Moja kwa moja, Trump afungua soko la Marekani kwa mafuta ya Urusi, Zelensky akerwa

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ameikosoa vikali hatua hiyo, akiitaja kuwa "uwekezaji katika vita vinavyopaswa kukomeshwa badala ya kupewa nguvu mpya."

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Wicknell Chivayo
  • Kijanangoma
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. AC Milan inamfukuzia Endrick Real Madrid

    Endrick

    AC Milan inaongoza mbio za kumsajili Endrick kwa mkopo kutoka Real Madrid mwezi Januari. Mabingwa hao wa Italia wanaamini wana nafasi nzuri ya kumpata mshambuliaji huyo wa Brazil ikiwa ataendelea kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha miamba hao wa La Liga. (La Gazzetta dello Sport)

    Arsenal imeijiunga na kinyang'anyiro cha kuwania saini ya nyota chipukizi wa Mexico, Gilberto Mora. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 17, anayeichezea Club Tijuana, ana kipengele cha kuondoka chenye thamani ya pauni milioni 21.2. Hata hivyo, Washika Bunduki wanakabiliwa na ushindani kutoka Real Madrid, Barcelona, Liverpool, Borussia Dortmund na Benfica, ambazo pia zinamfuatilia kwa karibu. (El Porvenir)

    Nottingham Forest inajiandaa kwa ofa zinazoweza kuwasili kwa Murillo wakati wa dirisha la Januari. Beki huyo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 anawindwa na Manchester United, Liverpool na Chelsea, ambazo zinaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo yake. (Teamtalk)

    Harry Kane
    Maelezo ya picha, Bayern Munich yapania kumbakiza Harry Kane

    Bayern Munich imeonyesha nia ya kumbakisha Harry Kane kwa muda mrefu zaidi Allianz Arena. Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Christoph Freund, amesema mazungumzo ya kuongeza mkataba wa nahodha huyo wa England yanaendelea vizuri na klabu ina dhamira kubwa ya kufikia makubaliano mapya. (ESPN)

    Paris Saint-Germain imeelekeza macho yake kwa Pablo Barrios, Atletico Madrid. Mabingwa hao wa Ufaransa wanaripotiwa kuwa tayari kutoa takribani euro milioni 70 ili kumnasa kiungo huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 23 katika dirisha lijalo la usajili. (Fichajes)

    Tottenham Hotspur imeongeza juhudi za kumsaka Vangelis Pavlidis. Mshambuliaji huyo wa Benfica na timu ya taifa ya Ugiriki amejumuishwa kwenye orodha ya Spurs wanapojiandaa kuimarisha safu yao ya ushambuliaji mwezi Januari. (CaughtOffside)

    Kiungo mshambuliaji wa BarcelonaDani Olmo aivutia Bayern
    Maelezo ya picha, Kiungo mshambuliaji wa BarcelonaDani Olmo aivutia Bayern

    Bayern Munich pia imejiunga na mbio za kumwania Luka Vuskovic. Beki huyo chipukizi wa Croatia mwenye umri wa miaka 19, anayehusishwa na Brighton, anatambuliwa kama moja ya vipaji vinavyochipukia kwa kasi Ulaya, huku Chelsea na Barcelona nazo zikiendelea kumfuatilia. (Teamtalk)

    Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Dani Olmo ameibuka kwenye rada za Bayern Munich, ambayo inaendelea kutathmini chaguzi za kuimarisha kikosi chake katika siku zijazo. (beIN Sports)

    Manchester United huenda ikalazimika kuingia sokoni katika dirisha la usajili la Januari kuimarisha kikosi chake, huku changamoto katika nafasi ya beki wa kushoto na ukosefu wa ubora wa kumalizia nafasi za mabao vikiongeza shinikizo la kusajili wachezaji wapya. (The Sun)

    Soma pia:

  2. Trump afoka baada ya kukosa Tuzo ya Amani ya Nobel

    Donald Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ameelezea kutoridhishwa kwake na uamuzi wa Kamati ya Nobel kutomtunuku Tuzo ya Amani ya Nobel, akielezea uteuzi wa mwaka huu kuwa "aibu na fedheha".

    Kamati hiyo ilimtangaza jaji wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, Navi Pillay, kuwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel siku ya Ijumaa. Hata hivyo, saa chache baada ya tangazo hilo, Trump aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara kwamba hajawahi kumsikia mshindi huyo.

    Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika mjini Syracuse, New York, Trump alisema uamuzi huo ni doa kwa Norway na akaonya kwamba hatua hiyo haitasahaulika kirahisi.

    Rais huyo amekuwa akieleza mara kwa mara kwamba anaamini anastahili kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel. Hii si mara ya kwanza kulalamikia uamuzi wa kamati hiyo, kwani mwaka 2025 pia alikosoa tuzo hiyo baada ya kutolewa kwa kiongozi wa upinzani wa Venezuela, María Corina Machado.

    Mwaka jana, Waziri Mkuu wa Norway, Jonas Gahr Støre, alimkumbusha Trump kwamba mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel huchaguliwa na kamati huru ya Nobel yenye makao yake nchini Norway, na sio serikali ya nchi hiyo.

    Katika hotuba yake, Trump alirudia madai kwamba alisaidia kumaliza vita nane na alikuwa karibu kusuluhisha migogoro mingine miwili, ingawa hakutoa ushahidi wa kuthibitisha kauli hizo.

    "Tuzo ya Amani ya Nobel imepoteza hadhi yake kutokana na kundi dogo la watu wenye misimamo mikali wanaopinga demokrasia na ambao, kwa mtazamo wangu, ni maadui wa ustaarabu," alisema Trump.

    Unaweza pia kusoma:

  3. Trump afungua soko la Marekani kwa mafuta ya Urusi, Zelensky akerwa

    Trump na Putin

    Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amekosoa vikali tangazo la Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu makubaliano ya kuingiza dizeli kutoka Urusi, akisema hatua hiyo ni sawa na kumpa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, "zawadi" inayochangia kuendeleza vita badala ya kuvikomesha.

    Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, Zelensky alisema makubaliano hayo yanatoa fursa kwa Urusi kuimarisha uwezo wake wa kuendeleza vita dhidi ya Ukraine, akionya kuwa mapato yatokanayo na biashara hiyo yanaweza kufadhili mashambulizi zaidi.

    Trump alitangaza kuwa Putin amekubali kusambaza tani 300,000 za dizeli mara moja kwa soko la Marekani na la kimataifa, zikifuatiwa na tani 500,000 mwezi Novemba na tani milioni moja zaidi baadaye.

    Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Wizara ya Fedha ya Marekani itasitisha baadhi ya vikwazo dhidi ya usafirishaji wa dizeli ya Urusi hadi tarehe 7 Aprili, huku vikwazo vingine, ikiwemo mali za Urusi zilizozuiliwa katika benki za Marekani, vikisalia kutekelezwa.

    Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Truth Social, Trump alisema Urusi pia inaweza kusambaza tani nyingine milioni tatu za dizeli ndani ya muda mfupi, kutegemea uwezo wa viwanda vyake vya kusafisha mafuta ambavyo vimekuwa vikilengwa katika mashambulizi ya Ukraine.

    Kwa upande wake, Putin alisema Urusi iko tayari kupeleka mafuta na bidhaa nyingine za petroli katika masoko ya Marekani na duniani, ingawa hakutaja kiwango maalum cha usambazaji.

    Akijibu tangazo hilo, Zelensky alisema Urusi "italipa deni hilo la dizeli kwa vitendo zaidi vya ugaidi," huku akitoa wito kwa Marekani kuendelea kuunga mkono juhudi za Ukraine za kulinda raia wake.

    "Tunatarajia Marekani kuonyesha msimamo thabiti katika mazungumzo yake na Urusi. Tunahitaji mazungumzo yalio na tija, sio yanayoashiria udhaifu," alisema Zelensky. alisema Zelensky.

    Soma zaidi:

  4. Natumai hujambo.