Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, uhusiano wa Marekani na Israel unaelekea ukingoni? - Telegraph
Katika uchambuzi wetu leo tunaangazia baadhi ya maoni katika magazeti ya Uingereza Jumapili, likiwemo lile linaloibua maswali ikiwa uhusiano wa Marekani na Israel umeingia katika awamu ya mageuzi makubwa na ya kudumu na lingine ambalo linazungumzia kile ambacho uongozi mpya wa Iran unaweza kujifunza kutokana na vita vya hivi majuzi na Marekani na Israel.
Katika Gazeti la Telegraph tunaangazia taarifa ya Roland Oliphant na David Blair inayouliza: "Je, uhusiano kati ya Marekani na Israel umesambaratika kabisa?"
Waandishi hao wanaanza kwa kueleza hatua ya Trump ya kutomjali mshirika wake Benjamini Netanyahu inaashiria kwamba ushirikiano huo uliokuwa na nguvu sana umefikia hatua ya kuporomoka, lakini Netanyahu huenda amechangia pakubwa mgawanyiko huu.
Waandishi hao wanasema kwamba Netanyahu alijionyesha kama kiongozi mwenye uwezo wa kulinda usalama wa Israel na kushughulikia hilo ipasavyo kuwa ushirikiano na Trump, lakini rais huyo wa Marekani, inaonekana, alikua na mtazamo tofauti kabisa kuhusu sifa za Netanyahu, kwani Trump alishawahi kusema: "Kama si mimi, Israel haingelikuwepo," siku mbili baada ya kutia saini makubaliano ya amani na Iran ambayo yalionyesha kutokujali usalama wa mshirika huyo wa Marekani.
Waandishi wanaamini kuwa kauli hii "isiyo ya kawaida" ndiyo dalili ya wazi zaidi kwamba muungano huo ambao umedumu kwa miongo kadhaa na ulizingatiwa kuwa umeimarishwa hauwezi tena kuchukuliwa kama nzaha.
Ni vyema kutambua kwamba mvutano huu umeibuka mwishoni mwa vita ambavyo pande hizo mbili zilianza pamoja, na muhimu zaidi, Mshirika mwenye nguvu zaidi baadaye kufukia amani na "adui" bila kushauriana na mshirika wake katika vita, ambayo iliweka Israel katika nafasi dhaifu sana, kulingana na makala hayo.
Waandishi hao wanahoji kwamba kutozingatia kwa Trump wajibu muhimu zaidi wa mshirika—kutomwacha mshirika wake—kunazua swali kuu: Je, uhusiano maalum kati ya pande hizo mbili hatimaye umeporomoka?
Kulingana na kifungu hicho, kinachofanya hali hii kuwa tofauti sio tu vitendo vya Trump, lakini pia kuongezeka kwa ukosoaji wa Wamarekani dhidi ya Israel na ndani ya Chama cha Republican na hata miongoni mwa Wakristo wa kiinjilisti. Wakati huo huo, haki ya Marekani inazidi kutilia shaka ushirikiano wote wa kigeni bila ubaguzi, ikiwa ni pamoja na Israel.
Kwa mtazamo wa waandishi wa makala hiyo, sababu kubwa zaidi zinazovuruga uhusiano kati ya nchi hizo mbili huenda zinatokana na kupungua kwa uungwaji mkono wa umma wa Marekani kwa Israel, kwani wafuasi wa chama cha Democratic hasa wameelekea zaidi hasira zao kwa vita vya Gaza vilivyozuka kufuatia shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7, 2023, wakati Warepublican wa mrengo wa kulia wameanza kuhoji ni kwa kiwango gani Marekani imejihusisha na mzozo huo.
Mbali na vita vya Gaza, makala hiyo pia inasema kwamba shambulio la pamoja la Marekani na Israel dhidi ya Iran, ambalo lilipingwa na theluthi moja ya watu wa Marekani, lilizidisha pengo hilo hata zaidi, hasa baada ya "vita vilivyolenga kuipindua utawala wa Iran na kuondoa kabisa tishio la makombora yake, mpango wake wa nyuklia, na ufadhili wake wa ugaidi, ulimalizika kwa Iran kuwa na nguvu zaidi kuliko kabla ya utawala, labda hata utawala wa Iran uliosalia madarakani."
