Habari za hivi punde, Navanethem "Navi" Pillay atangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2026

Chanzo cha picha, Getty Images
Ameshinda kwa juhudi zake za kukuza amani na sheria za kimataifa, amesema Mwenyekiti wa Kamati ya Nobel ya NorwayJørgen Watne Frydnes
Navi Pillay "amepanua kwa kiasi kikubwa wigo na athari za sheria ya kimataifa," Jørgen Watne Frydnes anasema.
Ameongeza kuwa kuwa Pillay ameongoza njia ya "amri ya kisheria ya kimataifa iliyo pana zaidi," akisema alifanya hivyo kwa ujasiri wa kipekee.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Nobel ya Norway ameendelea kusifu kazi yake, akisema alianza kama wakili nchini Afrika Kusini akikabiliwa na ubaguzi mkubwa.
Anasema ana "dira thabiti ya maadili".
Historia ya Tuzo ya Amani ya Nobel
Tuzo ya Amani ya Nobel imetolewa mara 106 kwa washindi 143, wakiwemo marais wanne wa Marekani - Theodore Roosevelt , Woodrow Wilson , Jimmy Carter na Barack Obama.
Malala Yousafzai aliweka historia kama mpokeaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea - akishinda Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2014 akiwa na umri wa miaka 17 pekee.
Mnamo 1973, mwanasiasa wa Vietnam Le Duc Tho alishinda tuzo hiyo "kwa kujadiliana kwa pamoja kuhusu kusitisha mapigano nchini Vietnam mnamo 1973" - lakini alikataa kuikubali kwa misingi kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yalikuwa yamekiukwa.
Watu binafsi 112 wameshinda Tuzo hiyo na Nobel huku mashirika 31 yakishinda Tuzo hiyo ikiwa ni pamoja na Nelson Mandela, Martin Luther King Jr na Mother Theresa.
Unaweza pia kusoma:



























