Marekani yaichapa Paraguay 4-1, kufanya maajabu mwaka huu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Marekani imeanza vyema kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Paraguay mabao 4-1 mjini Los Angeles na kuongoza Kundi D.
Nyota wa zamani wa Arsenal, Folarin Balogun, alifunga mabao mawili katika ushindi huo mkubwa wa wenyeji wenza wa mashindano hayo.
Katika mchezo mwingine, mwenyeji mwingine Canada ililazimishwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya Bosnia-Herzegovina na kujikusanyia alama moja katika mechi yake ya kwanza ya kundi.
Nayo Mexico ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini, ikiweka wazi dhamira yake ya kufanya vizuri mbele ya mashabiki wake.
Hadi sasa, mataifa yote matatu yanayoandaa Kombe la Dunia 2026 yamecheza mechi zao za ufunguzi, huku Mexico na Marekani zikianza kwa ushindi na Canada ikipata sare. Zitafanya maajabu mwaka huu?



