Je, nywele zako zimekuwa zikipukutika polepole ? hii hapa tiba

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Chakula tunachokula ni muhimu katika kutufanya kuwa na afya njema kimwili, na kiakili.

Chakula pia huathiri ngozi na nywele.

Kunyonyoka nywele sio jambo dogo. Kupoteza nywele isivyo kawaida ni ishara ya kwanza kwamba kuna tatizo na haitupasi kupuuza.

Kunyonyoka nywele kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa kama msongo wa Mawazo,vinasaba,mabadiliko ya homoni au matumizi ya dawa Fulani Fulani.

Hivi ndivyo namna ya kutunza nywele kwa njia rahisi pamoja na kujua mambo yanayoathiri nywele zetu.

Wataalamu wanasema kwamba tunaweza kufahamu aina ya chakula tunachokula kwa kuangalia nywele zetu

Chanzo cha picha, Getty Images

Vyakula vinavyofaa

Baadhi ya vyakula vyenye protini nyingi, vitamini B, madini kama chuma na zinki ni muhimu sana kwa nywele zenye afya.

Mpangilio mbaya wa mlo kama vile anorexia (uzito mdogo) na bulimia (kula kupita kiasi) yanahusishwa sana na unyonyokaji wa nywele.

Huenda isijulikane haswa ni mambo gani maalum ya lishe husababisha unyonyokaji wa nywele.

Lakini, kwa mfano, vyakula vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta kwa wingi sio tu husababisha ugonjwa wa moyo, lakini pia matatizo na kuvimba seli. Kwa haya miili hupokea mabadiliko na kukumbwa na kadhia ikiwemo kunyonyoka kwa nywele.

Bado haijafahamika rasmi ni chakula gani hasa kinachosababisha unyonyokaji wa nywele.Lakini kwa mfano

Ni kwa sababu hii tiba nyingi zinazopatikana kwenye soko zinazingatia matokeo yasiyochochea hali hii.

Kwa hivyo vyakula vilivyo na lishe inayozuia tatizo hili kama samaki na mafuta ya mizeituni vinapaswa kupewa kipaumbele.

Baadhi ya mitazamo hushauri kuepuka vyakula vinavyosababisha kiungulia kunaweza kulinda afya ya nywele.

Tafiti nyingi zinaunga mkono hili.

Kwa mfano, wengine husema kwamba kufuata mlo wa Mediterania (mlo ulio na matunda mengi, mboga mboga, nafaka, njugu, mbegu, na mafuta asilia), ambayo yenye sifa nyingi za kuzuia kiungulia, inaweza kusaidia kudumisha afya ya nywele.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Sababu nyingine kuu ya kupoteza nywele ni msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo huongeza kiwango cha homoni ya cortisol katika mwili. Ikiwa homoni hii itatolewa kwa wingi sana au kidogo, kutakuwa na matatizo.

Msongo wa mawazo umekuwa wa kawaida katika maisha ya kila siku. Ikiwa hali hizi za msongo zinaendelea kwa muda mrefu, tatizo la kunyonyoka kwa nywele huanza.

Homoni ya Cortisol inayozalishwa na tezi ya adrenal inahusiana na kupoteza nywele.

Msongo unapopungua, viwango vya homoni hii katika mwili vitarudi kwa kawaida.

Je, inawezekana kudhibiti uzalishaji wa homoni hii kwa kutumia chakula?

Hakika inawezekana.

Homoni ya Cortisol inaweza kuzuiwa kwa kujumuisha parachichi, samaki wenye mafuta mengi, aina fulani za mbegu, vyakula vilivyo na omega-3 fatty acids, na vitamini na madini mbalimbali.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Vyakula vyenye chachu

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Vyakula vilivyochachushwa vimethibitishwa kuwa vyema katika kudhibiti upotevu wa nywele.

Hapa ndipo jukumu la ‘’gut microbiota’’bakteria waishio ndani ya utumbo wanakuwa na umuhimu. Microbiota ni vijidudu ambavyo vinaishi katika mfumo wetu wa kusaga chakula.

Microbiota inahusika katika afya na magonjwa yetu. Microbiota huingiliana na virutubisho tunavyotumia.

Microbiota katika miili yetu hutofautiana kulingana na chakula tunachokula.

Mfumo wetu wa mmeng’enyo wa chakula na urutubishaji wa lishe katika miili yetu hutegemea idadi ya microbiota.

Kwa mujibu wa idadi yao, ishara mbalimbali za kemikali na kimmeng’enyo wa chakula hutolewa katika mwili.

Husaidia pia kukabiliana na msongo wa mawazo.

Ikiwa lishe yetu ni tofauti, ndivyo ilivyo hata bakteria kwenye utumbo.

Kwa hivyo kutumia vitu kama mtindi, kefir pamoja na vyakula vingine vilivyochacha vinaweza kusaidia kuimarisha afya ya nywele.

Ukifuata haya, nywele zako zitakuwa na afya.

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha San Jorge Sayansi ya Afya PDI Kitivo Pilar Argento Arizona.

Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Yusuf Jumah