Atletico Madrid na Juventus
wanamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Noni Madueke.
Chelsea, Arsenal, Liverpool, Manchester
United na Manchester City zote zinaonesha nia ya kumsajili beki wa Barcelona
na Ufaransa, Jules Kounde (miaka 27), huku klabu hiyo ya Hispania ikiwa tayari
kusikiliza ofa kubwa.
Mshambuliaji wa England, Harry
Kane, yuko katika hatua za mwisho za kukubaliana mkataba mpya wa
miaka mitatu na Bayern Munich.
AC Milan inaweza kujaribu tena
kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Joshua Zirkzee (miaka 25), mwezi
Januari kwa mkopo wenye chaguo la kununuliwa moja kwa moja baadaye.
Arsenal, Liverpool na Borussia
Dortmund zinamuwania mshambuliaji wa Fulham, Josh King (miaka 19), ambaye
thamani yake inakadiriwa kufikia pauni milioni 51.
Real Madrid imepanga kusimama
kidete katika uamuzi wake wa kutomuuza mshambuliaji wa Brazil, Endrick (miaka
20), licha ya kuvutiwa naye na Arsenal pamoja na Tottenham Hotspur.
Nia ya Tottenham Hotspur ya
kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez (miaka 26),
inaonekana kuwa ngumu kufanikiwa kwa kuwa Muarjentina huyo bado anatamani
kuhamia Barcelona.
Wawakilishi wa klabu kadhaa za Premier
League na Major League Soccer (MLS) wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji wa timu
ya vijana ya Colombia chini ya miaka 20, Edmilson Herazo (miaka 18),
anayekipiga katika klabu ya Barranquilla.
Liverpool na Manchester United
zinamfuatilia beki wa kushoto wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Alejandro
Balde (miaka 22), ambaye pia anahitajika na Juventus.
Paris Saint-Germain (PSG)
imeonyesha tena nia ya kumsajili beki wa Manchester United na Ufaransa, Leny
Yoro (miaka 20).
Inter Milan na Juventus zote
zinamfuatilia beki wa kati wa Liverpool, Giovanni Leoni (miaka 19), ambaye ni
mchezaji wa kimataifa wa Italia anayechipukia.