Je, vitamin D inaweza kumkinga mtu asiambukizwe na mafua?

Watu walio na mafua
Maelezo ya picha, Watu walio na mafua
Iliyochapishwa

Ushapatwa na mafua ya pneumonia? basi si wewe peke yako, wewe ni miongoni mwa asilimia 70 ya watu waliougua mafua au pneumonia nchini Uingereza.

Lakini utafiti mpya unaonyesha kuwa watu milioni 3 huenda wakapata kinga ya mafua ikiwa watatumia vidonge vya Vitamin D.

Hiyo ni mara mbili ya watu ambao hupata kinga ya mafua kwa kupata chanjo.

Wale waliofanya utafiti huo wanataka Vitamin D kuongezwa kwa chakula ili kila mmoja aweze kupata vitamin hiyo.

Aina mbali mbali za vidonge
Maelezo ya picha, Aina mbali mbali za vidonge

Wataalamu pia wanawashauri watu kujaribu kuchukua hatua ambazo zitawakinga kutokana na mafua.

Mafua ni virusi ambavyo husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine, na njia kuu ya kuzuia ni kutowakaribia watu walio wagonjwa wanaokohoa.

Mwangaza wa jua
Maelezo ya picha, Mwangaza wa jua

Vitamin D wakati mwigine inafahamika kama "sunshine vitamin" kwa sababu mara nyingi hupatikana kutokana na jua .

Kutokana na hali ya hewa ilivyo nchini Uingereza watu hawapati vitamin hiyo kutoka kwa jua kati ya mwezi Oktoba na Machi.