Waziri wa Fedha wa Marekani: Umoja wa Ulaya umejiunga na operesheni ya kuitenga Iran kiuchumi

Chanzo cha picha, EPA
Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Besant, akirejelea taarifa ya mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa kundi la G20, alitangaza kuwa "Umoja wa Ulaya umejiunga rasmi na 'operesheni ya kuitenga Iran kiuchumi'" na kwamba Marekani "inathamini msimamo wao thabiti na wa mapema."
Bw. Besant aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: "Marekani inasimama kidete pamoja na washirika wetu kuhakikisha kuwa utawala wa uhalifu wa Iran hauwezi kutumia mfumo wa kifedha wa kimataifa kufadhili malengo yake ya nyuklia, programu za silaha, na makundi ya kigaidi yanayofanya kazi kwa niaba yake."
Waziri wa Fedha wa Marekani amesisitiza kuwa "dunia inatoa ujumbe wa wazi kwa utawala wa Iran: 'Hatutaacha hadi njia ya mwisho ya uhai wa kifedha itakapokatwa.'"
Siku mbili zilizopita, Tume ya Ulaya ilitoa taarifa pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa G20 huko Asheville, ikiunga mkono vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.
























