Trump amchagua mkuu wa ujasusi kuendesha kikosi kazi kipya cha Akili mnemba
Rais wa Marekani Donald Trump amemteua mkurugenzi wa ujasusi wa kitaifa kama mkuu wa kikosi kazi kipya kuhusu akili mnemba ambacho, alisema, kitaratibu ushiriki wa serikali na watumiaji, makampuni na "mashirika ya kidini".
Jay Clayton ataongoza kikosi kazi ambacho kimekosolewa na watu kama Seneta wa chama cha Democratic Elizabeth Warren ambaye ametaka udhibiti wa akili mnemba(AI).
Trump amekataa wazo la sheria kudhibiti maendeleo ya teknolojia licha ya mjadala kuhusu hatari zinazoweza kutokea za akili mnemba na maana yake kwa binadamu.
Wiki iliyopita, rais na wakuu wa makampuni makubwa ya akili mnemba walisaini hati ya "kimaadili", na kuwafanya wawe na jukumu la kuhakikisha usalama wa teknolojia yao wenyewe.
Trump ambaye anajaribu kwa upande mmoja kubadilisha jina la AI kama "akili ya hali ya juu", aliandika kwenye mitandao ya kijamii: "Kikosi cha Akili cha Juu kitaratibu ushirikiano wa serikali ya shirikisho na watumiaji, makundi ya maslahi ya umma, mashirika ya kidini, watoa huduma muhimu za miundombinu, na makampuni ya Akili ya Hali ya Juu."
Pamoja na Clayton, mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Usalama Andrew Ferguson, mkuu wa tume ya biashara ya shirikisho, atakuwa kwenye kikosi kazi pamoja na Emil Michael, waziri msaidizi wa ulinzi wa utafiti na uhandisi.
Itaripoti moja kwa moja kwa Trump na Mkuu wa wafanyakazi wa Ikulu ya White House Susie Wiles.
Trump amepinga aina yoyote ya kushuka kwa maendeleo ya Akili mnemba. Alisema Marekani inaongoza mbio hizo mbele ya China, akiongeza: "Na, kusema ukweli, nataka kuendelea hivyo kwa sababu yeyote anayeshinda katika Akili mnemba ndiye mshindi."
Unaweza pia kusoma: