Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Trump aingiza zaidi ya dola bilioni moja kutokana na sarafu za kidijitali tangu arejee madarakani

Katika ripoti hiyo yenye kurasa 927, Trump amesema alipata dola milioni 635 kutokana na mrabaha wa sarafu ya kidijitali ya Trump meme coin, ambayo thamani yake imeshuka kwa kiasi kikubwa tangu ilipozinduliwa siku tatu kabla ya kuapishwa kwake.

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Kombe la Dunia: Ivory Coast yaaga, Afrika yasalia na timu saba

    Ivory Coast imekuwa timu ya pili ya Afrika kuondolewa katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia baada ya kufungwa mabao 2-1 na Norway, na kuziacha timu saba za bara hilo zikiendelea na harakati za kutinga hatua ya 16 bora.

    Kuondolewa kwa Ivory Coast kunaiunganisha na Afrika Kusini, ambayo iliaga hatua hiyo mapema, huku Tunisia ikiwa ilitolewa katika hatua ya makundi.

    Katika mechi nyingine zilizochezwa usiku wa kuamkia leo, Ufaransa ilitinga hatua ya 16 bora baada ya kuichapa Sweden mabao 3-0, wakati Mexico nayo ilifuzu kwa kuishinda Ecuador mabao 2-0, asubuhi hii.

    Sasa matumaini ya Afrika yapo kwa timu saba zilizobaki kwenye mashindano hayo.

    Usiku wa leo saa moja usiku, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) itavaana na England, huku saa tano usiku Senegal ikikabiliana na Ubelgiji kuwania nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora.

    Ratiba ya Ijumaa inaonyesha Algeria ikicheza dhidi ya Uswisi, wakati Misri itavaana na Australia.

    Maelezo zaidi:

  2. Seneta wa Marekani ataka tathmini mpya ya uhusiano wa kiusalama na Uganda baada ya kufungwa kwa vyombo vya habari

    Baada ya kufungwa kwa vyombo vya habari Seneta wa Marekani, Jim Risch, ametaka kufanyika kwa mapitio ya uhusiano wa kiusalama kati ya Washington na Uganda.

    Risch, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Marekani inayoshughulikia Masuala ya Nje, amesema Uganda huenda isiwe mshirika anayefaa kufuatia kufungwa kwa baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni kwa agizo lililoidhinishwa na Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Muhoozi Kainerugaba.

    “Marekani inahitaji kupitia upya uhusiano wake wa kiusalama na Uganda. Mashambulizi ya Jenerali Muhoozi Kainerugaba dhidi ya uhuru wa kujieleza, yakiwemo ya kufunga taasisi kubwa za habari mwishoni mwa wiki hii, yanamfanya yeye pamoja na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda kuwa washirika wasiofaa.''

    Tunapaswa kushirikiana tu na wale wanaoimarisha usalama wa kikanda, si wanaoudhoofisha,” Risch aliandika kwenye ujumbe wake katika mtandao wa X almaarufu Twitter.

    Soma zaidi:

  3. Trump aingiza zaidi ya dola bilioni moja kutokana na sarafu za kidijitali tangu arejee madarakani

    Rais wa Marekani Donald Trump aliingiza zaidi ya dola bilioni moja kupitia shughuli zinazohusiana na sarafu za kidijitali mwaka jana, kwa mujibu wa ripoti yake ya lazima ya mwaka 2025 ya kutangaza mali zake.

    Katika ripoti hiyo yenye kurasa 927, Trump amesema alipata dola milioni 635 kutokana na mrabaha wa sarafu ya kidijitali ya Trump meme coin, ambayo thamani yake imeshuka kwa kiasi kikubwa tangu ilipozinduliwa siku tatu kabla ya kuapishwa kwake.

    Pia amesema alipata zaidi ya dola milioni 500 kutoka World Liberty Financial, kampuni ya sarafu za kidijitali iliyoanzishwa na wanawe pamoja na watoto wa mjumbe wake maalum wa Mashariki ya Kati, Steve Witkoff.

    Mbali na hilo, Trump alipata mamilioni ya dola kupitia biashara za mali isiyohamishika na bidhaa zinazobeba jina la Trump.

    Hata hivyo, Ikulu ya White House imekanusha kuwa Trump ananufaika kifedha kutokana na urais wake.

    Mapato yaliyoorodheshwa katika ripoti hii mpya ni makubwa zaidi kuliko yale aliyotangaza mwaka 2024, aliposema alikuwa ameingiza zaidi ya dola milioni 600.

    White House pia ilikanusha kuwapo kwa mgongano wa maslahi, ikisema Trump alihamishia biashara zake kwenye mfuko wa amana unaosimamiwa na wanawe.

    Naibu msemaji wa White House, Anna Kelly, amesema rais huyo ameifanya Marekani kuwa "kitovu cha dunia cha sarafu za kidijitali."

  4. Hujambo natumai umzima.