Wawakilishi wa Marekani wako Uswisi huku wa Iran wakiwa safarini kuelekea huko

Chanzo cha picha, Reuters
Vance: Jared Kushner na Steve Witkoff wako Uswisi kwa mazungumzo
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amesema kwamba Jared Kushner, mkwe wa Donald Trump, na mjumbe Steve Witkoff tayari wako nchini Uswisi kabla ya mazungumzo yaliyopangwa na Iran.
Vance alisema wawili hao “wanashughulikia baadhi ya vipengele vyenye utata katika mazungumzo haya.”
“Ninavyoelewa, baada ya kuzungumza na Jared na Steve asubuhi hii, mambo yanaendelea vizuri,” Vance alisema.
Alipoulizwa kama ana mpango wa kujiunga nao, alisema anatarajia kuondoka “siku chache zijazo.”

Chanzo cha picha, EPA
Ujumbe wa Iran ukiongozwa na spika wa bunge waondoka kwenda Uswisi
Ujumbe wa Iran, unaoongozwa na spika wa bunge Mohammad Bagher Ghalibaf, sasa umeondoka kwenda Uswisi, vyombo vya habari vya serikali vinaripoti.
Abbas Araghchi, waziri wa mambo ya nje wa Iran, pia anahudhuria mazungumzo hayo pamoja na maafisa wengine wakiwemo wawakilishi wa usalama wa taifa, benki kuu na mafuta.
Naibu waziri wa mambo ya nje Kazem Gharibabadi na msemaji wa wizara ya mambo ya nje Esmail Baghaei pia wanaripotiwa kuwa safarini.
Awali, Baghaei alisema kwamba Iran itaidai Marekani "itimize ahadi zake".
Soma zaidi:






























