Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Luke Shaw kuondoka Manchester United?
Klabu ya Luton Town inayoshiriki League One imewasiliana mara kadhaa na Arsenal kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji chipukizi wa England mwenye umri wa miaka 16, Max Dowman.
Beki wa England Luke Shaw huenda akaondoka Manchester United mwishoni mwa msimu ujao, hakuna dalili za mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba wake kwa sasa.
Wakati huo huo, kiungo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 17, Noah Ajayi, anakaribia kusaini mkataba wake wa kwanza wa kulipwa na Manchester United.
Arsenal, Brighton na Aston Villa zinaendelea kumfuatilia kiungo wa Austria mwenye umri wa miaka 17, Luca Weinhandl wa Sturm Graz, ambaye anaripotiwa kuwa anaweza kupatikana kwa ada ya takriban pauni milioni 17.
Liverpool inafikiria kumsajili mwezi Januari kiungo wa Monaco na timu ya taifa ya Senegal, Lamine Camara (22), baada ya kukosa kuhamia Chelsea siku ya mwisho ya usajili.
Tottenham Hotspur ni klabu ya karibuni zaidi kuhusishwa na mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi (33), ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Galatasaray mwezi Julai.
Arsenal pia inaendelea kufuatilia hali ya winga wa Brazil Rodrygo (25) aliyejeruhiwa akiwa Real Madrid, baada ya kuonyesha nia ya kumsajili wakati wa usajili la majira ya kiangazi.
Mshambuliaji chipukizi wa England Vincent Joseph (16) amethibitisha kuondoka Liverpool, huku akitarajiwa kujiunga na Arsenal.
Leeds United haitaharakisha uamuzi wa kugeuza mkopo wa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Jean-Matteo Bahoya (21), kuwa mkataba wa kudumu, licha ya kuwa na kipengele cha kumnunua kwa pauni milioni 19.7.
Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Anthony Martial (30), anatarajiwa kujiunga na klabu ya Malaga nchini Hispania kama mchezaji huru.
Pia unaweza kusoma: