Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Comey ajisalimisha kufuatia shitaka la kumtishia Trump maisha katika chapisho la Instagram

Waendesha mashtaka wanasema picha ya ganda la bahari ya 2025 iliyowekwa na mkurugenzi wa zamani wa FBI ilikuwa wito wa vurugu dhidi ya Trump.

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Mafuta yanapanda bei ya juu zaidi tangu 2022

    Bei ya mafuta inaendelea kupanda kwa kasi ikifikia kiwango cha juu zaidi tangu vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vilipoanza mwishoni mwa Februari mwaka huu.

    Bei ya mafuta ghafi ilivuka kwa muda hadi dola za marekani 120 kwa pipa huku kukiwa na wasiwasi kuhusu muda ambao mzozo huo utaendelea.

    Hali hiiinakuja baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais wa Marekani Donald Trump alijadiliana na kundi la wakuu wa kampuni za nishati Jumanne kuhusu uwezekano wa kuendeleza kwa miezi kadhaa kizuizi cha Marekani dhidi ya bandari za Iran na usafirishaji wake.

    Iran inavuruga usafiri kupitia Mlango Bahari wa Hormuz ambapo takriban thuluthu moja ya mafuta na gesi ya dunia hupita katika nyakati za kawaida.

    Vizuizi hivyo vinaendelea kuwepo licha ya kusitishwa kwa mapigano kwa muda.

  2. Arsenal na Atletico zatoka sare ligi ya mabingwa Ulaya

    Arsenal na Atletico Madrid walifunga penalti kila mmoja katika sare ya mkondo wa kwanza iliyojaa matukio ambayo yalisawazisha nusu fainali yao ya Ligi ya Mabingwa.

    Viktor Gyokeres alishinda na kufunga mkwaju wa penalti kwa wageni dakika moja tu kabla ya kipindi cha mapumziko baada ya kuangushwa katika eneo hatari na beki David Hancko.

    Lakini Julian Alvarez alisawazisha bao hilo dakika 11 baada ya kipindi cha pili baada ya Ben white kuunawa mpira katika eneo la ulinzi wa Arsenal

    Mchezaji wa akiba Eberechi Eze alifikiria kujishindia penalti alipokanyagwa na beki wa wa Atletico Madrid Hancko ndani ya eneo hatari lakini uamuzi huo ulibatilishwa baada ya ukaguzi wa VAR.

    Mchezo huo ulianza kwa kishindo huku kukiwa hakuna upande wowote unaotaka kuona lango la mwenzake

    Lakini baada ya Gyokeres kuweka The Gunners mbele, Atletico Madrid walianza kipindi cha pili kwa kuzidisha presha.

    Ademola Lookman alimlazimisha David Raya kuokoa kabla ya Gabriel Magalhaes kuokoa shambulio laAntoine Griezmann huku wenyeji wakitafuta bao la kusawazisha.

    Atletico walipata penalti wakati mkwaju wa Marcos Llorente kutoka pembeni mwa eneo la goli ulipogonga mguu wa Ben White na kugusa mkono wake.

    Soma zaidi:

  3. Habari za hivi punde, 'Milipuko kadhaa' yaripotiwa kisikika Tehran

    Vahid Online, Jukwaa maarufu la habari za kidijitali linaloendeshwa na mwanaharakati wa Iran na mwanablogu Vahid, muda mfupi uliopita limechapisha jumbe kadhaa zinazoripoti milipuko ya kusikia mjini Tehran.

    Walioshuhudia tukio hiloi wameiambia mtandao huo wa habari kwamba milipuko hiyo ilisikika katika sehemu ya mashariki ya mji mkuu, katika wilaya za Tehran-Pars na Hakimiyah.

    Baadhi ya watu walieleza milipuko hiyo kama "shughuli za kupambana na ndege za kivita."

    BBC haijafanikiwa kuthibitisha usahihi wa ripoti hizo.

    Katika siku chache zilizopita, maafisa wa serikali za mitaa na wa kikanda nchini Iran wameripoti kufanya shughuli za kuharibu vilipuzi ambavyo havijalipuka vilivyosalia baada ya mapigano, lakini watu wanafananisha milipuko ya Alhamisi asubuhi katika eneo la mashariki mwa Tehran na sauti ya mashambulizi ya ndege za kivita.

  4. Shambulio dhidi ya wanaume wawili wa Kiyahudi mjini London ni ugaidi- Polisi

    Wanaume wawili Wayahudi wamechomwa visu katika eneo la Golders Green, kaskazini mwa London, katika tukio lililotangazwa na polisi kuwa la kigaidi.

    Wanaume hao wawili, waliotajwa kama Shilome Rand na Moshe Shine, walipatiwa matibabu katika eneo la tukio na sasa wako katika hali thabiti hospitalini, kulingana na Polisi.

    Polisi wamesema mwanaume mwenye umri wa miaka arobaini na mitano, raia wa Uingereza aliyezaliwa Somalia, alipigwa kwa bunduki ya umeme yaani Taser na polisi kabla ya kukamatwa kwa tuhuma za jaribio la mauaji. Mshukiwa huyo kwa sasa yuko rumande.

    Waziri Mkuu Keir Starmer amesema shambulio hilo la chuki dhidi ya Wayahudi ni la kusikitisha sana, akiongeza kuwa “Mashambulizi dhidi ya jamii yetu ya Kiyahudi ni mashambulizi dhidi ya Uingereza.”

    Polisi wamesema maafisa wao waliitikia tukio hilo Jumatano baada ya kupokea taarifa kuwa watu walikuwa wamechomwa visu.

    Mshukiwa huyo pia alijaribu kuwachoma visu maafisa waliokuwa wamefika eneo la tukio, lakini hakuna aliyejeruhiwa.

    Polisi walitoa picha za tukio hilo kutoka kamera zilizovaliwa na maafisa, ambapo wanasikika wakimwamrisha mshukiwa mara kadhaa alale chini kabla ya kumshambulia kwa Taser, na kisha kumuamuru aachie kisu.

    Imeelezwa kuwa mshukiwa huyo alikuwa na historia ya vurugu kubwa na matatizo ya afya ya akili.

    Wachunguzi wanaamini mshukiwa huyo huyo alihusika katika tukio jingine la awali katika eneo hilo.

    Mkuu wa Polisi wa Kupambana na Ugaidi nchini Uingereza, Laurence Taylor, baadaye alitangaza rasmi tukio hilo kuwa la kigaidi.

    Rabbi Mkuu Ephraim Mirvis, ambaye anawakilisha jamii kubwa zaidi ya Wayahudi nchini Uingereza, amesema tukio hilo “linathibitisha kuwa ukiwa Myahudi unaoonekana wazi, hauko salama na hatua zaidi zinahitajika.”

    Shambulio hilo linakuja chini ya wiki moja baada ya jaribio la uchomaji moto dhidi ya ukuta wa kumbukumbu eneo la Golders Green, na zaidi ya mwezi mmoja tangu magari ya wagonjwa yanayoendeshwa na shirika la matibabu la Kiyahudi Hatzola kuchomwa moto.

    Maelezo zaidi:

  5. Comey ajisalimisha kufuatia madai ya kumtishia Trump maisha katika chapisho la Instagram

    Mkurugenzi wa zamani wa shirika la upelelezi la Marekani, FBI, James Comey, amejisalimisha kwa mamlaka ili kukabiliana na mashtaka yanayodai kuwa picha aliyosambaza kwa muda mfupi kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa tishio kwa maisha ya Rais wa Marekani Donald Trump.

    Kesi hiyo inatokana na chapisho la mwaka 2025 kwenye Instagram lililowekwa na Comey, lililokuwa na picha ya magamba ya baharini yaliyopangwa kuunda maneno “86 47”. ni istilahi ya mtaani inayomaanisha “kuondoa”, na waendesha mashtaka wanadai kuwa inahamasisha vurugu dhidi ya Trump, rais wa 47.

    Comey alikanusha mashtaka akisema hakujua maana ya namba hizo, na ameshutumu upande wa mashtaka kwa kuwa na nia za kisiasa.

    Hii ni mara ya pili kwa Wizara ya Sheria kumfungulia mashtaka ya jinai Comey, ambaye ni mkosoaji wa muda mrefu wa Trump.

    Comey hakuweka ombi la kujitetea wala kuzungumza wakati alipofikishwa mahakamani kwa muda mfupi katika jimbo la Virginia.

    Wakili wake, Patrick Fitzgerald, alisema mkurugenzi huyo wa zamani atataka kesi ifutwe kwa misingi ya mashtaka ya kuchagua na yenye nia ya kulipiza kisasi — akidai alilengwa kwa sababu ya kuzungumza dhidi ya Trump.

    Jaji Fitzpatrick alikataa juhudi za Wizara ya Sheria kuweka masharti ya kuachiliwa kwa Comey, akisema hayakuwa ya lazima, kwa mujibu wa CBS News.

    Waendesha mashtaka wamemshtaki Comey kwa kujua na kwa makusudi kutoa tishio la kuondoa maisha ya — na kusababisha madhara ya kimwili kwa — rais, na pia kusambaza tishio hilo kati ya majimbo.

    Kila shtaka lina adhabu ya juu ya hadi miaka 10 jela.

    Katika taarifa ya video Jumanne, Comey alisema ana nia ya kupambana na mashtaka hayo.

    Chapisho lake la awali la Mei 2025 lilikuwa na picha ya magamba ya baharini ufukweni yaliyopangwa kuonyesha “86 47”, likiwa na maelezo: “Mpangilio mzuri wa magamba ya baharini wakati wa matembezi yangu ufukweni.”

    Comey alifuta picha hiyo baada ya malalamiko ya umma.

    Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashtaka dhidi ya Comey Jumatano, Trump alimuita “mtu fisadi”.

    “Niseme yeyote anayejua kuhusu uhalifu, anajua 86. Ni istilahi ya magenge ya uhalifu inayomaanisha muue. Magenge hutumia neno hilo wanapotaka kumuua mtu, wanasema ‘86 huyo’.

    Watu kama Comey ni tishio kubwa sana, nadhani, kwa wanasiasa na wengine,”

    Baadhi ya wataalamu wa sheria — pamoja na wabunge — wamehoji uzito wa mashtaka hayo.

    Comey alifutwa kazi na Trump katika muhula wake wa kwanza baada ya kuanzisha uchunguzi kuhusu uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2016.

    Tangu wakati huo, Trump amekuwa akitaka mara kwa mara kufunguliwa mashtaka dhidi yake — na mashtaka ya sasa ni jaribio la pili la utawala kufanya hivyo.

    Soma zaidi:

  6. Natumai Hujambo.