Aina mpya ya ugonjwa wa kisukari unaowapasua vichwa wataalamu

Madaktari walimwambia Noella alikuwa na kisukari aina ya 5, ambayo huwaathiri vijana hususan wale walio na uzani mdogo sana.
Maelezo ya picha, Madaktari walimwambia Noella alikuwa na kisukari aina ya 5, ambayo huwaathiri vijana hususan wale walio na uzani mdogo sana.
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 6

Madaktari walipomchoma Noella Mukumbi sindano ya insulin mara ya kwanza, walidhani wananusuru maisha yake. lakini mwanamke aliye na umri wa miaka 30- kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo anasema tiba hiyo ilimfanya ajihisi kana kwamba anafariki dunia.

Noella, msusi na mama wa wattoeo wawili, alipatikana na kisukari aina ya type 1 mwaka 2023, lakini kuna kitu ambacho hakikuwa sawa.

Anasema alipoanza kutumia sindano ya insulin ya kila siku, alipatwa na kisunzi na kukosa uwezo kudhibiri mwili wake. Siku moja alizimia.

"Nilikuwa nawafulia nguo wanangu lakini nume wangu alinipata sakafuni kipiga mayowe," aliiambia BBC.

Maiaka mitatu baadaye wataalamu walimwambia huenda ana kisukari aina ya type 5.

Ugonjwa wa kisukari, unaoathiri zaidi ya watu milioni 830 kote duniani, humpata mtu wakati mwili unaposhindwa kudhibiti ipasavyo sukari ya damu kupitia insulini, kumaanisha kwamba viwango vinaweza kuwa juu na hatarisha hali ya afya.

Kisukari ya type 5 ni aina ya ugonjwa unaoaminika kutokana na lishe duni kwa muda mrefu, haswa utotoni na ujanani.

Shirikisho la Kimataifa la Kisukari (IDF), ambalo linajumuisha vyama 251 vya kitaifa vya kisukari, lililitambua rasmi aina hiyo ya kisukari mwaka jana.

Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) halitambui hali hii, kwa sababu bado hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kwamba ni aina tofauti ya ugonjwa huo.

Wanasayansi wengine wanaamini kuwa kisukari aina ya type 5 inaweza kuathiri hadi wagonjwa milioni 25, na wanaonya kuwa kuichanganya na aina nyingine ni hatari.

Dk. Meredith Hawkins, mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Duniani katika Chuo cha Tiba cha Albert Einstein, anaamini kwamba uainishaji mbaya ni "tatizo lililoenea sana" ambalo husababisha vifo kutokana na tiba duni ya insulini.

"Baadhi ya wagonjwa tuliotangamana nao mara kwa mara hawakuamka tena siku iliyofuata," anasema.

Aina ya 5 ya kisukari

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kisukari kinatokea wakati kongosho haizalishwi au haifanyi kazi ipasavyo, hivyo kusababisha sukari kujilimbikiza katika damu.

Katika aina ya kwanza (Type 1) kisukari kinatokea wakati kongosho haizalishwi au haifanyi kazi ipasavyo, hivyo kusababisha sukari kujilimbikiza katika damu.

Na katika aina ya 2 (Type 2), kinatokea kongosho inapokuwa haitoi insulini ya kutosha au homoni haifanyi kazi vizuri.

Hata hivyo, wanasayansi wanasema kwamba aina ya 5 ya kisukari inaweza kuhusishwa na utapiamlo wa muda mrefu, unaoathiri ukuaji wa kongosho, chombo kinachozalisha insulini.

Wagonjwa hawa bado wanaweza kutoa insulini, lakini haikidhi mahitaji ya mwili.

Kutokana na hali hiyo, tiba ya kawaida ya kisukari hayafanyi kazi inavyostahili, wakati mwingine, inaweza kuwa na madhara.

Hata kipimo kidogo cha insulini kinaweza kusababisha hypoglycemia (wakati viwango vya sukari ya damu hupungua kupita kiasi), ambayo inaweza kusababisha kifo.

Sawa na aina nyingine ya kisukari, aina ya 5 ya ugonjwa huo inaweza kusababisha matatizo makubwa, kama vile upofu, figo kushindwa kufanya kazi, na majeraha kutopona kiwango ambacho kinaweza kumanya mtu kukatwa kiungo cha mwili

Sophia, ambaye alikuwa na uzito mdogo sana katika ujana wake, anaamini kuwa ana kisukari cha aina ya 5.

Chanzo cha picha, Sophia Sharer

Maelezo ya picha, Sophia, ambaye alikuwa na uzito mdogo sana katika ujana wake, anaamini kuwa ana kisukari cha aina ya 5.

Kwa kuwa mara nyingi huathiri vijana ambao wana uzani mdogo sana na wana viwango vya juu vya sukari ya damu, ni rahisi kufikiria ni kisukari cha aina ya 1. Dalili pia zinaweza kufanana sana.

Noella, ambaye kwa sasa anaishi Uganda, anasema alikumbana na hali hiyo. Anakumbuka alikuwa amekonda sana kwa muda mrefu, na marai baada ya kujifungua mtoto wake wa pili, alianza kujisikia vibaya.

"Mdomo wangu ulikuwa mkavu kila wakati. Nilikunywa maji mengi na hata kuamka mara mbili au tatu usiku kutafuta maji," anasema.

Pia alipungua uzani kwa kasi, kutoka kilo 58 hadi 49, na alijihisi kuwa na uchovu kila wakati, dalili mbili za kawaida za kisukari aina ya 1.

''Kisukari cha uwembamba''

Kisukari Aina ya 5 ya kinawaathiri watu hasa katika sehemu za Asia na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako utapiamlo wa watoto bado umeenea.

Hata hivyo, tafiti zinaonyesha kwamba kisukari pia kinaongezeka miongoni mwa watu wenye uzani wa chini katika nchi nyingine.

Utafiti wa 2023 uliochapishwa katika Diabetes Care, kulingana na data kutoka kwa watu wazima zaidi ya milioni 2.6 wa Marekani, ulifunua kwamba viwango vya kile kinachoitwa "ugonjwa wa kisukari unaohusishwa na uwembamba" miongoni mwa watu wasio wanene kupita kiasi ilikuwa ikiongezeka.

Sophia Sharer, kutoka London, anaamini kuwa anakidhi kigezo hiki. Alikuwa na umri wa miaka 23 wakati vipimo vya kawaida vya damu vilionyesha bila kutarajiwa kuwa ana viwango vya juu vya sukari kwenye damu.

Mwanahabari huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 26, anasema alikuwa na uzito mdogo sana kwa kipindi kirefu utotoni na ujana wake, na kwamba kuna wakati alilazwa hospitalini.

Alipoanza kunenepa akiwa na umri wa miaka 19, alianza kujisikia vibaya.

"Nikiwa na njaa sana nilikuwa natetemeka sana, na nilihisi kama nitazimia."

Baada ya vipimo kudhibiti ugonjwa wa kisukari cha aina ya 1 na aina adimu za jeni za ugonjwa huo, hatimaye madaktari walimpeleka kwenye kliniki ya kisukari cha aina ya 2, anasema.

Mwanasayansi aliyehusika katika kutambua aina ya 5 alimwambia Sophia kwamba huenda ana baadhi ya sifa za ugonjwa huo.

Lakini kwa kuwa kwa sasa hakuna kipimo cha uchunguzi kinachotambulika rasmi nchini Uingereza, hali yake bado haijathibitishwa.

Utambuzi mpya

Ukosefu huu wa kipimo cha uhakika cha uchunguzi kwa sehemu unaelezea jinsi ugonjwa huo unavyotambuliwa kimataifa.

WHO iliitambua kama "kisukari kinachohusiana na utapiamlo" mnamo 1985, kabla ya kuiondoa rasmi miaka 12 baadaye, madaktari waloposhindwa kukubaliana ikiwa inatofautiana na kisukari cha aina ya 2.

Baadaye, ugonjwa huo ulitoweka kwenye vitabu vya matibabu na miongozo ya kawaida ya kliniki.

Mnamo Aprili 2025, Shirikisho la Kimataifa la Kisukari lilitambua rasmi ugonjwa huo. Utafiti uliofanywa na zaidi ya wanasayansi 50 na kuchapishwa katika jarida la Lancet mwaka jana ulichangia kutambuliwa kwake.

WHO ilisema kwamba mfumo wake wa uainishaji mwaka 1999 na 2006 "haukupata ushahidi wa kutosha wa kisayansi kuijumuisha kama aina tofauti ya kisukari."

Hata hivyo, inakubali kwamba uainishaji wake wa sasa "hauzingatii sifa za kimatibabu za visa vyote vya ugonjwa wa kisukari," na kwamba aina ya 5 inaweza kurejeshwa katika miongozo yake katika siku zijazo, "mradi tu kuna ushahidi wa kutosha" ili kuijumuisha kama aina tofauti.

Wanaounga mkono hoja hiyo wanadai kuwa utambuzi wa IDF pekee tayari huwasaidia wagonjwa kupokea matibabu yanayofaa zaidi.

"Afya yangu umeimarika sana"

Noella Mukumbi

Chanzo cha picha, Noella Mukumbi

Maelezo ya picha, Tangu aanze kutumia kiwango kidogo cha insulini, Noella anasema anahisi vizuri zaidi.

Mashirika kadhaa makubwa ya kimataifa, kama vile WHO na Chama cha Kisukari cha Marekani, pamoja na wanasayansi wengine, wanahoji ikiwa kisukari cha aina ya 5 ni ugonjwa tofauti.

Mtaalamu wa kisukari wa India anaamini kwamba kile kinachoitwa aina ya 5 kinaweza kuwa aina ya kisukari cha aina ya 2 kwa watu wenye uzito mdogo, au aina nyingine ya kisukari cha type 1, badala ya ugonjwa tofauti.

"Ikiwa ni aina ya 5, niambie jinsi inavyogunduliwa," anapinga Dk. V. Mohan, rais wa Kituo cha Maalum cha Dk. Mohan Diabetes huko Chennai. "Nionyeshe alama."

Bila vipimo vyovyote vya uchunguzi, madaktari hutafuta mifumo kama vile utapiamlo wa utotoni, uzito mdogo wa mwili, na majibu yenye nguvu isivyo kawaida kwa insulini.

IDF sasa imeanzisha jopo kazi ili kuunda vigezo rasmi vya uchunguzi na miongozo ya matibabu.

Utafiti wa awali unapendekeza kwamba baadhi ya wagonjwa wanaweza kukabiliana na lishe bora na usimamizi makini wa dawa.

Hata hivyo, ufadhili unasalia kuwa changamoto kubwa, katika muktadha wa kupunguzwa kwa bajeti ya kimataifa ya afya na misaada ya kigeni, hata na wafadhili wakuu kama vile Marekani na Uingereza.

Na watafiti wengine wanahofia kwamba hali hiyo inaweza kuwa ya kawaida zaidi katika maeneo yaliyoathiriwa na vita, njaa, na uhaba wa chakula.

"Inaonekana tuko ukingoni mwa mzozo mkubwa wa chakula duniani," Hawkins anasema. "Hii itamaanisha habari mbaya sana kwa kizazi kijacho."

Tangu apokee uchunguzi wake uliorekebishwa, madaktari wamepunguza insulini ya Noella na kuanza kutumia metformin, tiba ambayo hutumiwa mara kwa mara kukabiliana na kisukari cha aina ya 2.

Anasema afya yake imeimarika sana: anaona vizurina uzani wake wa mwili umeanza teka kuongezeka.

"Nilijihisi mdhaifu sana," anasema. "Lakini sasa hali yangu imeimarika."