Botswana yahaha kuhusu raia wake kujiunga na jeshi la Urusi

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty
Botswana inasema kuwa takribani raia wake wanane waliokuwa wakijaribu kujiunga na jeshi la Urusi wamezuiwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Botswana, Fenyo Butal, aliambia bunge mnamo Agosti 21 kuwa alizuia raia wanane wa nchi hiyo waliokuwa na mpango wa kujiunga na jeshi la Urusi ili kushiriki katika vita dhidi ya Ukraine.
"Serikali ina wasiwasi mkubwa kuhusu visa vinavyoongezeka vyaa raia wa Botswana kusajiliwa kuipigania Urusi katika vita vya Ukraine," alisema Bw. Butal.
Aliongeza kuwa serikali ina "ripoti za kutia wasiwasi" kuhusu "ahadi za ajira, mafunzo au kazi za usalama nchini Urusi" zinazotolewa katika ngazi ya jamii, kwa lengo la kuwahadaa raia na kuwapeleka kwenye mstari wa mbele wa vita vya nchi nyingine.
"Kufikia sasa raia 22 wa Botswana wamedanganywa na mipango hii ya uajiri," alisema waziri wa mambo ya nje wa Botswana.
Aliongeza: "Tulifanikiwa kuwazuia raia wetu wanane katika viwanja vya ndege vya Siretse Khama, O.R. Tambo, na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Addis Ababa, muda mfupi kabla ya safari yao kwenda Urusi na kuwarejesha nyumbani.
"Ripoti za maelfu ya Waafrika kusajiliwa katika jeshi la Urusi kwa njia za udanganyifu na zisizo halali katika miaka ya hivi karibuni zimeibua mivutano ya kidiplomasia.''
Maelezo zaidi:





















