Waombolezaji Ghana waghadhabishwa kwa kufunikwa jeneza la Kofi Annan

Iliyochapishwa

Raia Ghana wanatoa heshima zao za mwisho kwa katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan kabla ya maziko Alhamisi

Annan
Maelezo ya picha, Raia Ghana wanatoa heshima zao za mwisho kwa katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan
Waombolezaji Ghana watoa heshima kwa kofi Annan
Maelezo ya picha, Mwili wake Annan umelazwa katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa Accra akitarajiwa kuzikwa Alhamisi
Waombolezaji hawakuridhishwana kufinikwa kwa majeneza
Maelezo ya picha, Vyombo vya habari Ghana vinaeleza kwamba baadhi ya waombolezaji hawakuridhishwa na hatua ya jeneza la Annan kufinikwa na kuwazuia waombolezaji kumuona kwa mara ya mwisho kiongozi huyo wa zamani.
Elders Graca Machel and Gro Brundtland
Maelezo ya picha, Mjane wa aliyekuwa rais wa kwanza afrika kusini Nelson Mandela - Bi Graca Machel na Gro Harlem Brundtland ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu nchini Norway ni miongoni mwa wanaohudhuria mazishi ya Annan
Waombolezaji Ghana watoa heshima kwa kofi Annan
Maelezo ya picha, Sehemu ya shughuli zinajumuisha maafisa kutoa heshima zao kwa jamaa na familia ya Annan.
Waombolezaji Annan
Maelezo ya picha, Hizi ndio baadhi ya picha za karibu zilizopigwa na waandishi wa BBC Ayo Bello na Mayeni Jones zinazoonyesha msafara kutoka jimbo alikozaliwa Annan- Akwamu - ukiwasili katika jumba hilo la mikutano ya kimataifa mjini Accra.
Annan UN
Maelezo ya picha, Annan, ni kiongozi wa pili wa Afrika kuishikilia nafasi ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa. Alifariki mwezi Agosti akiwa na miaka 80.