Korea Kaskazini yatuhumiwa kuhusika na wizi wa sarafu za kidijitali kutoka Binance

Chanzo cha picha, Getty Images
Soko la kubadilishana sarafu za kidijitali duniani, Binance, limesema limeanza kurejesha mali zilizokuwa zimeibwa kwa watumiaji wake, baada ya mifumo yake kushambuliwa na wadukuzi, katika tukio linaloaminika kuwa mojawapo ya mashambulizi makubwa zaidi ya kimtandao kuwahi kutokea.
Sarafu za kidijitali zenye thamani ya dola bilioni 6.3 ziliibwa katika shambulizi hilo, huku shughuli za biashara kwenye jukwaa la Binance Alpha zikisitishwa kwa muda jana usiku.
Katika taarifa yake ya hivi karibuni, kampuni hiyo imesema kuwa imeahidi kufidia hasara zilizotokana na shambulizi hilo kwa kutumia fedha zake zenyewe.
Binance imesema imetenga zaidi ya dola bilioni 6.3 ili kutoa fidia kwa walioathirika na udukuzi huo.
Bado haijafahamika ni nani aliyehusika na shambulizi hilo, lakini wachambuzi wanaituhumu kundi la wadukuzi la TraderTraitor kutoka Korea Kaskazini.
Wataalamu wanasema wizi wa sarafu za kidijitali ni chanzo kikubwa cha mapato kwa utawala wa Korea Kaskazini.
Binance imesema inashirikiana na vyombo vya sheria kuwatambua wahalifu waliohusika.
Bei za sarafu za kidijitali zilishuka kufuatia taarifa hizo, huku Binance ikisitisha kwa muda huduma za kutoa fedha na
Binance imewahi kushambuliwa hapo awali
Hii si mara ya kwanza kwa Binance kushambuliwa na wadukuzi au kulazimika kusitisha huduma za kutoa fedha.
Kampuni hiyo imechukua hatua kama hizo mara kadhaa katika masoko mbalimbali kutokana na changamoto zilizoathiri shughuli zake.
Mwezi Mei 2019, soko hilo kubwa zaidi la sarafu za kidijitali duniani lilifichua kuwa lilikuwa limekumbwa na ukiukaji mkubwa wa mifumo yake ya usalama baada ya wadukuzi kuiba sarafu za kidijitali zilizokuwa na thamani ya dola milioni 41.
Kampuni hiyo ilisimamisha huduma za kutoa fedha kwa siku kadhaa.
Soma pia:

































