Usafirishaji wa siri wa madini ya Urani kutoka Kongo
Watafiti nchini Marekani wanasema kiasi kikubwa cha madini ya urani kinachimbwa na kusafirishwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na mauzo ya madini ya kobalti, jambo linalozua wasiwasi kuhusu usalama na uangalizi wa shughuli hizo.
Watafiti hao wameripoti katika jarida la Nature Communications kuwa wanakadiria hadi tani elfu tano za madini ya urani huenda ziliondoka DRC kati ya mwaka 2000 na 2024 na chini ya asilimia kumi kutangazwa au kuwekwa chini ya ulinzi wa kimataifa.
Watafiti wanasema matokeo yao yanafichua pengo kubwa katika uangalizi wa nyuklia na mazingira, katika ufunguo wa ugavi wa mpito wa nishati duniani.
Madini ya Cobalt kutoka Ukanda wa Shaba wa DRC ni muhimu kwa magari ya umeme, simu janja na mpito mpana wa nishati. Lakini watafiti kutoka Princeton na Chuo Kikuu cha Wisconsin wanasema Urani kiasili hufungamana na cobalt na inasafiri bila kutambuliwa katika mauzo ya nje.
Wanasema baadhi ya nyenzo za mionzi pia zinaishia kwenye taka za mgodi, na kuziweka jamii katika hatari. Watafiti wanatoa wito wa ulinzi mkali wa kimataifa katika mnyororo wa usambazaji wa cobalt ili kuendana na mahitaji yanayoongezeka. BBC iliwasiliana na serikali ya DRC, lakini bado haijatoa majibu kuhusu utafiti huo
DRC, ni mzalishaji mkubwa wa kobalti duniani.
Mbali ya Kobalt nchi hiyo pia ina hazina kubwa zaidi duniani ya madini mengine ya thamani kubwa na yale muhimu, yakiongozwa kama vile, koltani, na dhahabu. Rasilimali hizi zilizoko chini ya ardhi, zenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani trilioni 24, ndizo zinazochochea masoko ya teknolojia na nishati safi duniani.
Lakini nchi hiyo imebakia katika hali ya umaskini kutokana na madini mengi kuchinmbwa kiholela bila udhibiti wa serikali na kiasi fulani kutoka na na maeneo yenye utajiri wa madini kukumbwa na vita vya muda mrefu au vinavyojirudiarudia.
Pia unaweza kusoma: