Kwanini baadhi ya wanawake wanaota ndevu?

Kwanini baadhi ya wanawake wanaota ndevu?
Iliyochapishwa

Hali ya baadhi ya wanawake kuota ndevu kwa wingi inasababu kadhaa likiwemo uwiano usio sawa wa homoni lakini hali zote zinaweza kupatiwa matibabu, hii ni kwa mujibu wa Daktari Selestin Mpili anayehudumu jijini Dar es Salaam.

Dkt Mpili ameiambia hayo BBC baada ya kufanya mahojiano na Herice Mukele mkazi wa Kagera Tanzania ambaye tangu akiwa na miaka 16 anakabiliwa na hali hiyo na watu wamekuwa wakimnyooshea vidole wakidai ana jinsia mbili.

Video: Eagan Salla