Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Newcastle yamtaka Nicolas Jackson, Chelsea yamrejelea Conte
Newcastle imeingia katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, anayetarajiwa kurejea Chelsea mwishoni mwa msimu baada ya Bayern Munich kuthibitisha kuwa haitageuza mkopo wake kuwa uhamisho wa kudumu.(Talksport)
Nottingham Forest inamfikiria kiungo wa Middlesbrough Hayden Hackney, 23, kama mbadala wa Elliot Anderson iwapo ataondoka majira ya kiangazi. Haya ni kwa mujibu wa gazeti la Sun.
Atletico Madrid inatarajiwa kuingia katika ushindani na Tottenham kwa ajili ya beki wa Scotland Andy Robertson, 32, ambaye amesema ataondoka Liverpool mkataba wake utakapomalizika mwezi Juni.Haya ni kwa mujibu wa (Daily Record).
Chelsea inamfikiria kocha wa Napoli Antonio Conte kama mmoja wa wanaoweza kuchukua nafasi ya Liam Rosenior kwa kudumu msimu ujao.(Express)
Kocha wa Porto Francesco Farioli pia yuko kwenye orodha ya Chelsea, ingawa mkataba wake unaendelea hadi 2028 na una kipengele cha kuvunja mkataba cha euro milioni 20. (Nicolo Schira)
Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu England zilizomfuatilia mshambuliaji wa Ubelgiji Mika Godts, 20, baada ya kufunga bao la kuvutia akiwa na Ajax mwishoni mwa wiki.(Teamtalk)
Manchester United inafuatilia hali ya Xavi Simons huko Tottenham huku ikitathmini uwezekano wa kumsajili kiungo huyo wa Uholanzi, 23, katika dirisha la majira ya kiangazi.(Fichajes - in Spanish)
Everton inamuwania kiungo wa Aston Villa na Scotland John McGinn, 31. (Football Insider)
Liverpool inajiandaa kwa ushindani wa kumbakisha kipa wa Brazil Alisson Becker, 33, huku Juventus ikionyesha nia ya kumsajili.(Teamtalk)
Kiungo wa Manchester City Bernardo Silva, 31, anawaniwa na Juventus, Barcelona, Paris Saint-Germain na Al Hilal.(Caught Offside)
Beki wa England John Stones, 31, amejiweka katika rada za Barcelona huku akielekea kumalizia kuchezea Manchester City.(Fichajes - in Spanish)
Liverpool imeanzisha mawasiliano na wawakilishi wa winga wa RB Leipzig Yan Diomande, 19, kutoka Ivory Coast. (Football Insider)
Arsenal pia inamfuatilia mshambuliaji wa Brazil Endrick, 19, ambaye kwa sasa yuko Lyon kwa mkopo kutoka Real Madrid.(Mundo Deportivo - in Spanish)
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid