Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Tottenham inamfukuzia Rashford
Tottenham wameonyesha nia ya dhati ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford iwapo wataendelea kusalia ligi kuu, huku kukiwa na taarifa kwamba Barcelona ina mashaka ya kumfanya nyota huyo wa England kuwa mchezaji wa kudumu baada ya mkopo wake.(Sport - in Spanish)
Winga wa England Anthony Gordon huenda akaondoka Newcastle dirisha la majira ya kiangazi, huku uwezekano wa kuondoka kwake ukionekana kuongezeka.(Athletic - subscription required)
Chelsea wameanza mawasiliano ya awali na kocha anayeondoka Bournemouth, Andoni Iraola, kuhusu nafasi yao ya ukocha. (Football London)
Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal Andrea Berta alikuwapo Istanbul Jumapili kuitazama Galatasaray, huku kukiwa na tetesi kuwa klabu hiyo inamfuatilia mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen.(AS - in Spanish)
Jose Mourinho anaweza kurejea Real Madrid kwa muhula wa pili kama kocha mkuu majira ya kiangazi, huku akitajwa kuwa chaguo linalopendelewa na rais Florentino Perez.(Athletic - subscription required)
Liverpool wanatumaini uhusiano wao mzuri na RB Leipzig utawasaidia kumsajili mapema mshambuliaji wa Ivory Coast Yan Diomande mwenye umri wa miaka 19.(Football Insider)
Liverpool pia wanamfuatilia beki wa Napoli Sam Beukema, huku kocha Arne Slot akivutiwa kwa muda mrefu mlinzi huyo wa Uholanzi. (Teamtalk)
Mshambuliaji wa Feyenoord Ayase Ueda ameongezwa kwenye orodha ya washambuliaji wanaotakiwa na Everton, huku Leeds, Tottenham na Brighton nazo zikimtaka nyota huyo wa Japan.(Teamtalk)
Valencia wanataka winga wa Ubelgiji Largie Ramazani asajiliwe moja kwa moja kutoka Leeds baada ya kuvutia wakati wa mkopo wake La Liga.(ElDesmarque - in Spanish)
Everton wanajiandaa kumwania beki wa Manchester City Nathan Ake majira ya kiangazi, huku mchezaji huyo wa Uholanzi akitafuta nafasi zaidi ya kucheza. (Football Insider)
Newcastle na Aston Villa wanamfuatilia Maxi Araujo wa Sporting, ambaye ana uwezo wa kucheza beki wa kushoto na winga wa kushoto.(Sport Witness)