Jeneral Mstaafu wa Nigeria aliyetekwa afariki dunia

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Jenerali mstaafu wa jeshi la Nigeria ambaye alitekwa nyara na watu wenye silaha kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo amefariki dunia mikononi mwa watekaji wake, jeshi limesema.
Meja Jenerali Rabe Abubakar, ambaye alikuwa msemaji wa jeshi kati ya 2015 na 2017, alitekwa nyara akiwa na mkewe walipokuwa wakisafiri katika jimbo la Katsina mwezi uliopita.
Hakuna kundi ambalo limetangaza kuhuhusika na utekaji nyara huo.
Kutekwa nyara na kifo cha Abubakar kunaangazia changamoto zinazoendelea za kiusalama zinazokabili maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Nigeria, ambapo magenge ya wahalifu wanaofahamika kama "majambazi" mara kwa mara huwateka watu kwa lengo la kupata fidia, kuiba mifugo na kuwashambulia wanavijiji.
Kamishna wa Usalamai na Masuala ya Ndani ya Jimbo hilo, Nasiru Mu'azu, alielezea kusikitishwa kwake licha ya kile alichokiita "juhudi za pamoja zisizo kikomo" za serikali ya jimbo na vyombo mbalimbali vya usalama vya kusaidia kuachiwa kwa jenerali huyo.
"Jenerali huyo mstaafu alifariki kutokana na matatizo ya kisukari na shinikizo la damu," aliwaambia waandishi wa habari wakati akitoa rambirambi zake.
Wakati huo huo, familia ya marehemu imezitaka mamlaka kuimarisha juhudi za kumuokoa mkewe ambaye bado yuko mikononi mwa watekaji nyara hao.
Soma zaidi:

























