Moja kwa moja, Zaidi ya watoto 20 wamefariki kwa moto wa shule nchini DR Congo

Takribani watoto 24 wa shule wamefariki katika mkanyagano walipokuwa wakijaribu kuukimbia moto ulioteketeza shule mbili katika eneo la Bukavu.

Muhtasari

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote

Moja kwa moja

Na Lizzy Masinga

  1. Algeria yakata uhusiano wa kidiplomasia na UAE

    B

    Chanzo cha picha, AFP

    Algeria imesitisha ghafla uhusiano wa kidiplomasia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) siku ya Alhamisi, ikisema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na mfululizo wa vitendo ilivyovitaja kuwa “vya uchochezi au vya uhasama” kutoka Abu Dhabi, bila kutoa sababu mahususi ya uamuzi huo.

    Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE ilisema baadaye siku hiyo kwamba ilitarajia uamuzi wa Algeria wa kuvunja uhusiano wa kidiplomasia ungekuwa wa muda, na kuongeza kuwa Abu Dhabi bado imejitolea kudumisha uhusiano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili pamoja na maslahi yao ya pamoja.

    Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukizorota katika miaka ya hivi karibuni, huku vyombo vya habari vya Algeria vikiikosoa vikali UAE na kuituhumu kwa kujaribu kuchochea mgawanyiko katika eneo hilo.

    “Wizara ya Mambo ya Nje inathibitisha kuthamini kwake wananchi wa Algeria ambao ni ndugu, pamoja na kujivunia uhusiano unaowaunganisha wananchi wa nchi hizo mbili, hususan kupitia jumuiya ya Waalgeria wanaoishi UAE na wageni kutoka Algeria,” wizara hiyo ilisema.

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria ilisema vitendo vya UAE vimefikia hatua ambayo haviwezi tena kuchukuliwa kuwa vinakubalika au kuvumilika, na kwamba Algeria “imetumia njia zote za kuhifadhi uhusiano wa nchi hizo mbili.”

  2. AU yamfuta kazi mwanadiplomasia wa Burundi baada ya kuikosoa Kenya kuhusu wafanyabiashara

    S

    Chanzo cha picha, AU

    Tume ya Umoja wa Afrika (AU) imemfuta kazi mwanadiplomasia mwandamizi wa Burundi aliyekosoa namna Kenya inavyowashughulikia wafanyabiashara wa Burundi, wakati serikali ikiendelea na operesheni dhidi ya raia wa kigeni wasio na nyaraka zinazohitajika.

    Ngoga aliandika kwenye mtandao wa X akieleza wasiwasi wake kuhusu namna wafanyabiashara wa Burundi wanavyoshughulikiwa, akiuliza kwa nini raia wa Burundi wanaonekana kulengwa, wakati raia wa mataifa mengine ya kigeni pia wanaendesha biashara nchini Kenya.

    Kauli zake zilijiri wakati serikali ya Kenya ilipoongeza ukaguzi na utekelezaji wa sheria dhidi ya raia wa kigeni wanaoendesha biashara ndogo ndogo bila kuwa na nyaraka zinazohitajika za uhamiaji na biashara.

    Balozi Fred Gateretse Ngoga, ambaye alikuwa ametumikia Tume ya Umoja wa Afrika kwa miaka 17, alitangaza kujiuzulu muda mfupi baada ya kuhoji kwa nini raia wa Burundi walikuwa wakilengwa nchini Kenya.

    Hata hivyo, Tume ya Umoja wa Afrika imekanusha taarifa kwamba mwanadiplomasia huyo mwandamizi wa Burundi, Fred Gateretse Ngoga, alijiuzulu baada ya miaka 17 ya utumishi. AU imesema alifutwa kazi mara moja kutokana na utovu mkubwa wa nidhamu.

  3. Watu watano wameuawa katika shambulio la anga la Urusi, Ukraine yasema

    Athari za mashambulizi

    Chanzo cha picha, State Emergency Service of Ukraine

    Ukraine imetangaza kwamba watu watano wameuawa na wengine 67 kujeruhiwa baada ya droni ya Urusi kushambulia kituo cha ununuzi katika mji wa Pavlograd, katika mkoa wa Dnipropetrovsk.

    Waziri wa Mambo ya Ndani, Ivan Vihefsky, alisema maduka na magari yalishambuliwa mchana kweupe, “wakati barabara zilikuwa zimejaa watu.”

    Vyombo vya habari vya Ukraine viliripoti kwamba vituo vingine viwili vya ununuzi katika miji ya Zaporizhzhia na Sumy vililengwa na mashambulizi ya anga ya Urusi mapema wiki hii.

    Urusi ilikuwa imetangaza kwamba droni ya majini ya Ukraine ilishambulia mji wa mapumziko wa Sochi Jumatano usiku, na kusababisha watu 28 kujeruhiwa.

    Aidha, watu wengine watatu waliripotiwa kuuawa katika mashambulizi mengine yaliyofanywa na Ukraine.

    Vita vimekuwa vikiendelea kwa nguvu kati ya Urusi na Ukraine tangu Rais wa Urusi, Vladimir Putin, alipoanzisha uvamizi zaidi ya miaka minne na nusu iliyopita.

    Juhudi mpya za kuleta amani zilizoongozwa na wajumbe wa Rais wa Marekani, Donald Trump, mwishoni mwa wiki zinaonekana kuwa zimeleta matokeo machache tu, kufuatia mazungumzo yao na Putin mjini Moscow na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, mjini Kyiv.

    Unaweza kusoma;

  4. Waasi wa Houthi nchini Yemen wameuteka mji wa kimkakati wa Mokha

    Houthi

    Chanzo cha picha, AL MASIRAH/Handout via REUTERS

    Waasi wa Houthi nchini Yemen wameuteka mji wa kimkakati wa bandari wa Mokha, uliokuwa ukidhibitiwa na vikosi vinavyounga mkono serikali vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia, vyanzo vya kijeshi na mashahidi wamesema.

    Kutekwa kwa Mokha kumeacha kundi hilo linaloungwa mkono na Iran likiwa umbali wa kilomita 75 tu kutoka Mlango wa Bab al-Mandab, lango la kusini la njia ya biashara inayounganisha Asia na Ulaya.

    Houthi wamesema hawana tishio lolote kwa usafirishaji wa kimataifa wa majini, lakini wamerudia tishio lao la kulenga meli kutoka Saudi Arabia, ambayo imekuwa ikitegemea Bahari ya Shamu kwa usafirishaji wa mafuta nje ya nchi tangu vita vya Marekani na Israel vilipofunga kwa kiasi kikubwa Mlango bahari wa Hormuz katika Ghuba.

    Kuongezeka kwa mzozo kati ya Houthi, serikali ya Yemen na Saudi Arabia kumechangia kupanda kwa bei ya mafuta.

    Inaripotiwa kwamba mamia ya watu wameuawa na maelfu wameyahama makazi yao tangu Houthi walipoanzisha mashambulizi katika eneo la kusini-magharibi wiki moja iliyopita.

    Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia pia umefanya mashambulizi ya anga katika maeneo ya magharibi mwa Yemen yanayodhibitiwa na Houthi, ukiunga mkono vikosi vinavyounga mkono serikali. Kwa upande wao, Houthi wamefyatua makombora na kutumia ndege zisizo na rubani kushambulia miji na vituo vya mafuta kusini mwa Saudi Arabia.

    Unaweza kusoma;

  5. Tetesi za soka Ulaya: Chelsea, Real Madrid zinamtaka Zubimendi wa Arsenal

    Martin Zubimendi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Martin Zubimendi anaweza kutaka kuondoka Arsenal mwezi Januari baada ya kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza, huku Chelsea na Real Madrid zikimvizia kiungo huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 27. (Teamtalk)

    Mshambuliaji wa Argentina ambaye hana timu kwa sasa Mauro Icardi, 33, yuko tayari kujiunga na Everton baada ya kuondoka Galatasaray mwezi Julai. (Teamtalk)

    Hata hivyo, vyanzo kutoka Everton vimekanusha taarifa zinazomhusisha Icardi na klabu hiyo pamoja na mshambuliaji mwingine aliye huru, Anthony Martial.

    Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 30 alicheza kwa mara ya mwisho akiwa na klabu ya Monterrey ya Mexico. (i Paper)

    Liverpool ilikuwa ikimfuatilia beki wa Italia Marco Palestra, 21, ambaye baadaye alihama Atalanta na kujiunga na Chelsea.

    Liverpool ilishindwa kumsajili kwa sababu ilihitaji kuimarisha zaidi safu yake ya ushambuliaji. (The Athletic )

    Real Madrid imempa kiungo wa Uturuki Arda Guler, 21, mkataba wa miaka sita. Kocha wa Chelsea Xabi Alonso ni miongoni mwa wanaomkubali mchezaji huyo. (Fabrizio Romano via Teamtalk)

    Beki wa Italia Giorgio Scalvini, 22, anayesakwa na Newcastle, amesaini mkataba mpya wa muda mrefu kusalia Atalanta. (Fabrizio Romano)

    Aston Villa iko katika mazungumzo na beki wa kushoto wa Uholanzi Ian Maatsen, 24, kuhusu mkataba mpya ili kubakia Villa Park. (Football Insider)

    Mshambuliaji wa Crystal Palace Eddie Nketiah, 27, anafikiria kubadili uraia wake kutoka England na kuichezea Ghana. (The Standard)

    Mshambuliaji wa Colombia Kevin Viveros, 26, yuko mbioni kusaini mkataba mpya na Athletico Paranaense baada ya vilabu vya Sunderland na Aston Villa kuonesha kumtaka wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (ESPN Brazil via Sunderland Echo)

    Unaweza kusoma;

  6. Zaidi ya watoto 20 wamefariki kwa moto wa shule nchini DR Congo

    Athari za moto

    Chanzo cha picha, Reuters

    Takribani watoto 24 wa shule wamefariki katika mkanyagano walipokuwa wakijaribu kuukimbia moto ulioteketeza shule mbili katika eneo la Bukavu linalodhibitiwa na waasi, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maafisa wa eneo hilo wamesema.

    Watu wazima pia wanaripotiwa kufariki katika moto huo, na kuna hofu kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi katika eneo la Kadutu lenye msongamano mkubwa wa watu.

    Walionusurika wamepelekwa katika hospitali za karibu, huku picha za tukio zikionesha watoto wakiwa wamelala kwenye sakafu za hospitali huku wakiwa kwenye maumivu.

    Takribani nyumba 300 pia zimeteketea katika moto huo, ambao chanzo chake bado hakijajulikana.

    Mamlaka zilizoteuliwa na waasi zilitangaza idadi ya awali ya vifo kuwa 24 Alhamisi jioni, na kuthibitisha taarifa zilizokuwa zimeripotiwa hapo awali. Hata hivyo, kuna hofu kwamba huenda watu zaidi wamefariki.

    Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha watoto wadogo wakiwa wamelala chini.

    Shahidi aliyenukuliwa na shirika la habari la Reuters alisema moto huo ulikuwa umezimwa kufikia mchana, lakini moshi ulikuwa bado ukipanda kutoka kwenye vifusi na mabati.

    Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini na mojawapo ya miji yenye msongamano mkubwa zaidi kwenye maeneo ya milima nchini DR Congo, ilitekwa na waasi wa M23 mwezi Februari mwaka jana.

  7. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu hii leo