Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Tottenham inamfukuzia Osimhen Galatasaray

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Klabu ya Tottenham imefanya jaribio la awali la kumsajili mshambuliaji wa Galatasaray, Victor Osimhen (27), kwa dau la hadi pauni milioni 55, lakini mabingwa hao wa Uturuki wanataka pauni milioni 65 kwa mchezaji huyo wa Nigeria. (Caught Offside)

Kiungo wa Newcastle na Brazil, Bruno Guimaraes (28), anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Arsenal katika dili lenye thamani ya karibu pauni milioni 80. (Athletic - usajili unahitajika)

Atletico Madrid inatafakari uwezekano wa kumsajili winga wa Manchester City, Jack Grealish, huku Everton na Aston Villa pia wakifikiria kuwasilisha ofa kwa Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sun)

Atletico Madrid inafikiria kumsajili winga wa Manchester City, Jack Grealish, huku Everton na Aston Villa pia zikitathmini uwezekano wa kuwasilisha ofa kwa mchezaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30. (Sun)

Tottenham imefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Liverpool, Cody Gakpo, lakini klabu yake ya Liverpool haina mpango wowote wa kumuuza mchezaji huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 26. (Teamtalk)

Kipa wa Braga, Lukas Hornicek (24), amekamilisha vipimo vya afya na anatarajiwa kujiunga na Newcastle baada ya kipengele cha kuvunja mkataba wake chenye thamani ya pauni milioni 25.7 kulipwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech. (Mail)

Hull City inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Nice, Mohamed-Ali Cho, aliye na umri wa miaka 22, kwa ada ya takriban pauni milioni 17 ili kumpata mshambuliaji huyo wa Ufaransa. (L'Equipe)

Hull Citypia iko mbioni kumsajili beki wa Australia, Lucas Herrington, 18, kutoka klabu ya MLS ya Colorado Rapids kwa pauni milioni 17. (Sun)

Wachezaji wawili wa Real Madrid, Gonzalo Garcia (22) na Cesar Palacios (21), wamefanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Fulham kufuatia makubaliano ya uhamisho wa kudumu kwa mshambuliaji na kiungo hao raia wa Uhispania. (Sky Sports)

Hull inatarajiwa kumenyana na Rangers na Cardiff City kanyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Norway, Jens Hjerto-Dahl, 20, kutoka Tromso. (Mail - inahitaji usajili)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi