Tetesi za soka Jumatano: Manchester United, Liverpool zamuwania Truffert

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanatarajiwa kupata ushindani mkali kutoka kwa Liverpool katika mbio za kumsajili beki wa kushoto wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ufaransa, Adrien Truffert (24), ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 60.
Mlinzi wa Brazil na Athletico Paranaense, Arthur Dias (19), anafuatiliwa na Barcelona baada ya hapo awali kuvutia ofa ya pauni milioni 18 kutoka Tottenham Hotspur.
Newcastle United wanaonekana kuwa mbele ya Nottingham Forest katika harakati za kumsajili kiungo wa Lyon, Tyler Morton (23). Morton ameonesha kiwango kizuri nchini Ufaransa tangu alipoondoka Liverpool mwaka uliopita.
Liverpool, Chelsea na Arsenal wote wanafuatilia maendeleo ya beki wa England Jarell Quansah (23), ambaye anaendelea kung'ara akiwa na Bayer Leverkusen.
Nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard (27), anatarajiwa kufuata nyayo za kocha Mikel Arteta kwa kusaini mkataba mpya wa muda mrefu katika Uwanja wa Emirates.
Arsenal wako tayari kufanya jaribio jipya la kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina, Julian Alvarez (26), mwezi Januari.
Inaelezwa kuwa mchezaji huyo sasa anafikiria kwa umakini uwezekano wa kuhamia klabu hiyo ya London Kaskazini.
Beki wa zamani wa Real Madrid, Dani Carvajal (34), bado hana klabu baada ya mpango wake wa kujiunga na Getafe kuvunjika.
Vigogo wa Bundesliga, Bayern Munich na Borussia Dortmund, wanamuwania chipukizi wa Tottenham Hotspur, Luca Williams-Barnett, ambaye aliichezea Spurs kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16.
Unaweza kusoma;
























