Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Shakahola: Mahakama yaendelea kutoa uamuzi wake dhidi ya Mackenzie
Mahakama nchini Kenya imelitaja kanisa linalohusishwa na vifo vya karibu watu mia mbili kuwa ni dhehebu la kidini lenye itikadi kali zinazotabiri mwisho wa dunia, wakati ikitoa hukumu katika kesi hiyo.
Mhubiri aliyejitangaza mwenyewe, Paul Makenzi, pamoja na washtakiwa wengine ishirini na tisa, walifikishwa mahakamani wakiwa wamefungwa pingu na kuwa chini ya ulinzi mkali.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa aliwashawishi wafuasi wake kuacha kutafuta matibabu na kujinyima chakula ili "wakakutane na Yesu".
Jaji amekuwa akisoma hukumu yenye kurasa elfu moja katika chumba cha mahakama kilichojaa watu jijini Mombasa. Kesi hii inafuatia kugunduliwa kwa makaburi ya pamoja katika msitu wa Shakahola, karibu na pwani ya Kenya.