Wafcon 2026: Wawakilishi wa Afrika Mashariki Kenya wachapwa na Morocco
Chanzo cha picha, Backpage Pix
Michezo ya kandanda ya mataifa ya Afrika kwa wanawake zimeanza kutimua vumbi jana Jumapili
nchini Morocco na kuchezwa michezo miwili ya kukata utepe.
Katika
mchezo wa kwanza Algeria waliwanyuka Senegal 2-0 magoli ya dakika ya 42 na 85 huku
wenyeji Morocco wakiwanyanyasa wawakilishi wa Afrika Mashariki Kenya kwa
ushindi wa magoli 4-0.
Magoli matatu yalitiwa kimiani ndani ya dakika 32 za
kwanza la nne likafungwa dakika 2 tu baada ya mapunziko.
Leo kuna michezo miwili. Afrika Kusini itakipiga na
wawakilishi wengine wa Afrika Mashariki Tanzania saa mbili usiku kabla ya Ivory
Coast kutoana jasho na majirani zao wa Kaskazini, Burkina Faso.
Macron aitisha kikao cha dharura huku moto mkubwa wa nyika ukiendelea
Chanzo cha picha, EPA
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ataongoza kikao cha
dharura cha baraza la mawaziri leo Jumatatu huku moto wa nyika ukikaribia mji
wa Bordeaux, ulioko kusini-magharibi mwa nchi hiyo.
Wimbi jingine la joto linatarajiwa kufanya juhudi za
kudhibiti moto huo unaoendelea kuenea kuwa vigumu. Moto huo kwa sasa uko umbali
wa takribani kilomita 15 (maili 9) kutoka Bordeaux, meya wa mji huo, Thomas
Cazenave, alisema. Awali, alisema hakuna mpango wa kuwahamisha wakazi wapatao
850,000 wa mji huo.
Ufaransa imekuwa miongoni mwa maeneo yaliyoathirika
zaidi, huku hekta 42,000 zikiathirika na moto kusini-magharibi mwa nchi hiyo.
Hilo limeufanya kuwa miongoni mwa moto mkubwa zaidi wa misitu nchini humo tangu
Vita vya Pili vya Dunia.
Kwa jumla, zaidi ya watu wapatao laki mbili na ishirini
wamehamishwa katika eneo la kusini-magharibi mwa Ufaransa.
Kapteni Nicolas Braz, mmoja wa viongozi wa operesheni ya
kuzima moto, amesema moto huo ulikuwa na upepo mkali sana ukiambatana
na vimbunga vidogo”, na kuongeza kuwa ulikuwa “haueleweki na usioweza
kudhibitiwa.
Wakazi wa Le Porge, mojawapo ya miji ya pwani
iliyoathiriwa na moto huo, wameanzisha mtandao wa kujitolea wa kusaidia wazima
moto waliochoka. Wanawapikia chakula
na kuwapa mahali pa kupumzika kati ya zamu zao.
Zaidi ya nyumba 150
zimeharibiwa katika mji huo wenye wakazi 3,500.
Wakaazi wengi wanasema wamehuzunishwa
na tukio hilo ulioathiri misitu yake, wanyamapori na watu waliopoteza vitu
vingi,” alisema Augonnet.
“Kwa sasa, tunazingatia
kuchukua hatua, hivyo hatuna muda wa kufikiria sana. Nadhani sehemu yenye
changamoto itakuja baadaye, wakati wa kuanza tena ujenzi.
Wakati huo huo nchini
Uhispania, moto unaendelea kusambaa, huku zaidi ya watu 90,000 wakihamishwa
kutoka maeneo yanayozunguka Madrid na Ávila.
Takriban hekta 77,000
zimeathiriwa na moto nchini Uhispania, alisema Waziri wa muda wa Ikolojia, Sara
Aagesen, siku ya Jumapili.
Iran: Tutasitisha mashambulizi iwapo Marekani haitatushambulia tena
Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Iran ameliambia shirika la
habari la Reuters siku ya Jumapili kuwa itasitisha mashambulizi yake, mradi tu
Marekani nayo iendelee kusitisha mashambulizi yake, kulingana na afisa mmoja
mwandamiz.
Hatua hiyo imekuja baada ya
Marekani kusitisha kwa muda kampeni yake ya mashambulizi ya anga, kufuatia
washauri wa Rais Donald Trump kumweleza kuwa walikuwa wakikabiliwa na wasiwasi
kuhusu kupungua kwa akiba ya silaha za Marekani.
Baada ya usiku 13 mfululizo
wa mashambulizi makali ya anga ya Marekani dhidi ya Iran, Wizara ya Ulinzi ya
Marekani ilisisitisha operesheni hiyo mwishoni mwa Ijumaa.
Hakukuwa na mashambulizi
yoyote ya Marekani yaliyoripotiwa Jumamosi wala Jumapili.
Kwa upande wake, Iran,
ambayo ilikuwa ikijibu kila usiku wa mashambulizi ya Marekani kwa kushambulia
nchi jirani zinazohifadhi kambi za kijeshi za Marekani, pia haijafanya
mashambulizi yoyote kwa siku mbili zilizopita hadi sasa.
Afisa huyo wa Iran, ambaye alizungumza na shirika la
habari la Reuters kwa sharti la kutotajwa jina, alisema msimamo wa Tehran
unaendelea kuwa "shambulio kwa shambulio." Alieleza kuwa, "Iwapo
mashambulizi yatasitishwa, Iran pia itasitisha operesheni zake. Ujumbe huo
tayari umefikishwa kwa Marekani."
Kwa upande mwingine, Balozi wa Marekani katika Umoja wa
Mataifa, Mike Waltz, aliviambia kipindi cha Fox News Sunday pamoja na vyombo
vingine vya habari vya Marekani kuwa Rais Donald Trump aliamua kusitisha kwa
muda mashambulizi ya Marekani ili kutoa nafasi zaidi kwa juhudi za
kidiplomasia.
Akizungumza kuhusu uamuzi wa Rais Donald Trump, Balozi wa
Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, alisema:
"Antoa fursa kwa mazungumzo yaendelee; anatoa muda
kidogo ili yaweze kusonga mbele."
Maafisa wa jeshi la Marekani katika siku za karibuni
wameonya kuwa mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa katika kipindi cha wiki mbili
zilizopita, yaliyolenga kuzuia vitisho vya Iran dhidi ya usafirishaji wa meli
katika Mlango-Bahari wa Hormuz—njia ya maji ambayo imesababisha mvutano
katika vita hivyo—yalikuwa yamekaribia kumaliza maeneo lengwa yaliyokuwa
yamechaguliwa mapema kwa ajili ya kushambuliwa, kwa mujibu wa afisa mmoja wa
Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina.