Marekani na Israel wamewaua viongozi wengi wa Iran, Je Trump anafanya mazungumzo na nani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi la Israel limeamrishwa kuwalenga maafisa wakuu wa Iran, bila kupewa idhini yoyote, amesema waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz.
Hii inajiri siku chache baada ya jeshi la Israel IDF, kuwaongeza Ali Larijani na afisa mkuu wa ujasusi Esmail Khatib katika orodha ya maafisa wakuu wa Iran ambao wameuawa na Israel.
"Waziri mkuu Benjamin Netanyahu pamoja na mimi tumeamrisha IDF kuwauwa maafisa wakuu wa Iran baada ya kupewa taarifa ya ujasusi bila kusubiria idhini yoyote" Alisema Katz
Ila viongozi hawa walikuwa na nguvu gani katika utawala wa Iran? na nani anashikilia usukani kwa sasa?Hivi ndivyo utawala wa Iran umebadilika kufikia sasa
Ayatollah Ali Khamenei - Kiongozi mkuu wa awali

Chanzo cha picha, IRANIAN LEADER PRESS OFFICE / HANDOUT via Getty
Kuuawa kwa kiongozi mkuu wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei kuliwashtuwa wengi, haswa kwasababu ilikuwa siku ya kwanza ya vita baada ya mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Kiongozi huyo aliyekuwa na miaka 86 aliongoza kwa miongo mitatu baada ya kumrithi Ayatollah Ruhollah Khomeini ambaye alianzisha taifa la kiislamu la Iran.
Khamenei aliongoza wizara zote na alikuwa mkuu wa majeshi ya ya Iran ikiwemo jeshi la mapinduzi la Revolutionary Guard.
Ingawa hakuwa kiongozi wa kiimla, alikuwa na nguvu za kubadilisha sera zozote za umma na kuwachagua maafisa wakuu.
Alikuwa msuluhuhishi wa tofauti za kisiasa na wakati mwingine hakupenda kujihusisha na siasa ila hakurushu sera ambazo hazimpendezi kupitishwa.
Mojtaba Khamenei - Kiongozi mkuu wa Iran

Chanzo cha picha, NurPhoto via Getty Images
Mojtaba Khamenei hajaonekana hadharani, kurekodiwa wala kupigwa picha tangu alipotajwa kuwa mrithi wa baba yake tarehe 8 Machi 2026.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, alisema bila kutoa ushahidi kwamba kiongozi huyo alikuwa "amejeruhiwa na huenda akawa ameharibika sura" katika mashambulizi ya tarehe 28 Februari mjini Tehran yaliyowaua wazazi wake na ndugu yake.
Katika hotuba yake ya kwanza kama kiongozi mkuu, iliyosomwa kama taarifa kwenye televisheni ya serikali tarehe 12 Machi, Khamenei aliapa kuendelea kufunga Mlango wa Hormuz kwa usafirishaji wa kimataifa hatua inayozuia takriban asilimia 20 ya usambazaji wa mafuta duniani na akaongeza kuwa serikali yake "haitaacha kulipiza kisasi damu" ya raia waliouawa katika vita.
Ali Larijani - Kiongozi wa baraza la ulinzi aliyeuawa.

Chanzo cha picha, COURTNEY BONNEAU/Middle East Images/AFP via Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ali Larijani, mwenye umri wa miaka 68, aliuawa katika shambulizi la Marekani na Israel katika eneo la Pardis, mjini Tehran, tarehe 17 Machi 2026, pamoja na mwanawe na mmoja wa wasaidizi wake. Anachukuliwa kuwa afisa wa juu zaidi wa Iran kuuawa tangu kifo cha Khamenei.
Akiwa kamanda wa zamani wa jeshi la mapinduzi (Revolutionary Guards), alipata umaarufu kama mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), nafasi aliyoshikilia kwa muongo mmoja, kabla ya kuwa mshauri wa usalama wa Khamenei mwaka 2004.
Larijani alihudumu kama mkuu wa mazungumzo ya nyuklia ya Iran na nchi za Magharibi kati ya mwaka 2005 hadi 2007, lakini aliondolewa katika nafasi hiyo kufuatia kutofautiana na Rais wa wakati huo, Mahmoud Ahmadinejad. Pia alikuwa spika wa bunge la Iran kwa miaka 12, muda mrefu zaidi kuwahi kushikiliwa na mtu yeyote katika nafasi hiyo.
Aidha, Larijani alimwakilisha Khamenei katika baraza kuu la usalama wa taifa na anaaminika kusimamia ukandamizaji mkubwa usio wa kawaida uliofanywa na vyombo vya usalama, ikiwemo wanamgambo wa Basij, dhidi ya maandamano yaliyoikumba Iran mwezi Desemba 2025 na Januari 2026. Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa angalau waandamanaji 6,508 waliuawa na wengine 53,000 kukamatwa.
Ali Shamkhani - Katibu wa baraza la ulinzi aliyeuawa

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images
Mshauri wa karibu wa Khamenei na mtu muhimu katika uundaji wa sera za usalama na nyuklia za Iran, pamoja na kuwa amiri jeshi mkuu wa majini wa ngazi ya rear admiral pekee nchini humo, Ali Shamkhani aliuawa katika mashambulizi ya tarehe 28 Februari mjini Tehran.
Alikuwa amenusurika shambulizi la nyumbani kwake wakati wa vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran mwezi Juni 2025.
Wakati wa vita vya Iran na Iraq katika miaka ya 1980, Shamkhani alikuwa mmoja wa makamanda muhimu zaidi wajeshi la Mapinduzi (Revolutionary Guards).
Katika kipindi cha zaidi ya miongo minne iliyopita, alishikilia nyadhifa kadhaa muhimu ikiwemo waziri wa Kikosi cha jeshi la mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), waziri wa ulinzi, kamanda wa jeshi la majini, na katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na katika miaka ya hivi karibuni, alichukua nafasi kubwa katika kukandamiza maandamano ya umma.
Meja Jenerali Mohammad Pakpour – Kamanda wa IRGC aliyeuawa

Chanzo cha picha, Morteza Nikoubazl/NurPhoto via Getty Images
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Iran, Meja Jenerali Mohammad Pakpour pia aliuawa katika mashambulizi ya tarehe 28 Februari mjini Tehran.
Akiwa kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha jeshi la Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kwa miaka 16, alichukua nafasi ya kamanda mkuu baada ya mtangulizi wake, Hossein Salami, kuuawa katika Vita vya Siku 12.
Masoud Pezeshkian - Rais wa Iran

Chanzo cha picha, IRANIAN PRESIDENCY / HANDOUT via Getty
Masoud Pezeshkian alichaguliwa kuwa rais wa Iran tarehe 6 Julai 2024, baada ya kupita katika mchakato wa ukaguzi ulioendeshwa na Baraza la Waangalizi lenye majaji 12.
Rais huyo mwenye miaka 71, alikuwa daktari wa moyo na mwanachama wa bunge la Iran.
Tarehe 11mwezi Machi 2026, Pezeshkian alichapisha kwenye X, akithibitisha tena "ahadi ya Iran ya kudumisha amani katika eneo hilo".
Siku tano baadaye, aliita msaada wa kimataifa dhidi ya Marekani na Israel, akisema: "Tunatarajia jamii ya kimataifa ishtumu uvamizi huu na kuwashawishi wavamizi waheshimu sheria za kimataifa."
Brigedia Jenerali Gholamreza Soleimani - Kamanda wa Basij aliyeuawa
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Iran, Kamanda wa Basij, Brigedia Jenerali Gholamreza Soleimani, aliuawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel tarehe 17 Machi 2026.
Brig Gen Ahmad-Reza Radan - police chief (yuko hai)

Chanzo cha picha, Morteza Nikoubazl/NurPhoto via Getty Images
Mkuu wa Polisi, Brigedia Jenerali Ahmad Reza Radan, jukumu lake ni kutekeleza kanuni kali za kijamii na kukandamiza upinzani.
Mwaka 2023, alitangaza mpango wa Noor, unaotumia kamera za ufuatiliaji na teknolojia kutambua na kuwaadhibu wanawake wanaokiuka sheria za hijabu, ikiwa ni pamoja na kutaifisha magari na kufunga biashara.
Hivi karibuni, Radan amechukua msimamo mkali dhidi ya maandamano yanayopinga serikali, na mwanzoni mwa vita alionya kuwa vikosi vyake vitamchukulia kama "adui" yeyote atakayeingia mitaani "kwa ombi la adui."
Gholamhossein Mohseni Ejei - Jaji mkuu wa Iran
Mwezi Januari, Jaji Mkuu mwenye msimamo mkali wa Iran, Gholamhossein Mohseni Ejei, alionya kwamba hakutakuwa na "huruma yoyote" kwa wale watakaopatikana na hatia ya vitendo vya vurugu wakati wa maandamano yaliyotokea kabla ya vita.
Brig Gen Eskandar Momeni - Waziri wa Ulinzi
Brigedia Jenerali Eskandar Momeni, amekuwa waziri wa mambo ya ndani tangu mwezi Agosti 2024, ana mizizi ya katika kikosi cha mapinduzi ya kiislamu (IRGC) .
Brig Gen Esmail Qaani - IRGC Quds Force Commander (yuko hai)

Chanzo cha picha, Fatemeh Bahrami/Anadolu via Getty Images
Anajulikana katika vyombo vya habari vya Iran kama "jenerali wa Levant", Brigedia Jenerali Esmail Qaani alikua kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC mwaka 2020.
Mwaka 2012, Wizara ya fedha ya Marekani ilimwekea vikwazo kwa kusimamia misaada ya kifedha na usafirishaji wa silaha kwa vikundi vya Kikosi cha Quds katika Mashariki ya Kati na Afrika, hasa nchini Gambia.
Esmail Khatib - Waziri wa Ujasusi aliyeuawa

Chanzo cha picha, ABEDIN via EPA
Esmail Khatib aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa Iran na Rais marehemu, Ebrahim Raisi, mwaka 2021.
Alikuwa amesomea dini ya Kiislamu , na alishikilia nyadhfa mbalimbali za juu katika Wizara ya Ujasusi na Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Iran.
Pezeshkian alisema tarehe 18 Machi 2026 kwamba "kuuawa kwake kwa kinyama" katika shambulio la anga la Israel kumeiacha Iran "katika maombolezo makubwa."
Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi - Mnadhimu mkuu wa majeshi ya Iran aliyeuawa

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images
Aliuawa tarehe 28 katika mashambulizi ya anga yaliyotokea Tehran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi alikuwa amemrithi Meja Jenerali Mohammad Bagheri aliyeuawa aktika vita vilivyodumu siku 12 kati ya Iran na Israel.
Sadegh Larijani - Mwenyekiti wa baraza la kutatua migogoro
Nduguye Ali, Sadegh Larijani ni mwenyekiti wa baraza la kutatua migogoro ya kisheria kati ya bunge na baraza la waangalizi.
Abbas Araghchi - Waziri wa mambo ya kigeni

Chanzo cha picha, Karim JAAFAR / AFP via Getty Images
Kumekuwa na ripoti za mawasiliano kati ya waziri wa mambo ya kigeni Abbas Araghchi na mjumbe maalum wa Marekani Mashariki ya kati Steve Witkoff, ila mazungumzo hayo bado yangali changa.
Tarehe 15 mwezi Machi, Abbas Araghchi, aliiambia CBS kuwa Iran haijawahi "kusema wanataka mapigano kusitishwa kati ya vita vinavyoendelea kati ya Marekani na Israel"
"Hivi ni vita alivyochagua Rais Trump na tutaendelea kujilinda"
Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh - waziri wa ulinzi aliyeuawa
Waziri wa ulinzi Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh aliuawa tarehe 28 mwezi Februari katika mashambulizi mjini Tehran.
Kuwalenga viongozi wa Iran kumetimiza lengo gani?
Mpango wa Marekani na Israel ilikuwa kuvuruga uongozi wa Iran,jenerali Dan Caine anayesimamaia majeshi ya Marekani alisema siku chache tu baada ya vita hivyo kuanza.
Mwanzo wa vita hivyo, lengo kuu la Marekani na Israel ilikuwa kubadilisha utawala wa Iran. Rais Trump kupitia mtandao wake wa Truth Social alitoa wito kwa raia wa Iran "kuchukua udhibiti wa serikali yao", wito uliotiliwa mkazo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu tarehe 19 mwezi Machi alipotoa wito kwa raia wa Iran "kuwa ni wakati wao sasa"
Lakini suala la kufia dini linaonekana kuipa nguvu utawala wa Iran badala ya kuilemaza.












