Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nyota 10 wa soka ambao huenda wanacheza Kombe la Dunia kwa mara ya mwisho
- Author, Aadam Patel
- Nafasi, Football reporter
- Iliyochapishwa
- Muda wa kusoma: Dakika 6
Huku awamu za muondoano zikiendelea, hawa hapa ni wachezaji 10 bora ambao huenda wanacheza Kombe lao la Dunia kwa mara ya mwisho.
1) Lionel Messi, Argentina - Matokeo bora: Mshindi (2022)
Uamuzi wa Messi kutoacha soka la kimataifa mwaka 2022 baada ya kushinda Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 35 unaonyesha wazi utu na tabia yake.
Akiwa na umri wa miaka 39 sasa, Messi anaendelea kuvunja rekodi moja baada ya nyingine katika michuano hii. Hakuna mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia kuliko Messi, ambaye amefunga mabao 19 na kutoa pasi nane za mabao.
Kwa sasa, amefunga mabao katika mechi saba mfululizo za Kombe la Dunia.
Mwaka 2014, alishinda mpira wa dhahabu kama mchezaji bora wa michuani hiyo wakati Argentina iliposhindwa katika fainali na Ujerumani. Alishinda tena tuzo hiyo 2022, na kuiongoza nchi yake kushinda kombea la kwanza la Dunia tangu mwaka 1986.
Hii ni mara yake ya sita kushiriki michuano ya Kombe la Dunia, pamoja na mshindani wake Cristiano Ronaldo mchezaji pekee aliyefanikiwa kufikia viwango hivyo.
Mechi inayofuata ya Messi itakuwa leo Juni 30 ambapo ataiwakilisha Argentina katika Kombe la Dunia, baada ya kucheza zaidi ya mechi 200 ya kimataifa.
Kombe la Dunia la 2030 itakuwa tofauti kwasababu nyita huyu huenda hatashiriki.
2) Luka Modric, Croatia - Matokeo bora: Washindi wa pili (2018)
Siku ya Jumamosi, Modric, akiwa na umri wa miaka 40 na siku 291, alikua mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuweka kurekodi ya pasi ya mabao ya Kombe la Dunia.
"Anacheza kana kwamba ana umri wa miaka 20. Alikuwa mzuri sana. Ni kiongozi wetu na mchezaji wetu bora," alisema Petar Sucic, mchezaji mwenzake wa Croatia.
Na unapaswa tu kuangalia jinsi Croatia walivyofanya katika michuano miwili iliyopita ya Kombe la Dunia ili kupata ufahamu wa uwezo wake.
Mnamo mwaka wa 2018, Croatia ilishangaza ulimwengu ilipofunzo kwa fainali, ambapo walishindwa na Ufaransa, na mara ya mwisho, wakatoka nafasi ya tatu - huku Modric akitumia dakika 120 akiwa na umri wa miaka 37 dhidi ya Brazil kwenye robo fainali, hali iliyo wazi. Kwa taifa lenye watu chini ya milioni nne, michuano ya hivi majuzi ya Croatia katika Kombe la Dunia ni ya kustaajabisha.
Ni wachezaji watano pekee ambao wamecheza zaidi ya mechi 22 za Modric katika michuano mitano ya Kombe la Dunia. Alijiondoa mwaka 2006 na ni mchezaji mwingine aliyeichezea nchi yake zaidi ya mara 200.
3) Cristiano Ronaldo, Ureno - Matokeo bora: Nusu - fainali (2006)
Kombe la Dunia limesalia kuwa taji kubwa ambalo limemponyoka Ronaldo.
Hakuna mchezaji aliyecheza mechi nyingi za kimataifa (231) au kufunga mabao (145) kuliko mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41, ambaye alichezea Ureno mechi ya kwanza mwaka 2003.
Mnamo 2016, aliiongoza nchi yake katika Mashindano ya Uropa lakini hii ni mara yake ya sita kwenye Kombe la Dunia na bado hajafanikiwa kutinga hatua nne bora katika mechi yake ya kwanza mnamo 2006.
Hata hivyo, rekodi ya kufunga mabao 10 katika mechi 25 za Kombe la Dunia ni ya kuvutia na hivyo basi kuwa mtu pekee kufunga katika Kombe la Dunia sita - licha ya uamuzi wa Ureno kumchezesha kila mara kuzua gumzo la mara kwa mara.
Ronaldo anajua pengine hii ni nafasi yake ya mwisho kushinda Kombe la Dunia. "Nimerudi," alisema, baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Uzbekistan wiki iliyopita. Ndio amerudi, lakini kwa muda gani?
4) Manuel Neuer, Germany - Matokeo bora: Mshindi (2014)
Itakuwa rahisi kumhukumu Neuer kwa uchezaji wake katika wiki za hivi karibuni, ambazo zimekuwa vigumu kuzitumia kushawishi ubora wake, lakini kuna sababu kwa nini kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann alimtaka arejee katika soka la kimataifa.
Kipa wa Bayern Munich ni mmoja wa wachezaji bora zaidi wa wakati wote. Neuer, 40, alishinda Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani mnamo 2014 na Glavu za Dhahabu (Golden Glove) msimu huo wa joto. Hili sasa ni Kombe lake la tano la Kombe la Dunia na katika muda huo, ameichezea nchi yake mara 23 kwenye fainali, tangu alipojiondoa mwaka 2010.
Hatua ya Ujerumani kuondolewa katika hatua ya 32 bora inaweza kuharibu urithi wa Neuer wa Kombe la Dunia lakini atakumbukwa milele kama mshindi wa Kombe la Dunia la 2014.
5) Neymar, Brazil - Matokeo bora: Nusu- Fainali (2014)
Kitu cha kwanza kinachokujia akilini unapomfikiri Neymar katika Kombe la Dunia ni kampeni ya Brazil nyumbani mwaka wa 2014. Mchezaji huyo wa miaka 22 wakati alichangia pakubwa ufanisi wa taifa lake lilipofunga mabao manne katika michezo mitano, kabla ya mashindano yake kufikia kikomo, alipovunjika mfupa mgongoni mwake wakati wa robo fainali.
Baadaye Brazil ilifungwa mabao 7-1 na Ujerumani katika nusu fainali. Mnamo 2018 na 2022, alifunga mabao mawili katika kila mashindano, huku Brazil ikiondolewa katika hatua ya robo fainali.
Akiwa na umri wa miaka 34, licha ya changamoto za majeraha yanayomkabili tangu 2022, bado anakamia kushindia nchi yake Kombe la Dunia. Machozi yaliyomdondoka Neymar baada ya kurejea tena kwenye kikosi cha Brazil dhidi ya Scotland yaliashiria mengi.
Huenda asiwe tena mchezaji mkuu lakini ndoto yake ya utotoni bado ni uwezekano kuwa mchezaji mwenye mabao manane na pasi nne za mabao katika michezo 14 ya Kombe la Dunia.
6) Kevin de Bruyne, Ubelgiji - Matokeo bora: Nusu fainali (2018)
De Bruyne alikuwa sehemu ya Kizazi mahiri cha Ubelgiji ambacho hakikufanikiwa. Baada ya kundolewa robo fainali mwaka wa 2014 na kushindwa nusu fainali mwaka wa 2018 kabla ya Ubelgiji kutolewa katika hatua ya makundi mwaka wa 2022.
Kikosi cha Rudi Garcia kitacheza dhidi ya Misri katika raundi ya 32, akijua kwamba mechi dhidi ya Marekani inasubiriwa.
Sasa akiwa na umri wa miaka 35, De Bruyne anacheza katika Kombe lake la Dunia la nne na amefunga mabao matatu kati ya hayo, akiwa na pasi nne za mabao, katika mechi 16.
7) Virgil van Dijk, Uholanzi - Matokeo bora: Robo fainali (2022)
Huenda ikashangaza kwamba Van Dijk ameichezea nchi yake mara nane pekee kwenye Kombe la Dunia lakini Uholanzi haikufuzu dimba la 2018 - mwaka ambao alihamia Liverpool.
Waholanzi hao walifanya vyema mnamo 2022, ambapo walitolewa kwa mikwaju ya penalti na washindi Argentina katika robo fainali. Na katika muda wa mechi tatu mwaka huu, tayari walikuwa wamefunga mabao mengi kama walivyofunga katika mechi tano nchini Qatar - ingawa pia walikuwa wameruhusu kiwango sawa na 2022 pia.
Van Dijk, nahodha wa Uholanzi, alifungua dimba lake kwa bao lakini lilimalizika kwa kushindwa kwa mikwaju ya penalti na Morocco katika hatua ya 32 bora.
Je, hii itakuwa mara ya mwisho kwa Van Dijk kucheza Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 34?
8) Mohamed Salah, Misri - Matokeo bora: Hatua ya 32 (2026)
Wakati Misri ilipoilaza New Zealand kwa timu zote ilijihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya 32 bora, ulikuwa ni ushindi wao wa kwanza wa Kombe la Dunia tangu 1934 na Salah alikuwa kiungo muhimu katika ufungaji wa bao la kipindi cha pili na pasi ya mabao.
Hii ni mara ya pili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kushiriki kwenye michuano hiyo, huku Misri ikifuzu mwaka 2018, kumaliza ukame uliodumu kwa miaka 38, kabla ya kukosa 2022.
Katika Kombe la Dunia lililoandaliwa nchini Urusi, Salah alifunga mabao mawili lakini taifa lake lilipoteza mechi zake zote mitatu ya makundi. Amefunga jumla ya mabao matatu na kusaidia kufumba mara mbili katika mechi tano katika Kombe la Dunia.
Misri ikiongozwa na Salah itamenyana na Australia siku ya Ijumaa kuwania nafasi ya 16 bora ambayo inaweza kumfanya akabiliane na Messi.
9) Son Heung-min, Korea Kusini - Matokeo bora: 16 Bora (2022)
Hakuna mchezaji wa Korea Kusini aliyefunga mabao zaidi ya Son (matatu) kwenye Kombe la Dunia au kucheza mechi nyingi za Kombe la Dunia (13) kuliko mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33. Lakini Kombe hili la Dunia tayari limekwisha kwa nchi yake.
Mchezaji huyo wa zamani wa Spurs anaweza kupata kibarua kingine katika kipindi cha miaka minne lakini hana nguvu tena kama alivyokuwa hapo awali, kama inavyoonyeshwa na maonyesho yake ya hatua ya makundi, ambapo alishindwa kufunga au kupata pasi. Son aliondolewa kwenye kikosi cha kwanza cha XI kwa mchezo wa mwisho wa kundi.
Nahodha huyo wa Korea Kusini amecheza Fainali nne za Kombe la Dunia na ubora wake unabaki 2018, ambapo alifunga dhidi ya Mexico na Ujerumani lakini yeye na raia wake wameshindwa kukaribia kiwango kilichowekwa na timu ya 2002 iliyofika nusu fainali kwenye ardhi ya nyumbani.
10) Sadio Mane, Senegal - Mwisho bora: 16 Bora (2022)
Kabla ya 2018, Senegal ilicheza peke yake kwenye Kombe la Dunia mwaka wa 2002. Wakiwa na Mane wamefuzu kwa Fainali tatu zilizopita za Kombe la Dunia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alifunga bao lake pekee la Kombe la Dunia hadi sasa mnamo 2018 lakini jeraha la goti lilimfanya asishiriki michuano ya 2022, wakati Senegal ilitolewa katika hatua ya 16 bora.
Hiyo ilikuwa baada ya kufunga penalti ya ushindi dhidi ya Misri katika mechi ya mchujo na kuisaidia nchi yake kufuzu kwa michuano hiyo nchini Qatar.
Kama Salah, huenda isiwe rahisi kumuona mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool kwenye mashindano ya 2030. Senegal itamenyana na Ubelgiji siku ya Jumatano kuwania kufuzu hatua ya 16 bora.