Tooro kumpata Mfalme mpya

Maelezo ya video, Tooro kumpata Mfalme mpya
Tooro kumpata Mfalme mpya
Iliyochapishwa

Mwanmfalme Edward Rukidi Kijanangoma Nyabongo II, anayetarajiwa kutawazwa kuwa mfalme wa Ufalme wa Tooro nchini Uganda baadaye leo, amekuwa mtu anayefahamika kwa muda mrefu nchini humo.

Kwa Waganda wengi, hakufahamika kama mrithi wa kiti cha ufalme, bali kama msimulizi, mtangazaji na mhariri wa muda mrefu katika shirika la utangazaji la serikali.

Lakini sasa Kijanangoma, mwenye umri wa miaka 56, amekuwa chanzo cha habari, huku kupanda kwake kwenye kiti cha ufalme wa Tooro kukizua utata na hisia mbalimbali ndani na nje ya Uganda.

Bosha Nyanje anaelezea zaidi.