Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Iran yasema ina uwezo wa kuzishambulia meli za kivita za Marekani

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, amesema katika saa 48 zilizopita vikosi vya Iran vilifanyia majaribio kwa mara ya kwanza kombora lililotengenezwa nchini humo dhidi ya meli ya Marekani.

Muhtasari

Iran yasema ina uwezo wa kuzishambulia meli za kivita za Marekani

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Tetesi za Soka Jumanne: Chiesa kuondoka Liverpool

    Mshambuliaji wa Liverpool, Federico Chiesa, mwenye umri wa miaka 26, huenda akaondoka klabuni hapo Januari iwapo atakosa muda wa kutosha wa kucheza baada ya kurejea kutoka kwenye majeraha.. (Football Insider), external

    Winga wa zamani wa Manchester United, Jadon Sancho, yuko kwenye mazungumzo na angalau klabu mbili za Ligi Kuu ya England kuhusu uwezekano wa kujiunga nazo.(Teamtalk)

    AC Milan inapanga kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Brazil, Endrick, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Real Madrid mwezi Januari. (Calciomercato, external)

    Manchester United bado inamtaka kiungo wa Leicester City, Louis Page, mwenye umri wa miaka 18, baada ya kushindwa kumsajili siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (ESPN, external)

    Manchester City inaendelea kumfuatilia kiungo wa Atletico Madrid, Alex Baena, mwenye umri wa miaka 25, ingawa huenda klabu hiyo isifanye uhamisho wake Januari. (Football Insider)

    Liverpool na Manchester United zimewasiliana moja kwa moja na Wolves kuhusu uwezekano wa kumsajili winga mwenye umri wa miaka 18, Matheus Mane.(Ekrem Konur}

    Brentford imeanza mazungumzo ya kuongeza mkataba wa mshambuliaji wake Mjerumani, Kevin Schade, mwenye umri wa miaka 24, katika jitihada za kuzuia Arsenal kumnasa.(Teamtalk)

    Manchester United imekamilisha usajili wa kiungo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 16, Isaac Konde.(Fabrizio Romano)

    Soma Pia:

  2. Iran yasema ina uwezo wa kuzishambulia meli za kivita za Marekani

    Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Majid Ibn e Reza, amesema jeshi la Iran lina uwezo kamili wa kushambulia meli za kivita za Marekani zinazotekeleza kizuizi cha majini dhidi ya Iran.

    Kauli hiyo inakuja baada ya maafisa wa Iran kudai kuwa vikosi vyao vilishambulia meli mbili za kivita za Marekani katika Ghuba ya Uajemi kwa kutumia silaha za kushambulia meli.

    Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, amesema katika saa 48 zilizopita vikosi vya Iran vilifanyia majaribio kwa mara ya kwanza kombora lililotengenezwa nchini humo dhidi ya meli ya Marekani. Hata hivyo, wataalamu wanasema aina ya kombora lililotumika haijathibitishwa kwa uhuru.

    Kwa upande mwingine, Kamandi Kuu ya Marekani, CENTCOM, haijajibu moja kwa moja madai hayo.

    Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, CENTCOM ilisema ikiwa Iran itashambulia meli mbili za Marekani, Marekani itasababisha madhara makubwa zaidi na kuharibu meli tatu za Iran.

    CENTCOM pia imesema haitasita kulinda vikosi vya Marekani na, ikibidi, kuharibu meli za Iran.

    Soma pia:

  3. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.