UEFA yatishia kususia Kombe la Dunia iwapo mipango ya FIFA itaidhinishwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Mpango wenye utata wa FIFA wa kuuza hisa katika mashindano yake kwa wawekezaji binafsi umepata pigo kubwa. Mashirikisho 41 ya soka kutoka Amerika Kaskazini, Amerika ya Kati na Caribbean yameukataa mpango huo, yakijiunga na upinzani wa pamoja wa mashirikisho yote ya Ulaya.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino, anasisitiza kuwa mpango huo ungeongeza kwa kiasi kikubwa ufadhili kwa mashirikisho ya soka ya kitaifa duniani kote.
Mataifa yote 55 ya soka ya Ulaya yamekubaliana kususia Kombe la Dunia iwapo FIFA itatekeleza mpango huo. UEFA imesema timu zake zitashiriki katika mashindano ya FIFA tu iwapo mpango huo hautatekelezwa.
Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa dharura wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA). Laura McAllister ni makamu wa rais wa Shirkisho la Soka Barani Ulaya.
"Hatua ni wazi kabisa ni kitisho kwa mchezo wa soka kwa sababu pale tu utakapouza hisa kwa wawekezaji binafsi kwenye mpira ni wazi kabisa inatoa picha tofauti kabisa na msukumo wa tofauti kwa wale ambao ni ni wasimamizi wa Mchezo husika" alisema Laura.
Uwezekano wa timu za Ulaya kujiondoa katika mashindano ya FIFA huenda ukawakatisha tamaa wawekezaji wa mradi huo wa kuuza hisa katika mashindano yake kwa wawekezaji binafsi chini ya Rais wake Gian Infantino, kwa kuwa timu za Ulaya ndizo zinazotawala mchezo wa soka.
Soma Zaidi:

























