Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja , Marekani yatangaza ushuru mpya kwa washirika wake wa biashara ikiwemo China

Ushuru huo mpya unatarajiwa kuathiri washirika wakubwa wa kibiashara wa nchi hiyo, wakiwemo China, Umoja wa Ulaya na maeneo mengine 12.

Muhtasari

Marekani yatangaza ushuru mpya kwa washirika wake wa biashara

Moja kwa moja

Na Beldeen Waliaula

  1. Trump atangaza ushuru mpya kwa bidhaa zinazoingia Marekani

    Marekani imetangaza ushuru mpya, dhidi ya bidhaa zinazoingia nchini humo.

    Ushuru huo mpya unatarajiwa kuathiri washirika wakubwa wa kibiashara wa nchi hiyo, wakiwemo China, Umoja wa Ulaya na maeneo mengine 12, yakiwemo Japan, Korea Kusini na Taiwan.

    China inakabiliwa na kiwango cha juu zaidi cha ushuru, cha hadi asilimia 40, ikifuatiwa na Vietnam ambayo inaweza kutozwa hadi asilimia 35. Nchi nyingine zitatozwa ushuru wa asilimia 20 au 25.

    Mwakilishi wa Biashara wa Marekani alitangaza mapendekezo hayo ya ushuru pamoja na ripoti za kina zinazoeleza jinsi sera za biashara za kila eneo husika zinavyodaiwa kuathiri biashara ya Marekani.

    Ushuru huo mpya utaanza kutekelezwa mwaka ujao baada ya mashauriano.

    Mapendekezo hayo ya ushuru yataathiri bidhaa kutoka mataifa yafuatayo: China,Umoja wa Ulaya,Singapore,Uswisi,Indonesia,Malaysia,Cambodia,Thailand,Korea Kusini,Vietnam,Taiwan,Bangladesh,Japan, India

    Soma pia:

  2. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja Alhamisi ya leo