Kwa nini baadhi ya watu wanashauriwa kujiepusha kula maembe

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Msimu wa joto kali maembe ni moja ya matunda ambayo yanawavutia watu wengi.

Utamu wake huwafanya watu wengi kushindwa kuiacha.

Lakini pamoja na umaarufu wa tunda hili, wataalamu wa afya wanasema si kila mtu anapaswa kunywa juisi au kula maembe kwa wingi.

Kile kinachochukuliwa kuwa "lishe bora" wakati mwingine kinaweza kusababisha matatizo kwa baadhi ya watu kwa mujibu wa mtaalamu wa lishe Dk. Amina Yusuf.

Je, ni virutubisho gani vinapatikana kwenye maembe?

Mtaalamu huyo anasema maembe yana virutubisho vingi vya manufaa vinavyoongeza nguvu mwilini na kuulinda dhidi ya baadhi ya magonjwa.

Virutubisho vinavyopatikana kwenye maembe ni pamoja na:

  • Vitamini C husaidia kuimarisha kinga ya mwili na kutengeneza seli.
  • Vitamin A (beta-carotene): Kirutubisho hiki ni cha manufaa kwa afya ya macho na ngozi.
  • Fiber - Anasema hii inasaidia usagaji wa chakula na kupunguza kuvimbiwa.
  • Potassium - Hii husaidia kudhibiti mapigo ya moyo na shinikizo la damu.
  • Folate (Vitamini B9) - Mtaalamu huyo anasema hii ni muhimu hasa kwa wanawake wajawazito.
  • Magnesium husaidia misuli na mishipa kufanya kazi anasema mtaalam.
  • Antioxidants kama vile Mangiferin, Quercetin, Catechins, na Gallic acid husaidia kulinda seli za mwili dhidi ya uharibifu..

Kulingana naye, viungo hivi husaidia kulinda mfumo wa kinga vizuri sana.

Ni nani hafai kula maembe?

Daktari huyo alisema pamoja na faida hizo za kiafya zinazopatikana kwenye, kuna baadhi ya watu abao wanapaswa kuwa waangalifu wanapokula tunda hili au kutotumia kabisa.

Watu hao ni pamoja na;

Walio na kisukari

Maembe yana sukari, ingawa sio aina inayopatikana katika desserts. Kula maembe kupita kiasi kunaweza kusababisha viwango vya sukari kwenye damu kuongezeka.

"Siwezi kusema kwamba wenye kisukari wasile embe kabisa, lakini wawe makini na kiasi wanachokula, kula kupita kiasi kwa wakati mmoja kunaweza kuathiri jinsi mwili unavyochakata sukari," alisema Dk Amina.

Watu walio na tatizo la figo

Mtaalamu huyo alisema kuwa potasiamu ni miongoni mwa virutubisho vingi katika embe. Ingawa potasiamu husaidia kudhibiti mapigo ya moyo na utendakazi wa misuli, watu walio na upungufu wa figo wanaweza kupata matatizo wakitumia.

Ikiwa potasiamu iko juu sana katika mwili, inaweza kusababisha matatizo ya mapigo ya moyo na matatizo mengine makubwa.

Ingawa ni nadra, kuna watu ambao miili yao inaonyesha kutovumilia embe, alisema.

"Watu wenye tatizo hili mara nyingi hupata muwasho mdomoni au kooni, au vipele kwenye ngozi au

"Kuvimba kwa midomo au kupumua kwa shida wakati mwingine hutokea wakati wa kula maembe."

Watu wanaokabiliwa na matatizo ya matumbo

Maembe yana nyuzinyuzi nyingi, ambazo husaidia kusukuma matumbo.

Hata hivyo, kwa watu wanaosumbuliwa na kuhara au matatizo mengine ya matumbo, kula embe nyingi kunaweza kuzidisha tatizo.

Watu ambao wanataka kupunguza uzani

Ingawa maembe yana manufaa kwa afya, yana kalori zaidi na sukari kuliko matunda mengine, alisema.

"Watu ambao wanataka kupunguza uzito au kupunguza mafuta hawapaswi kutumia maembe au wanapaswa kula kwa kiasi kidogo."

Jinsi ya kula maembe

Mtaalamu huyo alisema kuwa embe lina manufaa kwa afya likitumiwa kwa kiasi.

Alitaja hatua zinazopaswa kuzingatiwa katika ulaji wa maembe kama ifuatavyo;

  • Chagua embe lililoiva vizuri: Mtaalamu huyo anasema kula kipande kimoja au chache inatosha kikidhi mahitaji ya lishe bora.
  • Osha vizuri kabla ya kula.
  • Epuka kula maembe mengi kwa wakati mmoja.
  • Kunywa baada ya kula chakula chenye lishe.
  • Baadhi ya watu wanashauriwa kuepuka kula ganda la embe.