Vita vya Iran: Starmer akaribisha wito wa makubaliano kuelekea kufunguliwa tena kwa Hormuz
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amekaribisha "hatua iliyopigwa kuelekea makubaliano kati ya Marekani na Iran", na kuongeza kuwa ni "muhimu kwamba Iran kamwe isiruhusiwe kutengeneza silaha za nyuklia".
Akiandika kwenye X asubuhi ya leo, muda mfupi baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kuzungumza nchini India, Starmer alisema: "Tunarajia makubaliano ambayo yatamaliza mzozo na kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, kwa uhuru wa usafiri wa majini usio na masharti wala vikwazo."
Starme alisema serikali ya Uingereza itafanya "kila tuwezalo" kuwalinda Waingereza kutokana na athari za vita, akiongeza kuwa atafanya kazi na washirika wa kimataifa "kutumia furasa hii kufikia suluhisho la muda mrefu la kidiplomasia".
Soma zaidi: