi wa operesheni ya
kuzima moto, amesema moto huo ulikuwa na upepo mkali sana ukiambatana
na vimbunga vidogo”, na kuongeza kuwa ulikuwa “haueleweki na usioweza
kudhibitiwa.
Wakazi wa Le Porge, mojawapo ya miji ya pwani
iliyoathiriwa na moto huo, wameanzisha mtandao wa kujitolea wa kusaidia wazima
moto waliochoka. Wanawapikia chakula
na kuwapa mahali pa kupumzika kati ya zamu zao.
Zaidi ya nyumba 150
zimeharibiwa katika mji huo wenye wakazi 3,500.
Wakaazi wengi wanasema wamehuzunishwa
na tukio hilo ulioathiri misitu yake, wanyamapori na watu waliopoteza vitu
vingi,” alisema Augonnet.
“Kwa sasa, tunazingatia
kuchukua hatua, hivyo hatuna muda wa kufikiria sana. Nadhani sehemu yenye
changamoto itakuja baadaye, wakati wa kuanza tena ujenzi.
Wakati huo huo nchini
Uhispania, moto unaendelea kusambaa, huku zaidi ya watu 90,000 wakihamishwa
kutoka maeneo yanayozunguka Madrid na Ávila.
Takriban hekta 77,000
zimeathiriwa na moto nchini Uhispania, alisema Waziri wa muda wa Ikolojia, Sara
Aagesen, siku ya Jumapili.