Waandishi hao wanabainisha kuwa, kadiri taswira ya Iran ilivyokuwa ikinusurika katika vita hivyo ilipodhihirika, na baada ya kujibumapigo kwa kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz, vipaumbele vya Marekani vilihamia katika kuzuia kuporomoka kwa uchumi wa dunia na kuwalinda washirika wake katika eneo la Ghuba dhidi ya msururu wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora ya Iran.
Sababu kuu ya Trump ya kufikia makubaliano ya haraka na kumaliza vita ilikuwa ni kuhakikisha Mlango-Bahari wa Hormuz unafunguliwa tena ili bei ya mafuta ipungue. Hata hivyo, Israel iliona udhibiti wa njia ya meli kama suala la dogo ikilinganishwa na uwezo wa Iran wa makombora na nyuklia.
Waandishi wa makala hayo wanaeleza kuwa Marekani itaweka mbele maslahi yake kuliko ya Israel iwapo maslahi hayo yatagongana. Makala hiyo pia inaeleza masharti ya makubaliano ya Trump na Iran yaliwashtua wanasiasa wa Israel na umma, kwani Trump aliiruhusu Iran "kulinda mustakabali wake wa kiuchumi na kifedha, na hata kuupa uongozi wake mpango wa kuendelea mbele."
Hata hivyo, kwa mujibu wa makala hiyo, kuibuka kwa mpasuko huu wakati wa enzi ya Netanyahu "haikushangaza kabisa, kwani yeye mwenyewe amechangi ahilo."
Hatimaye, waandishi wa makala wanahitimisha kwamba kile kinachotokea sasa kati ya Marekani na Israel ni kwamba ushirikiano endelevu zaidi hutegemea masilahi binafsi. Kuhusu maono ya pamoja ya kimataifa hasa washirika wanaopigana vita pamoja wanapaswa kukua karibu.
Je utawala wa Iran utaacha kuwa wa kidini baada ya vita?
Gazeti la The Guardian limeelekeza uchambuzi wake kwa matokeo ya mzozo huo. Mwandishi Patrick Wintour anauliza "Uongozi mpya wa Iran umejifunza nini kutokana na vita vya siku 110?"
Mwandishi huyo anaanza makala yake kwa kubainisha kwamba baada ya kumalizika kwa vita hivyo, swali linabakia jinsi serikali ya Iran itakavyojiendesha, akibainisha kuwa dalili za awali zinaashiria ubabe zaidi na kutanguliza uhusiano na China.
Wintour anasema kwamba mafunzo sahihi ya kiitikadi ambayo uongozi mpya wa Iran unayapata kutokana na vita vya siku 110 yanaashiria kuwa wao ndio wenye uwezo wa kuamua ikiwa mazungumzo yao na Marekani yatafikia makubaliano ambayo yatazuia nchi hiyo kutengeneza silaha za nyuklia, na pia yanaweza kuleta enzi mpya katika uchumi wa Iran, na wakati huo huo kuunda upya Mashariki ya Kati.
Mwandishi anauliza maswali mawili: Je, uongozi wa Iran bado unajumuisha kampeni ya itikadi ya Kiislamu? Na je, kukubalika kwa mkataba wa maelewano kati ya Marekani na Iran kunaweza kuonyesha mwelekeo wa kimantiki?
Wintour anaamini kwamba ombwe lililoletwa na "kutoweka kwa Kiongozi Mkuu wa Irani anayeugua, Mojtaba Khamenei, kunafanya wakati huu kuwa kama mkutano wa kati, haswa baada ya Khamenei awali kuchapisha barua ambayo alisema kwamba anapinga makubaliano hayo kimsingi, lakini alipendelea kukabidhi kwa Rais Masoud Pezeshkian baada ya kupokea hakikisho kwamba ikiwa Marekani haitakubali."
Mwandishi wa makala hayo amenukuu wataalamu wakisema kwamba viashiria vya awali vinaonyesha kuwa uongozi mpya unafanya kazi kwa mujibu wa stratijia mpya adhimu, na kwamba utakuwa wa kimabavu zaidi, wenye mwelekeo zaidi kuelekea China, na utayari zaidi wa kusikiliza, kivitendo, ushauri wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Maandalizi ya mazishi ya Ali Khamenei hayaonyeshi hata kidogo kwamba Iran inakaribia kubadilika na kuwa utawala wa kidunia.
Mwandishi Patrick Wintour anamalizia makala yake kwa kuashiria tatizo jingine ambalo bado halijatatuliwa, nalo ni siasa. Wairan ambao waliweka matumaini yao kwenye ahadi ya Trump kwamba "msaada uko njiani" wanahisi kuaachwa bila njia panda.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi