Tishio dhidi ya mwana wa Netanyahu lasababisha kuondolewa kwake MarekanI

Chanzo cha picha, Getty Images
Vyombo kadhaa vya habari vya Israel vimeripoti kuwa shirika la usalama wa ndani la nchi hiyo, Shin Bet, limethibitisha kile lilichokitaja kuwa tishio kubwa dhidi ya Yair Netanyahu, mwana wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Kwa mujibu wa ripoti hizo, tathmini ya usalama ilisababisha uamuzi wa kumhamisha Yair Netanyahu kutoka Marekani kwenda Israel pamoja na kikosi chake cha ulinzi.
Taarifa hizo zimekuja baada ya kuibuka kwa ripoti kuhusu safari yake ya dharura kutoka Florida kwenda Israel. Shin Bet haijatoa maelezo zaidi kuhusu asili ya tishio lililoripotiwa au waliotuhumiwa kuhusika.
Hivi karibuni, Benjamin Netanyahu alidai kuwa Iran ilikuwa imejaribu kumuua mmoja wa wanawe, ingawa hakumtaja kwa jina wakati huo. Ripoti za sasa zinaeleza kuwa alikuwa akimuashiria Yair Netanyahu.
Kwa upande wake, Iran imewahi kukanusha madai ya kuhusika katika njama za mauaji dhidi ya viongozi au watu mashuhuri wa kisiasa wa Marekani na Israel. Kufikia sasa, Tehran haijatoa tamko rasmi kuhusu taarifa mpya zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Israel.
Maelezo zaidi:




















