Moja kwa moja, Lissu: “Maneno hayawezi kuwa matendo”

Kwa siku ya tatu hii leo Lissu anaendelea na majumuhisho juu ya kesi inayomkabili baada ya hatua ya ushahidi kumalizika kwa pande zote mbili. Alianza kugusia sheria na kanuni, anaendelea kugusia ushahidi

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Waandishi wa BBC Swahili

  1. Lissu: “Maneno hayawezi kuwa matendo”

    .

    Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu inaendelea leo ikiwa katika hatua ya majumuisho.

    Katika majumuisho yake ya mwisho jana, Tundu Lissu alijikita katika hoja yake; Je, maneno aliyotamka kwenye mkutano wa CHADEMA tarehe 3 Aprili 2025 yanatengeneza kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za Tanzania?

    Lissu alidai kuwa maneno yanayolalamikiwa ikiwemo “tutazuia uchaguzi”, “tutahamasiha uasi” na “tutakinukisha sana” hayajaainishwa kama kosa katika sheria ya uchaguzi wala hayafikii tafsiri ya kosa la uhaini chini ya Kanuni ya Adhabu. Alisema Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2024 imeorodhesha makosa na adhabu zake, lakini haijaweka kuzuia uchaguzi au kuhamasisha kususia uchaguzi miongoni mwa makosa hayo.

    Aliendelea kupinga hoja ya upande wa mashtaka kwamba maneno hayo yalikuwa tishio kwa Serikali kwa sababu uchaguzi unasimamiwa kwa mujibu wa sheria na Katiba. Lissu alisema hata shahidi muhimu wa upande wa mashtaka, PW17, aliyekuwepo kwenye mkutano huo, hakuyataja baadhi ya maneno yanayolalamikiwa katika maelezo yake ya awali na hakusema aliona kosa la uhaini katika mkutano huo.

    Kwa upande mwingine, Lissu alisema mashahidi wa upande wa mashtaka walijenga hoja kwamba maneno hayo yalilenga kuitishia Serikali kwa sababu Serikali ndiyo inayosimamia uchaguzi. Alipinga tafsiri hiyo, akisema hakuna mahali katika maneno aliyotamka ambapo alitaja Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Rais, Makamu wa Rais au viongozi wengine wa Serikali.

    Lissu pia alihamisha hoja kwenye maana ya kisheria ya “nia”, “kitendo” na “uchapishaji”, akisema upande wa mashtaka umejaribu kuyafanya maneno yake yaonekane kama “matendo” ili kujenga kosa la uhaini. Hoja yake ilikuwa kwamba maneno hayawezi kubadilishwa kuwa matendo kwa tafsiri ya upande wa mashtaka bila msingi wa sheria.

    Akitumia pia uamuzi wa Mahakama katika kesi ya Freeman Mbowe, Lissu alisema sheria za jinai zinapaswa kuwa wazi ili kumlinda raia dhidi ya matumizi holela ya mamlaka na kulinda haki ya kutoa maoni.

    Leo, Lissu anaendelea na majumuisho yake ya mwisho, akitarajiwa kuingia zaidi katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka na utetezi kuhusu nia yake, mkutano wa 3 Aprili 2025 na maana ya maneno yaliyotumika. Upande wa Mashataka nao utapata nafasi ya kufanya majumuisho.

  2. KESI YA LISSU INAENDELEA LEO SEPT 25, 2026

  3. Tundu Lissu: Je, haya maneno yanayolalamikiwa ni makosa kwa mujibu wa sheria?

    Lissu: Sasa nataka kufunga hoja yangu kwenye suala hilo na je, haya maneno yanayolalamikiwa ni makosa kwa mujibu wa sheria?

    Ni makosa yanayotambuliwa na sheria majibu ni hilo ambalo nimelionesha hayo maneno yanayolalamikiwa sio makosa ya uhaini wala sio makosa ya jinai nyingine yanayotambuliwa na nchi hii kwa sababu hilo jibu la suala namba 4 ni hapana, maneno yanayolalamikiwa sio makosa kwa mujibu wa sheria za Tanzania achilia mbali uhaini

    Waheshimiwa majaji naomba kwa ruhusa yenu niende kwenye suala namba 5 ambalo linahusu uchapishaji

    Uchapishaji waheshimiwa majaji ni kitendo

    Suala linasema hivi kutamka yale maneno ni kitendo kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2)D cha kanuni ya adhabu?

    Suala hili kwa lugha rahisi upande wa mashtaka unasema kusema ni kitendo ukitoa maneno ni kitendo kwa hiyo suala ni je maneno ni matendo?

    Kwanza naomba nianze kufafanua, huu mkanganyiko umetokea wapi, mkanganyiko huu ni wa kutengeneza makusudi na upande wa mashtaka ili kuhalalisha hoja fulani kifungu cha 39 (2) D kinasema “mtu yeyote ambaye ana nia ya kumchochea mtu au kikundi cha watu kususia shughuli za serikali kwa kuchapisha, kutenda kwa namna yoyote atakabiliwa na uhaini” masharti ya kifunguhicho lazima uthibitishe nia ya kutenda uhaini kwa kuchapisha, au kufanya kitendo cha wazi, sasa kosa langu ni kusema na maneno matupu kwenye uhaini hayatengenezi kosa kwa hiyo ili kunitengeneza kosa ilibidi mawakili waseme maneno yangu ni matendo wangepambana na Katiba hadi ndiyo maana wameitengeneza kwa kusema “mshtakiwa Kwa kitendo chake cha kutamka” kwa hiyo wametafuta namna ya kuhalalisha maneno haya ni kosa wamebadilisha kuwa matendo wanataka kuepeuka masharti ya sheria kwamba maneno sio uhaini wanataka kuepuka kwa kusema maneno ni matendo ndiyo mkanganyiko ulipo

    Na wamefanya kitu kingine wametenengeza maneno mawili tofati

    Nianze na Haya kitendo ni nini na nia nini ?

    Hoja yangu ya kwanza ni kwamba kitendo na nia kwa maana yake ya kawaida yana maanisha kitu kimoja

    Kwenye kiingereza kwa maana nia maana yake ni nini kwa mujibu wa kamusi ya Oxford, KITENDO kimetafsiri kuwa kitu fulani ambacho mtu anakifanya na hiyo kamusi inasema ni sawa na kusema kutenda

    Nia ni nini kwa mujibu wa kamusi ya oxford, NIA ni kitu ambacho mtu anakifanya hivyo NIA ni sawa na kitendo ni kitu kile kile kwa hiyo kifungu cha 39 (2) D kinaposema nia ya kufanya uhaini ni kitendo ambacho mtu anatakikiwa kukifanya sasa hayo maneno mawili kuthibitisha kwamba yanamaanisha kitu kimoja twende kwenye kamusi ya sheria inasema nini kuhusu kitendo, ni kitu kilichofanywa au kinachotekelezwa.

    Matumizi ya kawaida ni kitu fulani kinachofanywa. Kamusi ya kisheria inasema pia ni nia, ikiwa kitendo pia ni nia ni matendo.

    Kama kitendo ni sawa na nia kuwa ni kitu ambacho kinafanywa haiwezi kuwa kitu kilichosemwa maneno hayawezi yakawa vitendo kwa hiyo hii kesi inayonikabili inaposema nilithibitisha nia ya kutenda uhaini kwa matendo yangu ya maneno ni kitu kisichowezekana.

    Maneno hayawezi kuwa matendo..hii hati ya mashtaka ni mbovu sababu imetaja kitu ambacho hakipo kwenye sheria

    Sasa nimetumia kamusi ya Oxford na kamusi ya wanasheria kwa sababu sheria yetu haijafafanua hayo maneno

    Jana wakati naaga nilisema kesi hii vyovyote mtakavyoamua mtetengeneza msingi kwa miaka ijayo na kutoa msimamo juu ya maneno hayo mawili. Hii ni sehemu moja ambapo busara zenu zinahitajika

    Ukitaka kujua hiyo taarifa walioleta hapa hawajui lolote kuna neno altering.

    Altering maana yake kisheria ni nini sheria inasema ni matendo yanayohusiana na kughushi, kufoji

    Ndiyo maana moja wamashahidi nilimuiliza hilo neno altering limetafasiriwa wapi?

    Hilo neno ambalo wamelileta walilitoa kwenye kifungu cha 53 (1) cha sheria ya huduma za Habari.

    Ukitumia altering kwenye sheria ya kanuni ni kufoji ukitaka ya maneno ipo kwenye kifungu 53 ya sheria ya vyombo vya habari

    Swali langu ni unatumiaje neno moja kutoka kwenye sheria moja kwenda kwenye nyingine inawezekanaje sasa Kwakua nimeshtakiwa kwa sheria ya kanuni ya adhabu ni kufoji……

  4. Tundu Lissu: 'Makosa ninayoshtakiwa nayo sio makosa ya uhaini'

    .

    Tundu Lissu: Maneno yanayolalamikiwa ni maneno ya kuzuia uchgauzi, kuvuruga uchaguzi, kuhamasisha watu kuvuruga uchaguzi na mashahidi wote wamezungumzia uchaguzi. Je, hayo maneno ni makosa kwa mujibu wa sheria za uchgauzi Tanzania?

    Jibu la swali hilo linapatikana katika sheria ya uchgauzi wa rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2024 sheria namba moja, sheria hii ndiyo iliyotumika kwa mara ya kwanza katika maafa yaliyofanyika Oktoba 29, ilitungwa itumike katika uchaguzi. Sheria hii ilitungwa kwa ajili hiyo - swali ni je yapo mahali popote kwenye sheria hii makosa ninayoshtakiwa nayo ?

    Jibu lake lipo katika sura ya 7 katika sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya saba kichwa chake cha habari ni makosa na adhabu zake.

    Sheria hii katika sura ya saba imeorodhesha jumla ya makosa 23 na adhabu zake, kuanzia kifungu cha 114 hadi 136 ni orodha ya makosa na adhabu zake.

    Makosa ambayo ukiyatenda unaweza ukashtakiwa ukafungwa au ukapewa adhabu ya kijinai makosa 23.

    Maneno ambayo tunataka tujue kama ni makosa yake ni maneno” tutazui uchaguzi, tutavuruga uchaguzi, tutahamasisha uhasi, yote yale yaliyoimbwa tunataka kujua ni uhaini au ni makosa ya uchgauzi.

    Uzuri wa sheria hii ya uchgauzi imeandikwa kiswahili kila anayejua kusoma kiswahili anaweza kuisoma.

    Kosa la kwanza lipo kwenye kifungu cha 114 inahusu makosa ya uandikishaji wa wapiga kura lipo kwenye kuzuia uchgauzi ? Halipo

    Kosa la pili kifungu cha 115 linaitwa kutumia wadhifa kushawishi watu wengine wasiombe kuwa wagombea lina uhusiano wowote na ninayoshtakiwa nayo?

    Kosa la tatu mwenendo usiofaa kwa mtendaji wa uchaguzi mimi sikuwa mtendaji wa uchaguzi halinihusu

    Kosa la nne kifungu cha 119 kinahusu daftari la wapiga kura na kadi za wapiga kura ni kesi ukiharibu daftari lenyewe linahusika hapa kwenye haya mashtaka? Halihusiki

    Kosa la tano linaitwa mwenendo usiofaa wa maafisa waandikishaji halihusiki sikuwa afisa muandikishaji kifungu cha 120

    Kosa la sita lipo kifungu cha 121 ni makosa yanahusu fomu za uteuzi na karatasi za kura, sijashtakiwa nalo hilo pia halihusiki

    Kosa la 7 lipo kifungu cha 122 matangazo ya uongo ya kujitoa, mtu anatangaza kwamba mgombea amejitoa kwenye kinyanganyiro sijashtakiwa na hilo sihusiki

    Kosa la 8 lipo kwenye kifungu cha 123 ushawishi wa rushwa hilo vile vile sihusiki nalo

    Kwenye kifungu cha 124 kinasema kutoa ushahidi wa uongo au maelezo ya uongo wakati wa uchaguzi, sijashtakiwa kwa kutoa matamko ya uongo kwa hiyo hilo vile vile halinihusu

    Kosa 9 linahusu utunzaji wa siri ukivuruga hizo siri ni kosa kila kitu ni giza ndiyo maana tunataka kuleta mwanga…sijatuhumiwa kuvujisha siri

    Kosa la 10 ni kosa la hongo, takrima au kuhujumu sitatuhumiwa kwa kutoa takrima au hongo kwa hiyo sihusiki

    Kosa la 11 ni kujifanya mtu mwingine unachukua kadi ya mpiga kura ya mwenzako unajifanya wewe ndiyo yeye halinihusu

    Kosa la 12 linaitwa kupoteza sifa kwa kuhumumiwa kwa kosa la rushwa sijashtakiwa kwa kufanya matendo ya rushwa.

    Kosa la 14 watu wanaodaiwa kuwa na hatia ya ushawishi mbaya sijashtakiwa kwa kuwa na ushawishi mbaya

    Kosa la 15 lipo kifungu cha 130 hongo, rushwa na ushawishi mbaya kwa maafisa wa tume, sijashtakiwa kwa kuhonga maofisa wa tume halinihusu

    Kosa la 16 ni hatia ya kujifanya mtu mwingine, mimi ni Tundu Lissu wa miaka yote halinihusu

    Kosa la 17 ni adhabu ya vitendo vya rushwa na vitendo haramu vile vile halinihusu

    Kosa la 18 kuingilia mikutano halali ya hadhara, makosa ninayokabiliwa nayo hayahusu haya

    Kosa 19 ni makosa yanayohusu siku ya uchaguzi, kuvaa nguo za chama siku ya uchaguzi ni kosa, kufanya kampeni siku ya uchaguzi kosa pia, sijashtakiwa kwa kufanya hivyo

    Kosa la 20 linaitwa unyanyasaji wa kijinsia, hilo nalo halinihusu

    Kosa la mwisho la 21 linaitwa kuchafua matangazo ya uchaguzi, wagombea wameweka picha unararua

    Hayo ndiyo makosa kwa mujibu wa sheria ya uchgauzi ukiyafanya hayo ya adhabu zake hakuna kuzuia uchaguzi, hakuna kukinukisha sio kosa, hakuna kufanya uhasi dhidi ya uchaguzi sio makosa na sio makosa kwa sababu kifungu cha 5 cha kanuni ya adhabu kimefafanua makosa ni kitu gani?

    Ni kitendo, jaribio au kutenda kitu ambacho sheria umekiwekea adhabu hayo ndiyo makosa kama hakijawekewa adhabu sio makosa, kama sheria haijakitamka sio kosa, sasa hayo maneno yanayodaiwa ya kihaini sio makosa ya uhaini kwa mujibu wa kifungu cha 39 chote sio na vile vile sio makosa kwa mujibu wa makosa yakiorodheshwa kwenye sura ya 7 kwenye sheria ya uchgauzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya 2024 sio makosa ya jinai popote…huwezi ukachochea mtu kufanya jambo halali unachochea mtu kufanya jambo ambalo ni kosa ukichochea mtu afanye ambacho kile sheria imekataza ni kosa

  5. Lissu: 'Kosa ninaloshtakiwa nalo sio kosa la uhaini'

    Waheshimiwa majaji tulipoenda kwenye mapumziko nilipendekeza tuingie kwenye hoja ya sheria ya uchaguzi…kama ambavyo nimesema kosa la uhaini kama ilivyofafanuliwa kwenye katiba, kosa ninaloshtakiwa nalo sio kosa la uhaini kama uhaini ulivyofafanuliwa kwenye sheria ya kanuni ya adhabu, na sheria hii ndiyo sheria pekee nchini ambayo imefafanua kosa la uhaini ni sheria pekee,

    Kwa hiyo kama haya matendo ambayo nimeshtakiwa nayo hayafiti katika sehemu yoyote katika moja wapo ya matendo 10 ambayo kifungu cha 39 kimeyataja ukifanya haya unakuwa umefanya kosa la uhaini kama matendo haya hayaingii popote na yakiyokatazwa maana yake ni kwamba mimi sijafanya kosa lolote la uhaini, kama sijafanya kosa lolote la uhaini Je, nimefanya kosa lingine lolote kwa mujibu wa sheria za Tanzania? Ndicho ninachotaka nikijadili

  6. Tundu Lissu: 'Majaji nimefungwa bure, nimeonewa mwaka mmoja na nusu gerezani'

    .
    Maelezo ya picha, Tundu Lissu

    Lissu: Majaji nimefungwa bure...nimeonewa mwaka mmoja unusu gerezani mimi ni baba.

    Kuna watu hapa wanachama wanatoka kila sehemu ya Tanzania bara mwenyekiti wao amefungwa gerezani .

    Sasa Majaji kama hayo ninayodaiwa kufanya kwenye kanuni za adhabu ni ugomvi .

    Sasa haya maneno ni makosa kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi, kwenye kanuni ya adhabu hayo.

    Je sheria ya Uchaguzi tuliopanga kuuzuia ni makosa...?

  7. Lissu: Upande wa mashtaka unapaswa kufafanua ni makosa gani niliyofanya

    Lissu : Suala la nne linasema je, hayo maneno yaliyotamkwa na mshtakiwa yanatengeneza kosa lolote linalotambuliwa na sheria za nchi hii na maneno hayo yanaonesha kosa?

    Sababu maneno sio kosa hakuwezi kuwa na kosa hilo ndilo suala nataka nilijibu kwenye hoja hiyo…suala hili lilijitokeza kutokana na tuhuma iliyotolewa na upande wa mashtaka kwamba “Maneno hayo yaliyosemwa yalikuwa ni kosa la jinai” hayo maneno ni makosa?

    Maneno yenyewe yakoje “kwenye mkutano wa 3-4-25 mtuhumiwa alidhirisha nia yake ya kihaini kwa kusema na kuchapisha maneno yafutayo…wanasema hivi msimamo huu unaashiria uwasi ni kweli sababu tunasema tutasimisha iuchaguzi…

    tunakwenda kukinukisha vibaya sana” haya ndiyo maneno yaliyotuleta hapa ndiyo yanadhiirisha nia yake uhaini haya ndiyo maneno yanayodaiwa kuwa ni kosa la jinai….sasa kitu cha kwanza kabisa kuhusu maneno hayo ni kwamba hakuna mahali popote ambapo upande wa mashtaka umeyafafanua hayo maneno hawajasema kuvuruga uchaguzi ni nini na kama ni kosa..

    hawajasema kuhamasiha uhasi ni nini na kwa nini ni kosa…hawajasema kuzuia uchgauzi ni nini na kwa nini ni kosa…hawajafafanua kukinukisha ni nini na kwa nini ni kosa..sio wajibu wangu mshtakiwa mahali popote kuyatolea hayo maneno ufafanuzi na kuonesha kwamba si makosa sio wajibu wangu ni wajibu wa upande wa mashataka kusema hayo maneno yana maana yao na kwa nini wandhani ni makosa sio wajibu wangu kusema hayo maneno sio kosa…

    .sababu hajafafanua wameleta hisia zao juu ya hayo maneno….ushahidi upande wa Mashataka juu ya haya maneno upo kwenye ukurasa 183 hadi 184 kwa PW2

  8. Lissu: Ushahidi wa mashtaka una ndimi mbili kama nyoka

    Lissu

    Lissu: Muhimu zaidi kuhusu shahidi huyu ni kwamba ushahidi wake unaunga mkono ushahidi wa utetezi kwenye masuala yote muhimu kwenye kesi hii, kwenye hilo suala muhimu Pw1, pw16 ushahidi wao umetofautiana kwenye jambo moja kwamba hayo maneno maana yake ushahidi wote wa mashtaka hauaminiki kabisa ndimi mbili kama nyoka.

    Ulimi mmoja unasema uhaini mmoja unasema si makosa, kama ushahidi wa mashtaka hauaminiki kwenye jambo la je kulikuwa nia ya kutenda kosa la uhaini kama ushahidi hauamini kesi inakufa.

    Hoja hii inatosha kumaliza kesi lakini sio hii pekee yake, lakini hiyo dhana ni hoja ya maana kiasi gani.?...ninachotaka kusema ni kwamba kesi ya mashtakiwa kwenye suala hilo imejengwa kwenye hisia kwamba huyu mtu anapanga kuzuia uchaguzi ataitishia serikali hii imejengwa kwenye imani yao kwamba maneno ya mshtakiwa yalipanga kutishia serikali.

    Ni imani, ni msingi hewa kesi imejengwa kwenye msingi wa hewa kwa nini nasema hayo?.. hawa mashahidi na mawakili wao wamerudia sana swali ninalitaka mtafakari jambo moja kwamba ni kweli kwamba serikali ni chombo pekee kinachosimamia sheria kwenye nchi hii?

    Tuzungumze mambo ya wazi kwenye nchi hii kuna sheria ya usimamizi wa mahakama inasimamiwa na nani?

    Inasimamiwa na mahakama haisimamiwi na serikali nchi hii kuna sheria inaitwa ya tume ya utumishi wa mahakama inasimamiwa na mahakama, nchi hii kuna sheria ya chuo cha mahakama Lushoto inasimamiwa na Mahakama.

    Lissu: Uhaini ni kosa pekee ambalo limetajwa katika katiba ya nchi yetu na imesema yafutayo “Uhaini kama unafafanunuliwa na sheria utakuwa kosa la juu kabisa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

    WalionishtakI wanataka unihukumu kifo kwa sababu ya hisia zao kwa sababu wanahisi nililenga kuitishia serikali.

    Mahakama hii kwa misingi hii ya kisheria haiwezi ikawakubalia na usiitikie wIto wao ni wito wa hisia msikubali wito wanaowapa wa kunitia hatiani kwa sababu tu wanahisi nililenga kuitishia serikali.

    Nimezungumzia sana ushahidi wao ushahidi wa utetezi unasema? Mashahidi wangu na ushahidi wangu unasemaje juu ya hii hoja, ushahidi wa utetezi kwenye hii hoja ulikuwa mwepesi na wa moja kwa moja, ushahidi wangu upo kwenye ukurasa wa 589 hadi 590 mtaona kwenye hiyo sehemu DW1.

    Aliimbia mahakama kuwa kikao cha tarehe3 Aprili, 2025 ulipanga kuwaleta pamoja watia nia wote wa chama kutoka kote nchini na ukiitwa kujadili sera ya chama ya ‘No reform No Election’ iliyowekwa na sekretarieti ya chama 21-1-2025 hiyo ndiyo ilikuwa nia….

    Lissu: Lengo langu lilikiwa ni kuelezea changamoto iliyopo kwenye mfumo wetu wa uchgauzi ili waelewe na kuunga mkono sera ya No Reform No Election.

    Hakukuwa na nia yoyote yakutishia, sababu kutishia serikali haikuwa sehemu ya ajenda yangu, sikuwataka watu wafanye vurugu, nilihamasisha kususia uchaguzi mpaka baadhi ya mabadiliko yafanyike.

    Majaji kwenye maswali ya dodoso nilishughulikiwa kwelikweli lakini naomba muangalie kwenye rekodi kama huo ushahidi wangu juu ya nia yangu ya kusema maneno yale umehojiwa popote.

    Wameniuliza mambo mengi lakini juu ya nia yangu kwenye mkutano ule na maneno yangu…Mtaona pia DW2 alihojiwa sana na upande wa mashtaka lakini hakubalisha msimamo wake mtaona kwenye ukurasa wa 691…ushahidi huo huo uliungwa mkono na DW3, ushahidi wa DW3 ulishughulikiwa kweli kweli kwenye suala la nia hakubadilika…ushahidi wote huo wa upande wa utetezi ulihojiwa sana na mawakili wa serikali lakini suala la nia halikuulizwa hata kidogo.

  9. Lissu:Ushahidi wa shahidi PW17 unaunga mkono utetezi

    LISSU

    Lissu: PW17 alisema yafuatayo kuhusu mkutano wa tarehe 3 Aprili, 2025 kikao hicho kilipanga kuwaleta pamoja watia nia wa CHADEMA kujadili mambo yanayohusu uchaguzi na sera ya chama ya ‘No reforms no elections’ mengi yakijadiliwa kwenye kikao hicho lakini kitu kikuu kilikuwa kinahusu sera ya ‘No reform no election’ na jinsi CHADEMA ilivyojipanga kwenye uchaguzi mkuu ujao.

    Nakumbuka walisema bila mabadiliko ya sheria hawatoshiriki kwenye uchaguzi na kwa ziada mwenyekiti wao Tundu Lissu alisema namna walivyopanga kuzuia uchaguzi na maneno ninayoyakumbuka alisema ‘tutazuia uchaguzi tutakinukisha vibaya’ hayo ndiyo maneno ya shahidi aliyesikia hakuna uhaini wala kosa aliloliona.

    Lissu: PW17 pia alihojiwa maswali ya dodoso. Alipiulizwa wewe ulikuwepo? uliona chochote cha kiuhaini na ulikiandika?

    Alisema “Ni kweli kwenye maelezo yangu ya maandishi sikusema maneno yaliyozungumzwa na Lissu.

    Lissu: Maelezo ya PW17 kielelezo D16 hayo maneno tutakinukisha, tuta nini hayapo kabisa kwenye maelezo ya shahidi huyu wa upande wa mashtaka, nilimuiliza kwa nini yeye hakuyasikia haya maneno majibu yake yanasema hivi:

    "Maneno hayo haypo kwenye kielelezo D16, ni kweli kwamba nilikuwa kwenye kikao niliona na kusikia kila kinachoendelea mimi mwenyewe kwenye kielelezo D16 nakumbuka kuelezea kuhusu ‘No reforms no election’ nilipomuuliza kama maneno hayo ni makosa alisema “Viongozi hawakukosea kujadili changamoto zao zinazo wakabili.”

    Angekuwa shahidi wangu tungetegemea kusema hivyo ila huyo ni shahidi wao.

    Kifungu cha 67(1) cha sheria ya ushahidi kinazungumzia ushahidi wa moja kwa moja hicho kifungu kinaitwa “the best evidence rule” kama ni wakuona ni ushahidi wangu aliyeona kama ni wakunusa ni wa shahidi aliyenusa.

    PW17 ni shahid bora ni shahidi aliyeona aliyesikia kila kinachoendelea na alisambaza……yeye ni shahidi bora zaidi nimekaa gerezani mwaka na nusu wakati wakiwa na maelezo ya PW17 nisipozungumza haya kwa ukali mawe yatazungumza.

    PW17 alikuwa shahidi wa mafichoni na mimi ninashida sana na hilo sababu naamini kwenye ukweli ulio wazi, nina shida na hilo kwamba shahidi huyu alitoa ushahidi wake mafichoni lakini sio yeye aliyejipeleka mafichoni.

    Aliwaambia majaji hakuna mtu hata mmoja ambaye alimtishia..huyu shahidi bora aliyetoa ushahidi wake mafichoni hakuwahi kukamatwa kwa kupanga njama.

    Mashahidi wengine ni wahalifu waliopanga kufanya uhalifu PW17 hakukamatwa alikuja kama shahidi huru ushahidi wake unauzito mkubwa sana.

    Lissu: Muhimu zaidi kuhusu shahidi huyu ni kwamba ushahidi wake unaunga mkono ushahidi wa utetezi kwenye maswala yote muhimu kwenye kesi hii, kwenye hilo swala muhimu Pw1, pw16 ushahidi wao umetofauti kwenye jambo moja kwamba hayo maneno maana yake ushahidi wote wa mashtaka hauaminiki kabisa ndimi mbili kama nyoka ulimi mmoja unasema uhaini mmoja unasema si makosa, kama ushahidi wa mashtaka hauaminiki kwenye jambo la je kulikuwa nia ya kutenda kosa la uhaini kama ushahidi hauamini kesi inakufa, Hoja hii inatosha kunaliza kesi lakini sio hii pekee yake, lakini hiyo dhana ni hoja ya maana kiasi gani..ninachotaka kusema ni kwamba kesi ya mashtak kwenye swala hilo imejengwa kwenye hisia kwamba huyu mtu anapanga kuzuia uchaguzi ataitishia serikali hii imejengwa kwenye imani yao kwamba maneno ya mshtakiwa yalipanga kutishia serikali ni imani ni msingi wa hewa kesi imejengwa kwenye msingi wa hewa kwa nini nasema hayo hawa mashahidi Nan mawakili wao wamerudia sanaa swali ninalitaka mtafakali jambo moja kwamba ni kweli kwamba serikali ni chombo pekee kinachosimamia sheria kwenye nchi hii? Tuzungumze mambo ya wazi kwenye nchi hii kuna sheria ya usimamizi wa mahakama inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na mahakama haisimamiwi na serikali nchi hii kuna sheria inaitwa ya tume ya utumishi wa mahakama inasimamiwa na mahakama, nchi hii kina sheria ya chuo cha mahakama Lushoto inasimamiwa na Mahakama

  10. Lissu anaendelea..

    Lissu: PW2 hakubadilika msimamo uleule wa PW1 kukinukisha ni uhaini kwa nini kwa sababu uchgauzi ni kwa mujibu wa sheria na katiba na unasimamiwa na serikali hivyo unatishia serikali PW16 anasema hivi;

    “Mshtakiwa alitaka kuitishia serikali kwa kufanya matendo ambayo alikuwa anayasema, kitendo cha kuitishia serikali kwa kutishia kuzuia uchaguzi na kuhamasisha uhaini kilikuwa ni uhaini kwa sababu ulipanga kuzuia uchaguzi kwa sababu uchaguzi unasimamiwa na serikali.

    Waheshimiwa majaji PW16 akaelezea kwa nini haya maneno anadai ni uhaini “Maneno yakitumiwa na mshatakiwa kama ‘tutazuia uchgauzi, tutahamasiha uasi’ yalilenga kuitishia serikali ambayo imepewa mamlaka ya kulinda nchi” kwa hiyo kujaribu kuzuia uchaguzi ni uhaini haijalishi chochote kwa sababu gani, uchaguzi ni kwa mujibu wa sheria na katiba, na kuzuia ni kutishia serikali.

    PW 16 wakati anahojiwa kufafanua kwenye maswali ya dodoso alisema hivi “Nilichomaanisha kwenye maneno hayo ni kwamba serikali ndiyo ina mamlaka ya kusimamia sheria za nchi kwa hiyo ukisema kwamba utazuia uchaguzi kitendo hicho ni kutishia serikali na kutishia amani na utulivu wa nchi” huo ndiyo ushahidi wa mapolisi waliotoa ushahidi kuhusu suala hilo.

    Msimamo wao ndiyo huo ukitishia uchaguzi ni uhaini kwa sababu uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria na katiba, na serikali ndiyo inayosimamia hivyo kufanya hivyo ni kuitishia serikali.

    Sio kila shahidi wa upande wa mashataka alikuwa na msimamo huo PW17 ambaye ni shuhuda wa macho hakuunga mkono dhana hii ya polisi hivyo PW17 ndiyo shahidi pekee aliyepingana na msimamo huo.

  11. Lissu azungumzia hoja ya "kuitishia serikali"

    Lissu: Nasema hivyo kwa sababu uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa sheria na katiba. Serikali ndiyo inayosimamia sheria, iliitisha serikali kwa kuikata sheria ambayo imewekwa, kuikaidi sheria iliyowekwa na serikali ni kosa.

    Hapa ndipo kesi hii ipo, mtakumbuka kwamba PW1 alikiri kwamba kwenye hayo wanayolalamikia hakuna neno serikali wala hakuna neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala hakuna neno Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wala hakuna maneno rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , wala hakuna maneno Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wala hakuna maneno Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na zaidi ya hapo hakuna Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam na kwa maneno yake ukurasa wa 157.

    Hivyo hicho wanachodai kimetishiwa hakipo. Serikali yenyewe haipo na jina la kiongozi yeyote wa kiserikali lililotajwa huko ni kukiri kwake kwenye maswali ya dodoso.

    Licha ya hayo PW1 aliendelea kusisitiza kuwa serikali ilipangwa kutishiwa akasema “mtu anaposema ‘kukinukisha sana’ umetenda uhaini, maneno kukinukisha sana, kukinukisha vibaya sana, hayapo kwenye sheria isipokuwa ukiyasema umefanya kosa la uhaini kwa sababu serikali ndiyo inayosimamia sheria kwa hiyo unakuwa umetenda uhaini” huo ndiyo ushahidi unawashawishi mtoe hukumu ya kunyonga mtu...hawana hata aibu.

    Lissu: Ushahidi ulipo kwenye ushahidi wa PW1 kusema huu ni uhaini ukawa wimbo wa mapolisi wote na mawakili wote wa serikali waliopo mbele yenu…alipoamua tu kwamba huu ni uhaini hakuna kitu chochote kingebadili mawazo yake.

    Alipoulizwa PW17 aliyekuwa shahidi wa kuona na kusikia kwenye mkutano wala hakuona shida yoyote alipoambiwa hivyo alisema “ni kweli.

    Kwenye maelezo yake PW17 alisema ''mlikuwa mnazungumzia changamoto zinazowakabili na pia mlikuwa mnazungumzia sera yenu ya no reform no election nimesoma maelezo yake na nikaamua kufungua kesi ya uhaini ni mimi ndiye niliyeamua kufungua faili la uhaini''.

    Baada ya kusoma maelezo yote” D16 ni maelezo ya PW17 ambayo PW1 anakiri anayasoma hayajasema kulikuwa na kosa lolote achilia mbali suala la uhaini, hivyo hakuna ambacho kingembadilisha.

    Alipoulizwa na mawakili wa serikali. Unasema juu ya hayo maneno yanaweza kuihusu serikali ya Jamhuri ya Muungano?

    Kumbuka amesema maneno serikali ya Jamhuri ya Muungano hayapo, je hayo maneno yakibaki yanaweza kuihusu serikali pia alisema “Hayo maneno yaliyonukuliwa kwenye maelezo yake kwa muktadha wake yanamaanisha serikali”.

    Akaendelea kurudia maneno kwa vile uchgauzi unafanyika kwa sheria na katiba hivyo hayo maneno serikali yapo kwenye maneno ambayo tunalalamikia hayapo lakini yapo”.

    Kisichokuwepo kinaingizwa huo ni ushahidi wa PW1 alipotoa ushahidi huohuo ndiyo ukawa msimamo wa kila polisi aliyekuja hapa kutoa ushahidi, yeye ndiye aliyewaweka polisi waseme nini kila polisi ushahidi wao unafanana kama sare wanazo vaa.

  12. Lissu anaendelea kutoa majumuisho yake ya mwisho

    Lissu

    Lissu: Waheshimiwa majaji nawashukuru naomba kwamba nikumbushwe jana niliishia wapi?

    Jaji: Jana uliishia kwenye kesi ya Mbowe…ukasema umemaliza sehemu ya sheria kwa hiyo unaelekea kwenye ushahidi sasa.

    Lissu: Nashukuru naomba kabla sijaanza kuzungumzia ushahidi naomba niseme kitu kimoja muhimu ambapo mahakama hii ilikisema kwenye kesi ya Freeman Mbowe, kuhusiana na madhara ya kutokufafanua kwenye hati ya mashtaka,sheria inatakiwa kutoa tahadhari muafaka kwa wale wanaotakiwa kuzifuata, sheria lazima zilinde raia dhidi ya mamlaka holela, sheria ilinde raia dhidi ya matumizi holela ya madaraka, na sheria ilinde haki ya kuzungumza kama si hivyo wote tutakuwa wafungwa, muhimu zaidi mahakama hii ilisema yafuatayo kuhusu sheria za namna hii:

    Lissu: Kama sheria imeandikwa haina lindo na inanyima watu haki zao za kusema inasema mahakama inaweza ikafuta hata kama matendo inayokataza ni ya lazima sababu haki ya watu kusema lazima ilindwe, sasa mahakama ilimalizia hayo kwenye kesi ya Freeman Mbowe…. Je ushahidi?.

    Lissu: Katika mashahidi wa mashtaka ni mmoja tu aliyekuwa kwenye mkutano ambaye ni PW17 na huyo PW17 sio tu alisikia bali alirusha matangazo, Majaji kesi ya upande wa mashtaka imejengwa kwenye nini?

    Imejengwa kwenye ushahidi wa PW1, PW2 na PW16, hawa mapolisi ambao hakuwepo kwenye mkutano, dhana ya kesi hii ni kwamba mimi mshtakiwa nilichochea umma kwa kuzungumza maneno yale kwa lengo la kuitishia serikali kwa sababu moja tu ambayo wameelezea kwenye ushahidi wao.

    Kwa sababu hii serikali ndiyo inasimamia sheria za nchi hii na hivyo kwakuwa ndiyo inayosimamia uchagauzi mkuu, hivyo ni kuitishia serikali ila inayosimamia huo uchaguzi hiyo ndiyo dhana yao kwakuwa uchaguzi unaendeshwa kwa katiba na sheria.

    Nianze na shahidi PW1 alisema juu ya nia ya kushaiwishi umma kuzuia uchaguzi, maneno yake yapo kwenye ukurasa 146 kwenye rekodi za mahakama anazungumzia nini kilichomfanya aamini kuna kosa la uhaini ni maneno ya mshtakiwa “atahamasisha uasi, atazuia uchaguzi, atakinukisha sana, atakinukisha vibaya sana”.

  13. Lissu amtaja Mbowe akijitetea na kifo

    .

    Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, jana aliendelea na mawasilisho yake ya mwisho katika kesi ya uhaini, akijikita katika hoja za kisheria na kuhoji kama maneno anayodaiwa kusema yanaweza kisheria kuunda kosa la uhaini.

    Katika hoja zake, Lissu alisisitiza kuwa hakatai kusema maneno yanayotajwa na upande wa mashtaka, lakini hoja yake ni kama maneno hayo yanatimiza masharti yote yanayohitajika kisheria kuthibitisha kosa hilo.

    “Kuchochea umma” si kosa lililotajwa kwenye sheria, Lissu aliiambia Mahakama

    Moja ya hoja kuu za Lissu ilikuwa kuhusu lugha iliyotumika kwenye hati ya mashtaka. Alisema kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu kinachotumika katika kesi hiyo kinahusu kutishia Serikali kupitia kuchochea mtu au kikundi cha watu, wakati hati ya mashtaka inatumia maneno “kuchochea umma.”

    Kwa mtazamo wa Lissu, tofauti hiyo ni muhimu kwa sababu mahakama haiwezi kutengeneza kosa ambalo halijaainishwa na sheria.

    Pia alihoji shtaka la kutishia “Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, akitaka kujua ni sehemu gani ya Serikali inayodaiwa kutishiwa na kauli zake.

    Lissu pia alipinga ushahidi unaohusisha maandalizi ya mkutano wa CHADEMA wa Aprili 3, 2025. Alisema hakuuitisha wala kuuandaa mkutano huo, bali alikuwa mmoja wa watu walioalikwa. Kwa mujibu wa hoja zake, maandalizi ya mkutano yalifanywa na Sekretarieti ya CHADEMA.

    Hivyo, alitaka mahakama izingatie ushahidi uliotolewa kuhusu nani aliyeandaa mkutano huo na nafasi yake binafsi katika maandalizi hayo.

    Lissu pia alihoji ushahidi kuhusu kualika waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo, akipinga kuhusika na kualika, lakini pia kuchapisha maudhui ya video ya mkutano huo mtandaoni kupitia Jambo TV.

    Wakati wa maswali yake kwa shahidi mkuu wa upelelezi, Lissu alihoji kama yeye ni mfanyakazi, mtangazaji au mpiga picha wa Jambo TV, na kama alikuwa na nywila ya kuingia kwenye mfumo wa chombo hicho.

    Lissu pia alisisitiza kwamba kukiri kusema maneno yanayodaiwa hakumaanishi amekiri kosa la uhaini.

    “Maneno pekee hayatoshi kuthibitisha uhaini”

    Kwa mujibu wa hoja yake, mahakama inapaswa kuangalia maana ya maneno hayo, mazingira yalipotolewa na ushahidi mwingine wa kesi, kisha kuamua kama vipengele vya kosa linalomkabili vimethibitishwa.

    Upande wa mashtaka, kwa upande mwingine, unasema maneno hayo na mazingira yalipotolewa yanaonyesha dhamira ya kutishia Serikali na kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025.

    Katika kuunga mkono hoja zake kuhusu namna sheria inavyopaswa kutumika katika kesi za jinai, Lissu pia alirejea kesi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

    Lissu alitumia mfano huo katika kueleza hoja zake kuhusu namna mahakama inavyopaswa kufuata sheria na ushahidi uliowasilishwa badala ya kuunda kosa ambalo halijaainishwa kisheria.

    Kingine Lissu alichosema jana ni kuhusu uamuzi katika kesi yake kwamba hautamhusu yeye pekee, bali unaweza kuweka msingi wa kisheria ambao mahakama zinaweza kuufuata katika miaka ijayo.

    Alisema kesi yake ni tofauti na kesi mbili za uhaini alizotaja za Grey Likungu Mataka na wenzake ya mwaka 1970, na Hatibu Gandhi na wenzake ya mwaka 1983, ambazo alisema zilihusu madai ya kujaribu kuipindua Serikali au kumuua Rais.

    Kwa mujibu wa Lissu, kesi yake chini ya kifungu cha 39(2)(d) inahusu madai ya kutishia Serikali kwa kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025.

    “Leo nimezungumzia sheria. Naomba tuendelee kesho. Nataka kuzungumzia ushahidi.”Anasema Lissu akihitimisha hoja zake jana.

    Leo Alhamisi Septemba 24, anatarajiwa kuendelea na mawasilisho yake ya mwisho, safari hii akichambua ushahidi uliowasilishwa katika kesi hiyo. Iwapo atakutwa na hatia adhabu ya kosa la uhaini kwa sheria za Tanzania ni kifo.

  14. KARIBU KATIKA MUENDELEZO WA KESI YA UHAINI YA LISSU LEO SEPTEMBA 24, 2026

  15. Lissu: Kuanzia Rais hadi watendaji wa vijiji, ni nani niliyemtishia?

    .

    Lissu: Kuna lengo la kuchochea ili kuitishia serikali. Hakuna lengo la kuzuia uchaguzi wala lengo lingine lolote.

    Kwa hiyo ni wazi, kwa misingi hii tu, nimeshtakiwa kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria.

    Tatizo la tatu ni hili: hiki kinachoitwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni kitu gani ambacho naambiwa nimechochea watu wakitishie?

    Swali hili ni muhimu kwa sababu nilizozieleza.

    Hiki kinachoitwa kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni kitu gani?

    Hilo neno "Serikali ya Jamhuri ya Muungano" si jambo rahisi kama walivyofikiri wakati wanaandaa hati ya kesi hii.

    Serikali ya Muungano imefafanuliwa katika Katiba yetu.

    Imeelezwa katika Sura ya Pili ya Katiba. Sura nzima ya pili ya Katiba yetu inazungumzia serikali.

    Mosi, Rais wa Jamhuri ya Muungano, huyo ni serikali.

    Pili, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

    Tatu, Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri. Sehemu hiyo ya Sura ya Pili nayo vilevile ni serikali.

    Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni serikali.

    Mkurugenzi wa Mashtaka ni serikali.

    Kwa mujibu wa Sura ya Nane ya Katiba, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni sehemu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

    Baraza la Mapinduzi Zanzibar nalo pia ni serikali.

    Yote hayo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

    Lissu: Ili kuonesha kwamba sizungumzi kutoka kichwani, nawaalika muangalie tafsiri ya neno serikali katika Katiba.

    Kwa hiyo upande wa mashtaka ulipaswa kuniambia, katika hicho kitu chote kinachoitwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kuanzia Rais hadi kwa watendaji wa vijiji, waweke wazi hii serikali niliyoitishia ni ipi.

    Je, ni Rais? Waziri Mkuu? Makamu wa Rais? Polisi? Magereza? Watendaji wa vijiji? Ni nani?

    Sasa, Waheshimiwa Majaji, katika mazingira haya, hati hii ya mashtaka inayozungumzia kuchochea umma wakati sheria haitambui umma, na inayosema nimechochea umma ili kuzuia Uchaguzi Mkuu wakati sheria inasema kuchochea mtu au kikundi cha watu kuitishia serikali, hati hii ya mashtaka inakuwaje halali?

    Natambua kwamba kesi ya Freeman Mbowe ni uamuzi wa mahakama hii. Ni uamuzi wa jaji mwingine, na hamfungwi nao.

    Nimejulishwa kwamba tayari ni saa 11.

    Naomba tuendelee kesho.

    Nataka kuzungumzia ushahidi.

    Leo nimezungumzia sheria.

    Unaweza kusoma;

  16. Lissu: Sheria isipotaja kosa, Mahakama haiwezi kulibuni

    .

    Lissu: Nilisema PGO Order No. 1, aya ya 25, inasema:

    "Makosa ni matendo ambayo sheria imeyatamka kuwa ni makosa."

    Kama sheria haijaandika kwamba kuchochea umma ni kosa, basi hakiwezi kuwa kosa.

    Nilisema pia kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya Bahame 6 na wenzake. Mahakama ilizungumzia kanuni ya uhalali na ikasema kwamba:

    "Mtu asihukumiwe kwa kitendo ambacho hakikuwa kosa wakati anapokifanya."

    Nimeshtakiwa kwa kosa ambalo halipo.

    Kwenye kesi ya Bahame 6 na wenzake, washtakiwa walishtakiwa kwa kuingia kinyume cha sheria katika hifadhi ya taifa. Wakati huo, sheria husika ilikuwa tayari imebadilishwa. Walishtakiwa kwa kosa hilo na wakafungwa kwa kosa hilo, lakini Mahakama ya Rufani ikakataa.

    Mimi nakabiliwa na kosa la jinai, kosa la uhaini, ambalo Ibara ya 28(4) imelifanya kuwa miongoni mwa makosa makubwa zaidi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Uhaini, kama unavyofafanuliwa na sheria, ni ule uliofafanuliwa katika kifungu cha 39 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Na kifungu cha 39(2), kilichotumika kunishtaki, kimeeleza ni aina gani ya uhaini ninaoshtakiwa nao.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, nimezungumzia kesi ya zamani kidogo.

    Hapo zamani kulikuwa na kodi ya kichwa.

    Mwanamke mmoja aitwaye Mwanangomeni alishtakiwa kwa kutolipa kodi ya kichwa, wakati sheria haikueleza kwamba wanawake walikuwa na wajibu wa kulipa kodi hiyo.

    Mahakama Kuu ya Tanganyika ikasema kwamba kama sheria haijaelekeza wanawake kulipa kodi, basi haitakuwa kosa kwa wanawake kutolipa kodi hiyo.

    Hiyo ilikuwa miaka 93 iliyopita, wakati wa ukoloni.

    Na kwenye kesi niliyoitaja ya Amin Salum Mrisho ya mwaka 1971, mshtakiwa alipatikana na hatia ya kosa la kawaida la wizi na akahukumiwa kwa vifungo.

    Mahakama Kuu ikasema hapana, kwa sababu usipomshtaki mtu kwa kosa hilo huwezi kumhukumu kwa kosa hilo.

    Naomba nipendekeze kwenu msome maamuzi ya Mahakama Kuu katika kesi iliyozungumzwa sana hapa. Nimepewa hukumu yake tu, lakini imekuwa ikitajwa mara kwa mara.

    Ni kesi ya Freeman Mbowe na wenzake saba dhidi ya Jamhuri.

    Kesi hiyo ni muhimu kwa ushahidi wa kesi hii.

    Nimeitaja hapa kwa sababu ya umuhimu wake wa kisheria.

    Unaweza kusoma;

  17. Lissu: Nimeshtakiwa kwa kosa ambalo halipo kwenye sheria

    .

    Lissu: Waheshimiwa majaji, kifungu cha 39(2)(d) cha sheria iliyotumika kunishtaki kinasema: "Mtu yeyote anayechochea mtu au kikundi cha watu..."

    Shtaka dhidi yangu linasema nimechochea umma. Kwenye kifungu hicho cha 39(2) hakuna umma, kuna mtu au kikundi cha watu.

    Sasa umma ni nini? Hiki kitu kinachoitwa umma ni kitu gani?

    Kanuni ya Adhabu imetoa tafsiri ya neno umma. Tafsiri ya umma kwa mujibu wa sheria hii ina maana ya watu wote wa Tanzania Bara bila kujali uraia wao. Kila mtu aliyeko ndani ya mipaka ya Tanzania Bara, pamoja na watu wanaokaa mahali popote au wanaotumia sehemu yoyote, mfano baa, gesti au vilabu. Ni idadi yoyote ya watu, hata watu ambao hata ufanyeje huwezi kuwajua.

    Huo ndio umma ambao ninatuhumiwa kuuchochea ili uzuie uchaguzi.

    Sheria niliyoshitakiwa nayo inasema unachochea mtu au kikundi cha watu. Mtu anajulikana. Lakini kikundi cha watu ni nini hasa?

    Natumia Oxford Advanced Learner’s Dictionary. Kikundi ni idadi ya watu au vitu ambavyo vipo pamoja katika sehemu moja au vinaunganishwa kwa namna fulani.

    Hiyo ndiyo maana ya kikundi.

    Si watu wote. Watu wote hawawezi kuwa kikundi. Kikundi ni sehemu ya watu wote.

    Nimeshtakiwa kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria.

    Sheria iko wazi kabisa.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, hili kosa lilivyoletwa, hizi taarifa zilivyoletwa, haziwezi kujibika.

    Hakuna mtu anayeweza kujitetea kwa hati kama hii, kuambiwa umechochea watu wote, waliopo uwanja wa ndege na waliopo majumbani kwao.

    Hilo halipo kwenye kifungu cha sheria ya Kanuni ya Adhabu niliyoshitakiwa nayo.

    Waheshimiwa majaji, kwa sababu ya upana wa hilo neno umma, upande wa mashtaka ulikuwa na wajibu wa kisheria kueleza huo umma ni upi katika hati yao ya mashtaka ili kumwezesha mshtakiwa kuandaa utetezi wake.

    Upande wa mashtaka ulitakiwa kueleza huo umma unaodaiwa kuchochewa.

    Hawakufanya hivyo.

    Wameleta kitu ambacho hakipo kwenye sheria.

    Basi turudi kwenye misingi.

    Nilisema kitu kinachoitwa kosa la jinai ni kile kilichokatazwa na sheria. Ni kitendo.

    Kifungu cha 39(2) kimetengeneza kosa la uhaini kwa mtu yeyote anayechochea mtu au kikundi cha watu kuitishia serikali.

    Sheria haijatengeneza kosa la mtu kuchochea watu wote, yaani umma.

    Hakuna sheria ya namna hiyo.

    Hakuna sheria inayosema ukichochea watu wote ni kosa.

    Sheria inasema ukichochea mtu au kikundi cha watu.

    Nimeshtakiwa. Nipo gerezani kwa mwaka mmoja na nusu sasa kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria za nchi hii.

    Ibara ya 13(6)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema:

    "Ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa kitendo chochote ambacho alipokifanya hakikuwa kosa chini ya sheria."

    Nimeshtakiwa kwa kuchochea umma.

    Hakuna sheria inayoitwa kuchochea umma.

    Kuna sheria inayosema kuchochea mtu au kikundi cha watu.

    Nimeshtakiwa kwa kitendo ambacho wala si kosa.

    Unaweza kusoma;

    Tundu Lissu kuanza kujitetea baada ya kukutwa na kesi ya kujibu

  18. Lissu: Ushahidi uliobaki mahakamani una jibu moja tu

    .

    Lissu: Hoja yangu ni kwamba, kwa sababu migongano hiyo inahusu jambo kubwa linalohusu ushahidi wa kwamba mshtakiwa aliwaalika au hakuwalika waandishi wa habari, inaonesha kwamba ushahidi huo hauna thamani yoyote.

    Vipi kuhusu ushahidi wa utetezi kwenye hoja hii? Unasemaje?

    Ushahidi wa utetezi umefuta shaka yoyote kuhusu mshtakiwa kuwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.

    Kama kulikuwa na shaka kwamba mshtakiwa aliwaalika waandishi wa habari, imeondolewa yote na ushahidi wa utetezi.

    Sisi tunasema kwamba waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025 walialikwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, bila shaka yoyote. Wote wamesema hivyo.

    Ushahidi huu upo katika ukurasa wa 592. Ushahidi wa DW2 upo katika ukurasa wa 621 hadi 622. Ushahidi wa DW3 upo katika ukurasa wa 693. Ushahidi wa DW4 upo katika ukurasa wa 800.

    Mashahidi hao wote wanne wamesema kwamba aliyewaalika waandishi wa habari ni DW4, Brenda Rupia.

    Waheshimiwa majaji, ushahidi huo haukuhojiwa hata mara moja.

    Sasa, nini maana ya kutokuhojiwa kwa ushahidi huu?

    Lissu: Kwa sababu hizi, jibu la swali la pili, je, mshtakiwa aliwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025, jibu lake ni hapana.

    Hiyo ni kusema kwamba mshtakiwa hakuwalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.

    Swali la tatu ni hili: Je, mshtakiwa alitengeneza nia ya kuchochea mtu yeyote au kikundi cha watu kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

    Kwa kesi hii, hili ni suala la kufa au kupona, kwa sababu ni moja ya mambo muhimu zaidi katika kesi nzima dhidi yangu.

    Taarifa iliyopo mahakamani inayonishtaki inanituhumu kwamba nilitengeneza nia ya kuhamasisha umma na kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Hiyo ndiyo tuhuma.

    Unaweza kusoma;

  19. Lissu aibua migongano mikubwa kwenye ushahidi wa mashtaka

    ,

    Lissu: PW16, mnakumbuka, ndiye aliyekuwa mpelelezi mkuu wa kesi. PW16 alisema yafuatayo kuhusu nani aliyewaalika waandishi wa habari. Anasema hivi wakati anaongozwa:

    "P na P1 wamesema kuwa walipewa maelekezo na mkurugenzi wao, John Marwa, kwenda kurekodi na kurusha mtandaoni taarifa inayodaiwa... John Marwa alialikwa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA."

    Nilimuuliza: Je, mimi ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA?

    Kwenye ukurasa huo huo mmeandika:

    "Hapana, Tundu Lissu si Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA."

    Lissu: Ni shahidi gani wa upande wa mashtaka ambaye ushahidi wake uaminiwe na mahakama hii kwenye suala muhimu ambalo upande wa mashtaka umeleta?

    Majibu yapo kwenye msimamo wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika kesi ya Khamis Said Hassan. Nilishatoa mfano wake. Mahakama ikisema:

    "Imeamuliwa sasa kwamba migongano na mikwaruzano kwenye ushahidi ni msingi wa kujua ukosefu wa uaminifu."

    Hii mikanganyiko kwenye ushahidi si midogo. Inahusu jambo muhimu. Kwa hiyo, mkanganyiko kuhusu jambo lililotolewa ushahidi, kwamba mshtakiwa ndiye aliyewaalika waandishi wa habari, si mkanganyiko mdogo.

    Unaweza kusoma;

  20. Lissu ahoji ushahidi wa mashtaka kuhusu waandishi wa habari

    .

    Lissu: Ushahidi wa DW2 umeungwa mkono na DW3, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, na DW4, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa CHADEMA. Maafisa wa chama ndio waliandaa huo mkutano.

    Hii tuhuma kwamba ni mimi ndiye niliyeandaa mkutano ni tuhuma ya uongo. Ninachoweza kusema kwa upole kabisa ni kwamba haijathibitishwa kabisa. Nikisema hivyo, nasema kwa upole.

    Upande wa mashtaka haujathibitisha kuwa mshtakiwa ndiye aliyeitisha mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.

    Kwa ruhusa yenu, naomba niende kwenye suala la pili. Je, ni mtuhumiwa ndiye aliyewaalika waandishi wa habari kwenye huo mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025?

    Swali hilo ni muhimu. Kama lengo la mkutano lilikuwa la kihaini, kuwaalika waandishi wa habari ni kitendo cha wazi, na waandishi wa habari waliokuja kwa mwaliko wangu wanakuwa washirika wa kosa hilo. Kosa la uhaini litakuwa linawahusu pia.

    Kwa hiyo, tuhuma hii si ya bahati mbaya wala haijaletwa bure. Ina lengo la kuthibitisha kitendo cha wazi. Wakithibitisha hilo, wanathibitisha uhaini.

    Lissu: Kwenye maelezo ya ziada ya tarehe 22 Septemba 2025 hawakusema waziwazi. Walisema tu kwamba waandishi wa habari walialikwa, lakini hawakusema walialikwa na nani.

    Kwangu mimi, kutokumtaja aliyewaalika waandishi wa habari hakukuwa bahati mbaya. Kulikuwa na nia mbaya kwa sababu, kwenye ushahidi, walileta mashahidi waliosema mimi ndiye niliyewaalika waandishi wa habari.

    PW1, ACP George Bagyemu, alisema hivi wakati anaongozwa kutoa ushahidi wake kuhusu suala hili. PW1 alisema:

    "Ni mtuhumiwa aliwaalika waandishi wa habari ili hotuba yake iweze kusikilizwa na Watanzania, na wasio Watanzania waweze kuiona kupitia Jambo TV."

    Ushahidi wa PW1 uliungwa mkono na PW2, Inspekta John. Ushahidi wake kuhusu hoja hii upo kwenye kurasa za 210 na 221 za kumbukumbu za mahakama.

    Mtakumbuka nilimhoji sana PW1 kuhusu suala hilo. Baada ya maswali, PW1 alisema hivi, katika ukurasa wa 161:

    "Ni kweli kwamba ni wewe ndiye uliyewaalika waandishi wa habari. Sijui ni njia gani ulitumia kuwaalika, lakini ninachojua ni kwamba uliwaalika."

    Na ushahidi huu, kama nilivyoeleza majaji, uliungwa mkono na PW2.

    Sasa, ushahidi huu ulipingwa moja kwa moja na PW16 na PW17.

    Unaweza kusoma;