uchunguzi wabaini kuwa madada watatu waliozama baharini nchini Uingereza walijiua

Chanzo cha picha, Poolisi wa Sussex
Madada watatu waliozama baharini karibu na Brighton nchini Uingereza walijiua, mchunguzi wa vifo amethibitisha.
Jane Adetoro, 36, Christina Walters, 32, na Rebecca Walters, 31, walikuwa wakiishi "maisha ya faragha sana" kufuatia kifo cha mama yao, ambaye alizama majini mwaka wa 2010, mchunguzi mkuu wa vifo Penelope Schofield alisema.
Mnamo tarehe 11 Mei, wanawake hao ambao wote walikuwa wakiishi pamoja huko Greenford, London walitembelea eneo la Birmingham karibu na mahali ambapo mama yao alifariki kabla ya kusafiri siku iliyofuata hadi ufukweni mwa Brighton, ambapo walizama katika hali mbaya ya baharini mapema asubuhi tarehe 13 Mei mwaka huu. Mchunguzi wa vifo alisema hawakuweza kuogelea.
Baba yao Joseph Jacobsen alisema lilikuwa jambo la kuhuzunisha kuwapoteza "binti zangu wote watatu wapendwa".
Alikuwa miongoni mwa wanafamilia waliofuatilia kesi hiyo kupitia video.
Katika taarifa ya hisia iliyosomwa kwa niaba yake, alisema aliwaona binti zake wakikua kutoka wasichana wadogo hadi wanawake warembo na werevu "wenye nafasi maalum moyoni mwangu".
Alisema: "Hakuna maneno yanayoweza kuelezea vya kutosha uchungu wa kufiwa na mtoto."
"Kuwapoteza binti zangu wote watatu wapendwa ni huzuni kubwa kuliko kitu chochote ambacho ningeweza kufikiria."
Hakuweza kuelewa ni kwa nini maisha ya binti zake yaliisha ghafla hivyo, na alitumaini kwamba wangeungana tena na mama yao "katika maisha ya milele ya uangalizi wa Mungu", aliongeza.
Unaweza pia kusoma:































