Tetesi: Atletico Madrid na Juventus zamtaka Noni Madueke
Atletico Madrid na Juventus wanatafakari uwezekano wa kumsajili kwa mkopo mwezi Januari mshambuliaji wa Arsenal na England, Noni Madueke, mwenye umri wa miaka 24. (Caught Offside)
Liverpool, Bayern Munich na Real Madrid zote zina nia ya kuimarisha safu yao ya kiungo kwa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Austria mwenye umri wa miaka 20, Paul Wanner, anayechezea PSV Eindhoven. (Teamtalk, External)
Lazio wameanza tena mazungumzo na mshambuliaji wa Argentina, Mauro Icardi, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Galatasaray, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 yuko tayari kwa uhamisho huo. (Sky Sports Italia, External)
Everton pia wamehusishwa na Icardi lakini kocha wa timu hiyo, David Moyes, anasita kuingia sokoni kutafuta wachezaji huru kwa sasa. (Football Insider External)
Crystal Palace wanalenga kumpatia kipa wa England, Dean Henderson, mwenye umri wa miaka 29, mkataba mpya. (The Athletic – Subscription Required External)
Nottingham Forest watamsajili mshambuliaji wa Shamrock Rovers, Michael Noonan, mwenye umri wa miaka 18, kwa utaratibu wa fidia ya mafunzo mwezi Januari. (Irish Mirror, External)
Inter Milan wako katika mazungumzo ya kuongeza mikataba ya mchezaji wa upande wa kushoto wa Italia, Federico Dimarco (28), na kiungo wa Uturuki, Hakan Calhanoglu (32). (Football Italia, External)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema (38), amezungumza na wachezaji wa Bayer Leverkusen huku akitafuta klabu mpya baada ya kuondoka Al-Hilal katika kipindi cha majira ya joto. (Fichajes – In Spanish, External)