Mashambulizi ya Urusi yaua watu tisa nchini Ukraine
Watu tisa wauawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika wimbi la mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine ambapo jengo kubwa la kidini huko Kyiv lilishika moto, ripoti zinasema.
Watu wanne waliuawa katika mashambulizi dhidi ya Kyiv, huku wafanyakazi watano wa uokoaji wakifariki wakati wakijaribu kuzima moto uliosababishwa na shambulio la Urusi katika mji wa Kharkiv kaskazini-mashariki, maafisa wa Ukraine walisema.
Kanisa Kubwa la Dormition la Karne ya 11 liliharibiwa vibaya katika kile Waziri Mkuu wa Ukraine Yulia Svyrydenko alichokiita "shambulio la kikatili kwa watu wetu na urithi wetu".
Wakati huo huo, shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine katika mji wa Tula, kusini mwa Moscow, liliua watu watatu na kuwajeruhi wengine watatu, akiwemo mtoto wa mwaka mmoja, maafisa walisema.
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora yalichoma moto majengo na magari na kuwaacha zaidi ya watu 140,000 katika mji mkuu wa Ukraine bila umeme, Meya wa Kyiv Vitali Klitschko alisema. Sehemu kubwa ya Ukraine ilikuwa imepewa onyo la mashambulizi ya anga siku ya Jumatatu.
Mashambulizi ya Kyiv, ambayo yalilenga majengo kadhaa ya makazi, yalisababisha takriban watu 23 kujeruhiwa, huku wengine watano wakijeruhiwa huko Kharkiv.
Soma zaidi: