Kuanzia kuuawa kwa Khamenei hadi tishio la Trump ''kuingamiza Iran": Matukio 10 muhimu ya siku 100 za kwanza za vita

.
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 8

Siku mia moja zimepita tangu vita vilipozuka asubuhi ya Februari 28, 2026, na mashambulizi ya wakati mmoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran; vita vilivyolenga uongozi wa juu wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu kuanzia mwanzo na kuenea haraka hadi kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz, na nchi za Kiarabu katika eneo la Ghuba, na Lebanon.

Taarifa hii inaangazia matukio 10 muhimu za siku 100 za kwanza za vita.

Mbali na kiongozi huyo aliyekuwa na umei wa miaka 86, makamanda kadhaa wakuu wa kijeshi pia waliuawa katika mashambulizi hayo ya siku ya kwanza ya vita. Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza la Kitaifa la Ulinzi, Abdulrahim Mousavi, Mkuu wa Majeshi, Mohammad Pakpour, Kamanda Mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi, na Aziz Nasirzadeh, Waziri wa Ulinzi, walikuwa miongoni mwa watu muhimu zaidi waliouawa.

Tukio hili lilikuwa pigo kubwa zaidi katika muundo wa utawala wa Iran tangu kuasisiwa kwake, na kuanzia siku hiyo vita hivyo vilegeuka kuwa mzozo wa kikanda.

Kuanza kwa vita na kuuawa kwa Ali Khamenei

Alfajiri ya Jumamosi, Februari 28, 2026 Marekani na Israel zilifanya mashambulizi makubwa dhidi ya vituo vya kijeshi, usalama na kisiasa vya Iran.

Moja ya malengo ya kwanza na muhimu zaidi katika mashambulio hayo ilikuwa Jengo la Pasteur huko Tehran, ambapo Ali Khamenei, kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu, alikuwepo.

Jeshi la Israel lilitangaza siku hiyo kwamba limeshambulia kwa wakati mmoja maeneo matatu ambapo wajumbe wa serikali ya Iran walikuwa wamekusanyika, na kwamba "vigogo kadhaa" wa serikali ya Iran "wameuawa" katika operesheni hiyo.

Baada ya saa 20, televisheni ya taifa ya Iran ilitangaza rasmi kifo cha Ali Khamenei.

Shambulio dhidi ya shule ya Munib

Shule ya msingi ya Minab, Mkoani Hormozgan, ililengwa siku ya kwanza ya vita.

Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu 156, wengi wao watoto wa shule wenye umri wa kati ya miaka 7 na 12. Walimu kadhaa na wazazi wa wanafunzi hao pia waliuawa katika shambulio hilo.

Maafisa wa Iran walizilaumu Marekani na Israel kwa kutekeleza shambulio hilo, na ripoti zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa zilieleza kuwa jeshi la Marekani lilihusika katika shambulio hilo, lakini Washington haijakubali rasmi kuhusika.

Shambulio hilo lilikosolewa vikalii ndani ya Marekani na pia kuzua hisia za kimataifa.

Ramani

Chanzo cha picha, Getty Images

Kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika siku za kwanza za vita, Iran ilidhibiti vikali usafiri wa meli kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, hatua ambayo iligeuza mkondo wa vita kutoka kwa makabiliano ya kijeshi na kuwa mgogoro wa nishati ya duniani.

Hatua hii ilikuja baada ya vitisho vya miaka mingi na, kwa mara ya kwanza hatua hiyo, iliruhusu Iran kudhibiri usafiri wa baharini kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz kujibu mashambulizi ya Marekani na Israel.

Mlango wa bahari wa Hormuz ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta na gesi duniani, na hatua ya Iran kuzuia meli kupitia hapo kumesababisha kuongezeka kwa bei ya mafuta, kuongezeka kwa gharama za bima ya meli, na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa meli katika Ghuba ya Uajemi.

Tangu wakati huo, kufunguliwa tena kwa njia hii ya kimkakati ya majini imekuwa lengo kuu la Marekani katika mazungumzo yaliyofuata, lakini sjku 100 baadaye, usafiri katika Mlango wa Hormuz bado haujarejea katika hali ya kabla ya vita.

Baadhi ya wachambuzi wanaamini kwamba vita vya siku 40 viliifanya Iran kutambua zaidi ya hapo awali umuhimu wa mkondo huu kama kichocheo kikuu cha shinikizo.

Kushambuliwa kwa kambi za jeshi la Marekani katika mataifa ya Ghuba

Katika wiki za kwanza za vita, Iran ilifanya mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel, pamoja na malengo kadhaa katika nchi za Kiarabu katika eneo hilo.

Bahrain, Kuwait, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Qatar ziliripoti kuzuia makombora na ndege zisizo na rubani au mashambulizi dhidi ya maeneo yanayohusiana na wanajeshi wa Marekani.

Baadaye, uchunguzi wa idara ya uchunguzi ya BBC Idhaa ya Kiajemi ulifichua kuwa wakati wa vita vya siku 40, Iran ilishambulia kambi 20 za jeshi la Marekani katika mataifa manane, ina huenda idadi halisi ya vituo vilivyoharibiwa inaweza kuwa kubwa zaidi.

Mashambulizi hayo yalisababisha uharibifu mkubwa kwa mitambo ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na rada za gharama kubwa na muhimu na ndege zilizowekwa kwenye vituo hivi.

Wakati huo huo, Marekani na Israel ziliendelea kushambulia malenge mengi ya kijeshi, hifadhi ya makombora, majini na usalama ndani ya Iran.

Katika kipindi hiki, hospitali kadhaa, vyuo vikuu, na vituo vya kiraia pia vililengwa au kuharibiwa katika mashambulizi, ikionyesha mwelekeo wa kibinadamu wa vita.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mojtaba Khamenei: kiongozi wa tatu wa Iran

Mnamo tarehe 8 Machi, vyombo vya habari vya Iran vilitangaza kuwa Mojtaba, mtoto wa Ali Khamenei, ameteuliwa kuwa kiongozi mkuu mpya wa Jamhuri ya Kiislamu.

Kwa kuzingatia hali ya usalama na vita vilivyokuwa vikiendelea, hakuna taarifa nyingi zilizotolewa kuhusiana na muda wa kikao cha wataalamu kilichofikia uamuzi huo, na utaratibu uliotumika kumtambulisha mtoto wa kiongozi huyo wa zamani kuwa mrithi wa baba yake.

Uteuzi wa Mojtaba Khamenei ulikuwa ni moja wapo ya sehemu muhimu za mabadiliko ya kisiasa katika vita hivyo. Serikali ya Iran iliiwasilisha kama ishara ya kuendeleza utawala na kudumisha hali ya utulivu, lakini wakosoaji walisema uamuzi huo unaonyesha jinsi uongozi wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu na IRGC unavyoelekezwa kwa watu wanaomzunguka kiongozi mkuu.

Kuuawa kwa Ali larijani

Mnamo Machi 17, Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Iran, aliuawa katika shambulio la Israel.

Kuuawa kwa Ali Larijani kulionyesha kuwa wigo wa mashambulizi hauko kwa makamanda wa kijeshi pekee, na kwamba viongozi wakuu wa kisiasa pia wako kwenye orodha ya wanaolengwa.

Kuuawa kwake pia kulionyesha hoja kwamba kumuondoa mtu aliyekuwa na jukumu muhimu katika kuunda taratibu za nje na pia za ndani za serikali kutoka kwa muundo wa mamlaka kungefanya maamuzi huko Tehran kuegemea kwenye nafasi ngumu zaidi.

Bwana Larijani aliuawa katika wakati na chini ya mazingira ambapo, bila ya Ali Khamenei, kiongozi wa zamani wa Jamhuri ya Kiislamu, na kisha kutokuwepo kwa kiongozi mpya, ilisemekana kwamba alikuwa "kiongozi" katika udhibiti wa masuala ya serikali.

Shambulio dhidi ya "daraja kuu Mashariki ya Kati" huko Karaj

Tarehe 2 Aprili, Daraja la B1 katika eneo la Bilqan mwanzoni mwa Barabara ya Chalus (Janbazan Boulevard) na Mto Karaj lilivamiwa na wanajeshi wa Marekani na kuharibiwa vibaya. Daraja hilo, ambalo lilipaswa kushikilia rekodi ya daraja "kubwa zaidi" katika eneo la Mashariki ya Kati, limekuwa mfano wa shambulio la miundombinu ya kiraia ya Iran.

Saa chache baada ya sehemu za daraja hilo kuporomoka, Rais wa Marekani Donald Trump alichapisha picha za daraja hilo likilengwa katika ujumbe kwenye Twitter, kuandika: "Daraja kubwa zaidi nchini Iran limeporomoka na halitatumika tena. Mengi zaidi yanakuja!"

Rais wa Marekani pia alionya: "Wakati umewadia kwa Iran kufikia makubaliano kabla mambo hayaharibika!"

Ingawa shambulio dhidi ya daraja hilo lilikabiliwa na athari nyingi, halikuwa shambulio la kwanza la miundombinu ya Iran. Hapo awali, Kiwanda cha Chuma na Isfahan, Kiwanda cha Chuma cha Mobarakeh huko Ahvaz, Kisiwa cha Kharg, na Uga wa Mafuta wa Pars Kusini zililengwa.

Wakati wa vita, mbali na kambi za kijeshi za Marekani, Iran pia ililenga maeneo ya kiraia katika eneo, vikiwemo viwanja vya ndege na vituo vya mafuta na petroli katika nchi za Ghuba ya Uajemi.

Tishio la Trump la "kuiangamiza Iran"

Donald Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Donald Trump

Mnamo Aprili 7, Donald Trump, katika moja ya kauli zake kali dhidi ya Iran, alionya kwamba ikiwa Tehran haitazingatia makubaliano, "itaangamizwa."

Kauli hiyo ilikosolewa vikali kimataifa, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakiitaja kuwa tishio la kutia hofu raia. Msimamo huu, pamoja na kuongezeka kwa shinikizo la kijeshi na kidiplomasia la Marekani, ulizua wasiwasi kuhusu wigo mpana wa vita.

Usitishaji mapigano

Siku moja baada ya vitisho vya Trump ambavyo havijawahi kushuhudiwa, Aprili 8, Iran na Marekani zilikubaliana kusitisha mapigano kwa muda.

Ingawa usitishaji huu wa mapigano ulisababisha kupungua kwa uhasama, makubaliano hayo yalikuwa dhaifu tangu mwanzo.

Mzozo kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz, kuendelea kwa mashambulio ya Israel huko Lebanon, na masharti ya makubaliano haya ya kusitisha mapigano yaliwafanya wahusika kupunguza kiwango cha makabiliano.

Katika wiki zilizofuata, pande hizo mbili zilituhumiana mara kwa mara kuhusu ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mazungumzo ya moja kwa moja nchini Pakistan, kizuizi cha majini cha Iran

Tarehe 11 na 12 Februari, siku chache baada ya kutangazwa kwa mpango wa usitishaji vita, mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja ya ngazi ya juu kati ya Iran na Marekani yalifanyika nchini Pakistan.

Mohammad Baqer Qalibaf, Spika wa Bunge na mmoja wa viongozi wakuu wa Tehran, alizungumza na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance.

Mazungumzo haya hayakufikia makubaliano ya mwisho, lakini yalikuwa na umuhimu mkubwa wa kisiasa, kwani yalikuwa mawasiliano ya kwanza ya moja kwa moja katika kiwango kama hicho tangu kuanza kwa vita. Mkutano huo pia ulizingatiwa kuwa wa kwanza wa maafisa wakuu wa nchi hizo mbili katika kiwango hiki tangu mapinduzi ya 1979.

Wakati huo huo, muendelezo wa operesheni za jeshi la majini la Marekani katika Mlango-Bahari wa Hormuz na shinikizo kwenye njia za meli zilionyesha kwamba diplomasia na shinikizo la kijeshi lilikuwa likiendelea kwa wakati mmoja.

Siku moja baada ya mazungumzo kati ya Bw. Qalibaf na Vance huko Islamabad, Donald Trump alitangaza kuanzisha kizuizi cha majini dhidi ya bandari za Iran na kwamba hataruhusu meli kutoka au kwenda Iran. Tukio hili lilisababisha kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili na pia kuongezeka kwa bei ya mafuta kwenye masoko ya kimataifa. Juhudi hizo, ambazo zinaonekana kuwa na lengo la kuilazimisha Iran kufikia makubaliano ambayo Trump alitaka kwenye meza ya mazungumzo au kufungua Mlango-Bahari wa Hormuz, bado hazijafanikiwa.

Siku 100 Baadaye: Usitishaji mapigano dhaifu, Makabiliano, na ujumbe wa kidiplomasia.

Katika wiki za mwisho za kipindi hikikabiliano ya hapa na pale yameendelea katika Ghuba ya Uajemi.

Mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo ya pwani ya Iran, uvamizi wa ndege zisizo na rubani, na hatua ya Tehran kwa kushambulia maeneo ya Kuwait na Bahrain kama hatua ya kulipiza kisasi yalionyesha kuwa vita havijakoma.

Mlango Bahari wa Hormuz bado haujafunguliwa, na vizuizi vya majini dhdi ya bandari za Iran havijaondolewa; hata hivyo, juhudi za upatanishi badi zinaendelea.

Siku 100 baada ya kuanza kwa vita, eneo hilo limesalia katika hali ya vita na amani; Usitishaji mapigano sio thabiti kiasi cha kuashiria kumalizika kwa mzozo huo, wala wahusika hawako tayari kukubali athari ya kurejea vitani. Katika mazingira kama haya, macho yanabakia kwenye hatima ya mazungumzo na mustakabali wa Mlango-Bahari wa Hormuz.