Moja kwa moja, Iran yaonya dhidi ya meli za Marekani zinazokaribia mlango wa Hormuz

Ali Mohammadi, naibu afisa wa masuala ya kisiasa katika Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi (IRGC), akirejelea kauli za Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kudhibiti wa Lango la Hormuz, alisema: "Ikiwa ndivyo ilivyo, kwa jina la Mungu, leteni mojawapo ya meli zenu ndani ya umbali wa kilomita 100."

Muhtasari

  • Vuguvuu la kisiasa nchini Kenya Linda mwanachi lazuru Nairobi
  • Wahouthi watangaza mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya kambi ya kijeshi ya Saudia
  • Iran yaonya dhidi ya meli za Marekani zinazokaribia mlango wa Hormuz

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Vuguvuu la kisiasa nchini Kenya Linda mwanachi lazuru Nairobi

    .

    Chanzo cha picha, Photo Courtesy

    Maelezo ya picha, Linda Mwananchi

    Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anakabiliwa na kibarua kigumu cha kisiasa Jumapili hii anapojiandaa kupima umaarufu wake katika kaunti anayoiwakilisha katika Bunge la Seneti la Nairobi kwa kuandaa mkutano mkubwa wa kisiasa.

    Muungano wa kiaissa wa Linda Mwananchi unapeleka kampeni yake mjini Nairobi katika ziara kuu ya uhamasishaji inayotarajiwa kuhitimishwa kwa mkutano mkubwa katika Uwanja wa Jacaranda ambao ulikuwa maarufu na mojawapo ya ngome za kisasa za kinara wa zamani wa ODM Raila Odinga.

    Ziara hiyo ya Nairobi inayosubiriwa kwa hamu imeanza katika Kanisa Kuu la All Saints ambapo kundi hilo lilifika saa tatu asubuhi kuhudhuria ibada ya Jumapili, kabla ya vuguvugu hilo kuanza ziara katika baadhi ya masoko na maeneo yenye shughuli nyingi jijini.

    Polisi wameshika doria katika maeneo mbalimbali Jijini Nairobi hasa Katikati mwa Jiji na kwenye barabara kuu za Outering na Jogoo na vile vile katika uwanja huo wa Jacaranda.

    Kutoka kanisani, Sifuna na wafuasi wake wanatarajiwa kuelekea masoko ya Marikiti na Gikomba kabla ya kuendelea hadi Soko la Burma.

    Ratiba hiyo kisha italipeleka vuguvugu hilo katika maeneo ya Stage 17, B Centre na Manyanja, ikifuatiwa na maandamano kando ya Barabara ya Jogoo.

    Ziara hiyo imepangwa kuhitimishwa katika Uwanja wa Jacaranda mwendo wa saa nane mchana, ambapo Sifuna anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa.

    Harakati hizi za uhamasishaji jijini Nairobi zinafanyika wakati seneta huyo akijaribu kupanua wigo wa Linda vuguvugu la Mwananchi nje ya msingi wake wa uungwaji mkono unaokua, na kuonyesha kuwa vuguvugu hilo linaweza kuvutia wafuasi wengi wa kisiasa jijini.

    Sifuna amewahimiza wafuasi wake kujitokeza kwa wingi katika tukio ambalo washirika wake tayari wamelielezea kama "mama wa mikutano yote" .

    Katika ujumbe ulioshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii, Sifuna aliwasilisha ratiba ya Jumapili kama mchanganyiko wa maombi na uhamasishaji wa kisiasa, akiwataka wafuasi kutokuwa na visingizio vya kutohudhuria.

  2. Wahouthi watangaza mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya kambi ya kijeshi ya Saudia

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Wahouthi

    Kundi la Houthi la Yemen limetangaza kuwa limeishambulia kambi ya kijeshi kusini mwa Saudi Arabia kwa kutumia makombora ya balistiki na ndege zisizo na rubani.

    Yahya Saree, msemaji wa kijeshi wa kundi la Houthi, aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba shambulio hilo lililenga kambi ya Sharura iliyoko kusini mwa Saudi Arabia.

    Kwa mujibu wake, mashambulizi hayo yalilenga "ghala za silaha pamoja na vituo vya amri na udhibiti" vya Saudi Arabia.

    Bw. Saree hakutaja muda kamili wa shambulio hilo, lakini alionya kuwa kuendelea kwa hatua za kijeshi dhidi ya Yemen kungesababisha mashambulizi makali zaidi na mapana yatakayofika ndani kabisa ya ardhi ya Saudi Arabia.

  3. IRGC yaonya dhidi ya meli za Marekani zinazokaribia mlango wa Hormuz

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ali Mohammadi, naibu afisa wa masuala ya kisiasa katika Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi (IRGC), akirejelea kauli za Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kudhibiti wa Lango la Hormuz, alisema: "Ikiwa ndivyo ilivyo, kwa jina la Mungu, leteni mojawapo ya meli zenu ndani ya umbali wa kilomita 100."

    Afisa huyo mwandamizi wa IRGC alisema: "Wamarekani wanajua kuwa iwapo meli zao zitakaribia, zitakabiliwa na jibu kutoka kwa vikosi vya Iran," na bila kutoa maelezo zaidi, alidai kuwa "mfano wa tukio kama hilo umeshuhudiwa pia katika siku za hivi karibuni."

    Akizungumza katika mkutano wa usiku wa wafuasi wa serikali mjini Mashhad, alisema: "Leo... hakuna wanajeshi wa Marekani katika Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Oman, na Lango la Hormuz, wala hakuna vifaa vya Marekani vilivyowekwa katika maeneo hayo. Iwapo Wamarekani watakaribia eneo hilo lililozuiliwa, wao wenyewe wanajua nini kitawapata."

    Kulingana na yeye, "Meli yoyote inayotoka Kuwait na Bahrain, bila ubaguzi, huwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Wanamaji la IRGC, na iwapo ukiukwaji wowote utabainika, hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa."

  4. Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja