Tazama: Polisi walivyokabiliana na mashabiki wa PSG jijini Paris
Tazama: Polisi walivyokabiliana na mashabiki wa PSG jijini Paris
Iliyochapishwa
Makabiliano kati ya mashabiki wa soka na polisi kote nchini Ufaransa yamesababisha zaidi ya watu 400 kukamatwa kufuatia ushindi wa Paris Saint-Germain (PSG) kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal.
Maelfu ya maafisa walitumwa kuzuia machafuko yaliyotatiza huduma za mabasi, treni na reli katika mji mkuu Paris.
Polisi walirusha vitoa machozi kutawanya umati wa watu katikati mwa jiji huku baadhi yao wakijeruhiwa katika vurumai hilo.
Vurugu sawa na hizo zilishuhudiwa wakati PSG iliposhinda kombe hilo mwaka jana, ambapo sherehe za ushindi ziligeuka kuwa machafuko.
Waziri wa Mambo ya Ndani Laurent Nuñez amasema mwaka huu, mamlaka ilikuwa imejiandaa vilivyo kudhibiti tukio kama hili likijitokweza.



