Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Iran na Oman; Ripoti kuhusu kuikabidhi Iran njia ya kuingia mlango bahari wa Hormuz kutolewa

Katika matamshi ambayo yanaonekana kumlenga Donald Trump, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amesema kwamba taarifa ya pamoja kuhusu makubaliano hayo inakamilishwa.

Muhtasari

  • Washington Post: Trump na Hegsett watofautiana huko Camp David kuhusu kupungua kwa akiba ya makombora
  • Iran na Oman; Ripoti kuhusu kuikabidhi Iran njia ya kuingia mlango bahari wa Hormuz kutolewa

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Rais wa Nigeria aagiza nyongeza ya mishahara ya asilimia 80 kwa askari wa vyeo vya chini

    Wanajeshi wa Nigeria wanatarajiwa kupata nyongeza ya mishahara ya hadi asilimia 80 – ikiwa ni mara ya pili kwa mishahara yao kuongezwa ndani ya mwezi mmoja – kutokana na kile ambacho Rais Bola Tinubu anakitaja kuwa ni "shukrani kubwa" ya serikali kwa wale wanaopambana na vitisho vikubwa vya usalama vinavyolikabili taifa.

    Mwezi Julai, Waziri wa Ulinzi aliongeza mishahara ya kila mwezi ya askari wa ngazi ya chini kabisa kutoka dola 36 (pauni 27) hadi dola 73.

    Kufuatia uamuzi wa Rais, sasa watapokea dola 132 kuanzia mwezi Septemba.

    Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Tinubu za kudhibiti vurugu zinazosababishwa na makundi mbalimbali yenye silaha, yakiwemo makundi ya wapiganaji wa Kiislamu na magenge ya uhalifu yanayojihusisha na utekaji nyara, ambayo kwa ndani yanajulikana kama "majambazi".

    Mwezi uliopita, aliamuru kuajiriwa kwa wanajeshi wa ziada 28,000 na kuanzishwa kwa vikosi vipya vinne vya jeshi.

    Hali ya ukosefu wa usalama inayoendelea nchi nzima imekuwa suala kuu la kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027.

  2. Washington Post: Trump na waziri wake watofautiana huko Camp David kuhusu kupungua kwa akiba ya makombora

    Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri wa Ulinzi Pete Hegsett walitofautiana kuhusu kupungua kwa akiba ya makombora na risasi za jeshi la Marekani wakati wa mzozo na Iran, katika mkutano wa maafisa wakuu wa serikali uliofanyika wikendi huko Camp David.

    Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, katika mkutano huo, Bw. Trump alimtaka Pete Hegsett kuelezea sababu ya kupungua kwa kasi kwa akiba ya silaha zenye usahihi wa hali ya juu na makombora ya masafa marefu, huku akionyesha wasiwasi kuhusu utayari wa kijeshi wa nchi hiyo kwa ajili ya mzozo unaoendelea.

    Ripoti hiyo inakuja baada ya vyombo vya habari vya CBS News na Reuters kuripoti hivi karibuni—vikinukuu vyanzo visivyotajwa majina—kwamba Marekani imetumia karibu akiba yake yote ya makombora ya masafa marefu yenye usahihi wa hali ya juu, ikiwemo mfumo wa makombora ya kimkakati ya jeshi la nchi kavu (ATCM) na makombora ya mashambulizi yenye usahihi wa hali ya juu, wakati wa operesheni yake ya kijeshi dhidi ya Iran iliyopewa jina la "Epic Fury."

    Ripoti hizo pia zinaonyesha kuwa akiba ya makombora ya kulinda anga aina ya Patriot na THAAD imepungua kwa kasi inayozidi uwezo wa uzalishaji wa viwanda vya ulinzi vya Marekani.

    Hata hivyo, maafisa wa serikali ya Marekani wamekanusha tathmini hizo. Sean Parnell, msemaji mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, amesema kuwa jeshi la Marekani "linaendelea kuwa na kila kitu kinachohitajika kutekeleza majukumu yake" na lina uwezo wa kutosha kulinda maslahi ya Marekani.

    Awali, Pete Hegsett alizitaja ripoti kuhusu kupungua kwa kutia wasiwasi kwa akiba ya silaha za Marekani kuwa "hadithi ya kubuni" na kusema kuwa akiba ya kijeshi ya nchi hiyo haijapungua, bali inaendelea kuimarishwa.

    Maafisa waliozungumza na Washington Post walidai kuwa sababu ya shambulio kubwa ambalo Bw. Trump alitishia kuifanyia Iran wiki iliyopita ilikuwa ni wasiwasi kuhusu uhaba huo wa akiba ya makombora..

  3. Mazungumzo kati ya Iran na Oman; Ripoti kuhusu kuikabidhi Iran njia ya kuingia mlango bahari wa Hormuz kutolewa

    Katika matamshi ambayo yanaonekana kumlenga Donald Trump, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amesema kwamba taarifa ya pamoja kuhusu makubaliano hayo inakamilishwa isipokuwa iwapo baadhi ya wahusika wengine wataingilia kati.

    Kulingana na ripoti, makubaliano yaliyopendekezwa yataipa Tehran udhibiti wa meli zinazoingia Ghuba ya Uajemi kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao baadhi ya wataalamu wanasema utakuwa mojawapo ya makubaliano makubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa Iran.

    Kuongezeka kwa matumaini kuhusu makubaliano hayo na uwezekano wa kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz kumesababisha bei za hisa kupanda katika masoko ya Marekani na Asia.

    Wakati huo huo, Shirika la Propaganda za Kiislamu nchini Iran limetangaza kwamba mikutano ya mitaani nchini Iran itaendelea hadi mwisho wa Safar, na, matokeo yake yatatangazwa baada ya kuidhinishwa na kiongozi mpya wa Iran, Mojtaba Khamenei.

  4. Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja