Moja kwa moja, Makubaliano ya kumaliza vita vya Iran 'yamejadiliwa kwa kiasi kikubwa' - Trump

Mpango wa kurefusha muda wa usitishaji mapigano umeripotiwa na vyombo vya Habari vya pande zote mbili lakini hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Mlango wa bahari wa Hormuz 'hautarejea' ulivyokuwa kabla ya vita - vyombo vya habari vya Iran

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Chini ya makubaliano kati ya Marekani na Iran, Mlango wa bahari wa Hormuz "hautarejea katika hali yake ya kabla ya vita" linaripoti shirika la habari la Iran la Tasnim.

    Chombo hicho cha habari kilicho na uhusiano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimekuwa kikiripoti maelezo yaliyomo kwenye makubaliano hayo na Marekani asubuhi hii, lakini Marekani haijathibitisha kuhusu maelezo ya makubaliano yoyote.

    Tasnim inaripoti kwamba mlango huo wa bahari hautarudi katika "ilivyokuwa" lakini idadi ya meli zinazopita inaweza kurudi katika viwango vya kabla ya vita ndani ya siku 30.

    Hata hivyo, inaongeza kuwa Iran "inasisitiza kutumia mamlaka yake kuhusu uamuzi huo".

    Inaongeza kuwa kizuizi cha majini cha Marekani dhidi ya meli zinazoingia na kutoka bandari za Iran lazima "kiondolewa kabisa" ndani ya siku 30.

    Maelezo zaidi:

  2. Makubaliano ya kumaliza vita vya Iran 'yamejadiliwa kwa kiasi kikubwa' - Trump

    Donald Trump

    Chanzo cha picha, gett

    Rais wa Marekani Donald Trump anasema makubaliano ya kumaliza vita vya Iran "yamejadiliwa kwa kiasi kikubwa" na maelezo yatatangazwa hivi karibuni.

    Katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Socialsiku ya Jumamosi, Trump alisema makubaliano hayo yatajumuisha kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.

    Asubuhi ya leo, shirika la habari la Iran la Tasnim limesema kuwa Mlango wa Bahari utarejea katika viwango vya kabla ya vita ndani ya siku 30, na kuongeza kuwa makubaliano huenda yakasimamisha mashambulizi pande zote.

    Muda mfupi ujao tunatarajia tamko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kufuatia mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa India mjini New Delhi - unaweza kufuatilia moja kwa moja hapo juu pindi atakapoanza.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghaei aliambia televisheni ya taifa jana kuwa wawakilishi wa Marekani na Iran wamekuwa wakikutana katika wiki za hivi karibuni.

    Lakini alionya hilol haimaanishi kuwa makubaliano yatafikiwa katika masuala muhimu na kuwashutumu Wamarekani kwa kutoa "taarifa zinazokinzana".

    Trump pia alisema alikuwa na "mazungumzo mazuri" na viongozi wa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, na wengine kuhusu "Mkataba wa Maelewano unaohusu AMANI".

    Maelezo zaidi:

  3. Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.