Watu 15 wauawa katika shambulio la bomu la Urusi kusini mwa Ukraine
Watu 15, wakiwemo watoto watatu, wameuawa baada ya Urusi kushambulia mji wa Zaporizhzhia, kusini mashariki mwa Ukraine, kwa mabomu matano ya angani, kwa mujibu wa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na huduma za dharura za nchi hiyo.
Mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya makazi, huku watu wengine wasiopungua 16 wakijeruhiwa. Mamlaka za Ukraine zinasema idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwani baadhi ya wakazi bado hawajapatikana na wanaaminika kufunikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Akizungumzia mashambulizi hayo, Zelensky alisema maeneo mengine 13 nchini Ukraine pia yalishambuliwa usiku kucha na kuahidi kuwa nchi yake itajibu hatua za Urusi.
"Majibu yetu kwa mashambulizi haya ya Urusi yatakuja," alisema Zelensky.
Mashambulizi hayo yametokea saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza makubaliano ya kuagiza dizeli kutoka Urusi.
Picha na video zilizochapishwa kutoka eneo la tukio zinaonyesha moja ya majengo ya ghorofa likiwa limeharibiwa vibaya kufuatia shambulio hilo.
Kaimu Meya wa Zaporizhzhia, Regina Kharchenko, alisema bomu lilipiga sehemu ya chini ya jengo na kusababisha ghorofa za juu kuporomoka.
"Sehemu ya chini ya jengo ilipigwa na ghorofa zilizokuwa juu yake zikaanguka," alisema Kharchenko akiwa katika eneo la tukio.
Zaidi ya wafanyakazi 80 wa huduma za uokoaji wanaendelea na operesheni ya kutafuta manusura chini ya vifusi, kazi inayotarajiwa kuendelea siku nzima.
Waokoaji wamekuwa wakisimamisha operesheni mara kwa mara ili kusikiliza sauti zozote kutoka kwa watu waliokwama chini ya vifusi, wakitumaini kupata manusura zaidi.
Maelzo zaidi: